Mzanzibari Huru
JF-Expert Member
- Apr 17, 2014
- 393
- 234
Ndugu Wana Jamii,
Tumeanza kusoma hisia tofauti, za watu tunaoweza kuwahisi ni wapinga maendeleo au wanaotaka kujaza matumbo yao binafsi kwa kutumia madaraka walioaminiwa na jamii, juu ya kauli adhimu ya Mama Raisi wetu kuhusiana na muelekeo wa maendeleo ya Tz na maendeleo binafsi ya raia.
Mama amesema Tz haina Skilled Labours ingawaje wanaobeba shahada za degree, masters na Phd ni wengi lakini waliosoma kweli na kuweza kuthibitisha usomi wao kwa vitendo ni wachache sana. Hili naomba mtu yoyote ajitokeze alipinge, nadhani tutakubaliana hapa kwamba tunaweza kuujua mti mzuri kwa matunda yake. Wanaotambulikana kama wasomi ni wengi lakini wanachokifanya hakitambulikani. Sisemi kama dalili hizi pungufu ziko kwa wote, la hasha!, lakini watizameni wasomi wa mashahada waliokadhiwa madaraka wanaifanyia nini jamii ya waTz. Sasa badala yake hawa wanataka kusisitiza kwamba muekezani akija Tz kuwekeza ni lazima aajiri Watz hata katika vitengo ambavyo hawawezi kuvihimili. Hilo ni sawa na kumtaka yule alokuwa obese kupanda mlima kilimanjaro kwa miguu.
Ni hikma nadhani kujuwa kwamba muekezaji anataka profit. It does not make any bsuiness sense, kumlazimishwa muekezaji kumuajiri Mtz mvivu na mzembe alobeba shahada tupu ijapokuwa hana taaluma juu ya kazi hiyo. hiyo si busara na italeta taabu katika mradi huo.
Wale wanaodai kwamba Mama Raisi amesema kwamba wawekezaji wanaruhusiwa kuajiri kutoka nje hadi walinzi na wafagiaji ni waficha ukweli na ukitizama kiju juu utawaona ni wapinga uwejezaji. Mama Raisi kasema ikiwa muekezaji anataka kuweka mtendaji imara katika kitengo fulani na ikiwa hakuna Mtz, kwanini asiruhusiwe kuleta anaweza kuifaya kazi hiyo kwa ufanisi zaidi.
Tuwacheni kulalamika wakati vyuoni wanafunzi wanapata grade zao kwa rushwa tu hata ikiwemo ya ng'ono. Sasa unatarajia nini? Ukitaka kuibomowa nchi huna haja ya kurusha nuclear bombs kwasababu walishajaribu hilo kwa japan na haikusaidia sana, leo Japan imepanda juu zaidi. Pia haina haja ya kurusha makombora kwasababau walishajaribu huko Ujerumani, lakini haikusaidia sana leo hii Ujerumani imepanda juu zaidi na zaidi. Ukitaka kuibomowa nchi ni kuruhusu rushwa katika vyuo vikuu, hapo utapata madokta fake, wahandisi feki, mahasibu feki, wanasheria feki na wakuu feki katika kila kitengo. Na ukitaka kujuwa ubora au uozo wa wasomi angalia matunda yao katika jamii.
Mama Raisi fanya kazi, safisha njia, boresha elimu zaidi na zaidi na zaidi ili Watz wajao wawe productive katika jamii. Ikiwa muekezaji hapati Mtz anayeweza kuifanya kazi fulani kwa usanifu basi mwache alete mgeni, tutasoma kwao.
Ahsanteni