Maprofesa kutaka kuongezewa muda wa Kustaafu ni ubinafsi wa hali ya juu

Maprofesa kutaka kuongezewa muda wa Kustaafu ni ubinafsi wa hali ya juu

Cvez

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
4,405
Reaction score
13,411
Screenshot_20211107_172540.jpg

Ni kweli tuna unapungufu wa wanataaluma katika vyuo vyetu ila haijatokea kwa bahati mbaya. Katika vyuo vyetu hivi kama huna Surname inayofanania ni na Profesa fulani kupata nafasi ya ukufunzi hiyo ni ndoto. Katika sehemu ambazo kwa kiasi kikubwa zimejaa undugu na kujuana kwa kiasi kikubwa ni hizi taasisi za elimu ya juu. Hata kama kuna upungufu wa wataalam ila kama wale wakuu wa idara hawana ndugu au rafiki wanaomjua wapo radhi wasitangaze hiyo nafasi na kukomaa wenyewe hivyohivyo. Ni endapo tu pale wataona washapata mtu wao ndio itatangazwa hiyo nafasi au hata kama hamna wataitengeneza.

Jambo lingine katika hizi taasisi za elimu wajitahidi katika kuajiri kutafuta watu wenye uwezo wa kufundisha na uzoefu wa kazi angalau miaka mitatu katika course husika. Mfano let's say ni course ya IT or Marketing chukueni mtu alietoka field, mitaala yetu ipo outdated ila kazini watu wanaenda na mabadiliko ndio maana graduates wengi wakifika kazini hufundishwa kila kitu upya.

Nishakutana na hawa wakufunzi ambao katoka chuo tu kabakishwa chuoni yaani akitoa mfano ni ule ambao upo kwenye kitabu na sio real life experience. Unakuta batches kama tatu zinafundishwa na mwalimu wa aina hii yet utegemee wataalam wa kuleta mabadiliko. Faida ya kupata mkufunzi mwenye uzoefu wa kazi hata kama atatumia mtaala huo huo wa zamani ila anajua ni kipi cha kutilia mkazo na kipi kupotezea plus hata mijadala ni yake darasani ni ya real life experience na sio mifano ya kwenye vitabu au dhahania tu.​
 
Back
Top Bottom