Kaunga
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 12,529
- 13,494
ahahahhahah sijui ilinipitaje hiii!
pitiku bana haina makuu!
ni majani ya maboga
chumvi
maji
na kapilipili
unakata majani ya maboga vidogo dogo,unaweka maji,na pilipili unabadnika jikoni!
maji yakichemka unaweka mboga
inaiva kama dk 8-10 hiv
halafu weka chumvi!
ehehehheheheh Kaunga come zis way!
Mentor hebu do ze nidful kwa huyo kamwali af unoe mambo!
A LOT IN STORE FOR YU!
lol!
Sisi tuna kitu ya msapagulo
Msusa mchanga (majani ya maboga) ukishauchambua na kuuosha (kama una mchanga, ila kuuosha unaufanya uwe mgumu), unakata mapande makubwa makubwa preferably na mikono sio kisu.
Unabandika maji kiasi jikoni, yakichemka unaweka chumvi na magadi kidogo (au baking powder) ili msusa usiwe mgumu; baadaye waweka msusa wako unafunika kidogo, ukigeuza katia nyanya moja tu, na pilipili (kwa ladha) funika kidogo then weka kinyori cha karanga (karanga iliyosagwa) kidogo sana sana, epua baada ya muda mchache hakikisha rangi ya kijani haipotei.
Waweza usiweke karanga, na bado ikawa nzuri, au ukaweka tone chache za mafuta; ila pilipili ni nzuri kwa walaji na inapendeza ikiliwa ikiwa ingali ya moto.