Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Mapishi ya supu ya matango ya baharini na pilipili manga
[TABLE="width: 90%, align: center"]
[TR]
[TD="class: FontStyle5"]
Mahitaji
Matango gramu 750, pilipili manga gramu 3, vipande vya vitunguu maji gramu 25, mvinyo wa kupikia gramu 15, chumvi gramu 4, chembechembe za kukoleza ladha gramu 5, tangawizi gramu 10, kiasi kidogo cha giligilani, mafuta ya ufuta na mchuzi wa sosi.
Njia
1. osha matango , halafu uyakate yawe vipande vipande. Chemsha maji, halafu weka vipande vya matango kwenye maji ya moto.
2. washa moto mimina mafuta kwenye sufuria halafu tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi korogakoroga, mimina maji, mvinyo wa kupikia, chembechembe cha kukoleza ladha, mchuzi wa sosi, chumvi na pilipili manga, korogakoroga, halafu tia vipande vya matango korogakoroga. Baada ya kuchemka ipakue kwenye bakuli. Mimina mafuta ya ufuta, weka vipande vya vitunguu maji na giligilani. Mpaka hapo supu hiyo iko tayari.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Mapishi ya ngisi na kuku
[TABLE="width: 90%, align: center"]
[TR]
[TD="class: FontStyle5"]Mahitaji
Ngisi gramu 50, kuku mmoja, pilipili hoho gramu 10, pilipili mboga gramu 10, mchuzi wa sosi vijiko viwili, sukari kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, pilipili manga kijiko kimoja, wanga vijiko viwili, kiasi kidogo cha vitunguu maji, tangawizi, na giligilani.
Njia
1. kata kuku awe vipande vipande, koroga pamoja na mchuzi wa sosi, sukari, chumvi na wanga.
2. osha ngisi halafu umkate awe vipande. Kata pilipili hoho, pilipili mboga, vitunguu maji na tangawizi ziwe vipande.
3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia vipande vya pilipili hoho, vitunguu maji na tangawizi, korogakoroga tia vipande vya kuku korogakoroga, halafu mimina maji, baada ya kuchemka punguza moto, baada ya dakika 15, tia vipande vya mboga na ngisi korogakoroga, mimina mchuzi wa sosi, tia chumvi, pilipili manga, korogakoroga halafu tia giligilani, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
Mapishi ya mchele unaonata na nyama ya kuku kwenye majani ya yungiyungi
[TABLE="width: 90%, align: center"]
[TR]
[TD="class: FontStyle5"]
Majani sita ya yungiyungi, mchele unaonata gramu 500, kamba mwakaje gramu 100, nyama ya kuku gramu 50, uyoga gramu50, chumvi kijiko kimoja, sukari vijiko viwili, pilipili manga vijiko viwili, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, wanga vijiko viwili
Njia:
1.osha majani ya yungiyungi, weka mchele unaonata kwenye maji kwa saa moja, halafu upakue. Washa moto, mimina maji kwenye sufuria, weka kamba-mwakaje kwenye maji korogakoroga, wapakue. Pia weka vipande vya nyama ya kuku na uyoga kwenye maji joto, korogakoroga, vipakue.
2 washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia kamba-mwakaje, vipande vya nyama ya kuku, uyoga, korogakoroga, tia chumvi, sukari, pilipili manga na mafuta ya ufuta, korogakoroga, tia maji ya wanga, korogakoroga, Vipakue. Chemsha mchele unaonata kwa mvuke kwa saa moja, halafu koroga pamoja na chumvi, sukari, mafuta ya ufuta, maji na mafuta, korogakoroga.
3 weka mchele unaonata kwenye jani la yungiyungi, halafu weka vitu vilivyokorogwa kwenye hatua ya tatu, halafu weka mchele unaOnata tena, funga jani hilo kuwa mraba, endelea kufanya hivyo, mwisho weka kwenye sufuria chemsha kwa mvuke kwa dakika 10. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]