Mapishi ya Mlenda wa majani ya maboga


Sisi tuna kitu ya msapagulo
Msusa mchanga (majani ya maboga) ukishauchambua na kuuosha (kama una mchanga, ila kuuosha unaufanya uwe mgumu), unakata mapande makubwa makubwa preferably na mikono sio kisu.
Unabandika maji kiasi jikoni, yakichemka unaweka chumvi na magadi kidogo (au baking powder) ili msusa usiwe mgumu; baadaye waweka msusa wako unafunika kidogo, ukigeuza katia nyanya moja tu, na pilipili (kwa ladha) funika kidogo then weka kinyori cha karanga (karanga iliyosagwa) kidogo sana sana, epua baada ya muda mchache hakikisha rangi ya kijani haipotei.

Waweza usiweke karanga, na bado ikawa nzuri, au ukaweka tone chache za mafuta; ila pilipili ni nzuri kwa walaji na inapendeza ikiliwa ikiwa ingali ya moto.
 

Yaani umenikumbusha mbali sana. Sisi tulizozaliwa bara tuna raha sana.
 
Yaani umenikumbusha mbali sana. Sisi tulizozaliwa bara tuna raha sana.

Wewe msukuma ndy washakukamata, maana usukumani upo mrenda mpaka wa majani makavu, mrenda pori, mrenda wa majani ya tango! Bara raha sana!
 

Hahaha, nimekukubali, kitu chukuchuku! Lakini nyanya usiweke, weka mauwa kadhaa ya maboga, na mafuta yasiwe mafuta ya dukani, ni samli mbichi! teh teh, wapi maziwa ya mgando!
 


Hahah, huyo mngoni wa kwanza umempatia kabisaa, waliokulia na kuishi ungonini waongo na wazushi kwelikweli, na wanapenda waume za watu hao...pia hawana wivu, jirani zangu ungonini alioa mke, wakati wa ujauzito akaja mdogo mtu kusaidia kazi, jamaa akasimamia show na kumpenda zaidi mdogo mtu, mke wake alivogundua akaamua kurudi kwao na kumwacha mdogo wake pale aolewe...saafi, na huwa anaffika pale kusabahi na kukumbushia gemu!...ahahahaa, Mngoni mpe pesa atafikisha lakin umpe mke/mume lazima achakachue!
 

Shukrani.
Ila kuweka magadi siyo unaua virutubishi vinavyopatikana kwenye chakula?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mrenda wa bombambili hautiwi karanga, itu chukuchuku; utakuwa umeiba sehem hii recipe! teh teh
labda kwenu bombambili hakuna karanga...
njoo mkongotema utaona kama utapeleka mlenda kwa meza usio na karanga
 
yaani hapa rafiki ndo umetupikia pitiku haswaaaaa....
na uzuri wa hii inapikwa baada ya kusongwa ugali, yaani ikiiva tu kitu kwa meza......
 
yaani hapa rafiki ndo umetupikia pitiku haswaaaaa....
na uzuri wa hii inapikwa baada ya kusongwa ugali, yaani ikiiva tu kitu kwa meza......

waoh, kumbe majina tu ndio tofauti lakini mboga ni ile ile, yaani naimagine kukiwa na manyunyu ya mvua kama sasa hivi upate ugali wa moto na hiyo pitiku ya moto iliyoongezwa nyanya chungu 3 na pilipili ya kutosha; nasahau diet kwa kweli. LOL
 
waoh, kumbe majina tu ndio tofauti lakini mboga ni ile ile, yaani naimagine kukiwa na manyunyu ya mvua kama sasa hivi upate ugali wa moto na hiyo pitiku ya moto iliyoongezwa nyanya chungu 3 na pilipili ya kutosha; nasahau diet kwa kweli. LOL
ha haaa, rafiki ugali na pitiku na nyama ya kuchoma ni diet tosha.....
umenikumbusha mbali sana. hapo napika kwa jiko la kuni na pembeni nachoma mahindi......
Pasaka itabidi niende kwa mama. maana hayo yoote huwa yanakuwepo. na maboga, lol!
 
Mimi chochote kinachoteleza mdomoni sisogeleiiiii
 
Da! Narudi Kwetu Kimbiji MBESA WIlaya Ya Tunduru Mkowa Wa Ruv Uma. Hivi Vote Vipo Takribani Wilaya Ya Tunduru Na Pand3 Za Songeha Kwa Sana Tu. Kwetu Kule Tunamix Na Majani Ya Magimbi,majani Ya Bamia, Nyanya, Chumvi, Magadi, Du! Tamuje! Narudi Kwetu Kimbiji. Chezea Tanganyika Wewe!
 
tamuje umitisha a useful uzi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…