Mapishi ya ugali unakuwaga kama ugomvi.

Mapishi ya ugali unakuwaga kama ugomvi.

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Nimewaza hapa naona upishi wa ugali huwa unatumia nguvu nyingi sana na kuna kuwa na vurugu sana. Hamna chakula kinapikwa kwa nguvu kama Ugali.
Kwanza unakuta sufuria inabanwa kisawasawa na boi. Halafu mwiko unaanza kuzungushwa na kubondwa kwa chini, ndiyo maana sufuria nyingi za kupikia ugali utakuta zimebondeka katikati, zinakuwa zimedumbukia chini. Pia sufuria yoyote ya ugali lazima utakuta imepindapinda.
Ikitokea moto mkali sana utakuta sufuria inaipuliwa huku bado imebananishwa na boi na ugali unaendelea kusongewa chini. Sometimes na miguu huusika kuibana. Kwakweli huwezi pika ugali ulioiva bila kutoka jasho.

Baada ya kuiva sehemu iliyopikiwa huwa kama uwanja wa vita. Unga na mabonge ya uji kila sehemu.
kazi kubwa ipo kwenye upishi wa ugali shule za bweni. Kwanza kunakuwa na wapishi wawili wenye nguvu. Na jikoni jinsi moto unavyowaka kunakuwa kama kiwandani hivi.

Hivi wakuu hatuwezi buni Ugali cooker kama ilivyo rice cooker. we unaweka tu kipimo cha maji na Unga na kusubiria msosi, haiwezekani?
 
Back
Top Bottom