Mapokezi ya Rais Samia: Kwanini watendaji hawajaweka zulia jekundu, kiprotokali hili limekaaje?

Tumezoea kuona viongozi wakubwa wakipokelewa kwa mazulia mekundu, kwanini kwa mama yetu haikuwa hivyo? Kiprotokali limekaaje hili wanabodi?View attachment 1742740
Naona ni kama vile bado kuna ambao hawaja kubali kwamba huyu mama ndio rais wa JMT, maana hata hii picha yenyewe huwezi amini kwamba ni ya ikulu.
 
Nimegundua leo kuwa kumbe Protocol ni tasnia nzito inayojitegemea kabisa.
Jibu la hii hoja ya mleta mada ni ni rahisi.
Rais, atawekewa Zulia Jekundu pale tu atakapokuwa anawasili nchini kutokea nchi nyingine ya jirani au ya ng'ambo, na pale anaposafiri kuelekea nje ya nchi yake.

Zulia jekundu haliwekwi kwa Ziara za ndani. Rais anapotoka Dodoma kwenda Dar hawekewi zulia, lakini atakapotokea au kuelekea Kenya au Rwanda lazima awekewe zulia jekundu, na Uongozi wote wa Mkoa husika utakuwepo kwenye mapokezi au kumuaga.
Chunguzeni hili.

Naona watu wameshaingiza masuala ya dini kuwa kwavile ni muislamu hataki complication, sio kweli.

Protokali ni Elimu, haiongozwi na dini, hisia au matakwa binafsi ya mtu. Hata asingetaka YEYE binafsi kuwekewa zulia, angelazimishwa na protokali maana wapo watu kwenye payroll walioajiriwa kwa kazi hizo na hawakosei kila Mkuu huyo anapowasili kutoka nje ya nchi.

Hivo wapendwa hiyo ndiyo sababu ya kitaalamu na tujaribu kufanya uchunguzi na kutofautisha aina ya safari.
 
Zulia hutandikwa kulingana na aina ya safari; STATE VISIT, OFFICIAL VISIT NA WORKING VISIT zinahitaji Red Carpet! Lakini kwa Private trip hakuna zulia
 
Yaani kina watu hawana kazi bali kuleta majungu kila kukicha kwa kufuatilia umbea wa vitu visivyo wahusu

Haya hawajaweka zuria amekufa au kadhurika?

Hawa ndiyo wanaosababisha bundle zipande matako yenu
Acha povu, heshima ya rais Ni heshima ya Taifa, ndiyo heshima yetu wote! Lazima tuidai heshima hiyo!.
 
Haongozi kidini, anaongoza kikatiba. Kuna viashiria vya kumkosea adabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…