kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Jamii inawaheshimu sana wasomi hasa maprofesa, jamii inadhani kuwa professor sio mtu wa mchezomchezo, anafahamu na kujua na kuweza kila kitu na kila jambo. Inapotokea tukio la professor kubezwa, kuzomewa na kutukanwa au kushindwa kufanikisha jambo inawashangaza sana.
Sio jambo la nadra jamii kusikia wizara inayoongozwa na prof fulani imeshindwa kutatua kero za wananchi na wizara ambayo inaongozwa na asiyekuwa prof inaupiga mwingi katika kutatua kero za watanzania. Lakini pia sio jambo la nadra kuona prof anadhalilishwa na ngazi ya uteuzi kama mtu mwingine tu.
Swali kwenu ni kunatokea nini kuyakimbia madarasa yenu mliyoyazoea na kuyamudu na kukimbilia siasa msizo na ujuzi nazo?
Rudini bhana, tulijenge taifa