Maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa yafunika/yasomba Watu na nyumba Moshi

Maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa yafunika/yasomba Watu na nyumba Moshi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Watu watatu katika kijiji cha Mbokomu, wilayani Moshi wamefariki dunia kwa kufunikwa na kifusi baada ya maporomoko ya udongo yaliyotokea usiku wa kuamkia leo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Mbunge wa Moshi vijijini Profesa Patrick Ndakidemi amesema mbali na vifo hivyo mamia ya watu wamepoteza makazi na makumi kujeruhiwa. Mafuriko hayo yameathiri zaidi maeneo ya Mbokomu, Kiboriloni na Old Moshi. Tuwakumbuke watu wa Moshi katika maombi. Swipe LEFT kuona athari zaidi za mafuriko hayo







MKUU WA MKOA AELEZA WATU WATATU KUFARIKI
Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro watu watatu wamefariki dunia wakiwamo wawili wa familia moja katika kata ya Mbokomu baada ya kuangukiwa na nyumba yao.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Mei 6, 2025, ambapo watu hao walikuwa wamelala ndani ya nyumba hiyo wakati janga hilo lilipotokea.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kuwa athari hiyo ni kutokana na mvua kunyesha ukanda wa mlimani na kushusha magogo makubwa yaliyofunga madaraja na barabara.

 
Bado tupo na game ya inter 😉😉😉

Inter 2 -Barce 0
Tucheke siye mashabiki WA Arsenal.

Ufaransa ndio kwetu .
 
Back
Top Bottom