Maprofesa wa vyuo vikuu TZ hutumia kiswahili kufundishia badala ya Kiingereza

educator2025

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Posts
395
Reaction score
455
Imekuwa kasumba na utamaduni unaozidi kuchipuka sasa kukuta maprofesa/walimu wa vyuo vikuu vingi hapa TZ (UDSM, SUA, SAUT, Makumira,TEKU, Muhimbili, ARU etc.) kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia badala ya lugha ya kiingereza kama inavyopaswa na sera ya Elimu ya Taifa (Tanzania Education and Training Policy, TETPO ya mwaka 1995) swali la kujiuliza hiv ni wapi Maprofesa/walimu hawa wanatupeleka? wasomi wetu wataweza kuimudu lugha hii ya kiingereza kweli kama maprofesa tu wanafundishia Kiswahili?TUJADILI
 
Chuoni si pahala pa kujifunzia lugha my dear. Hiyo ni kazi ya walimu wa msingi na sekondari. Kama hukujua kiingereza ktk levo hiyo usitegemee chuoni kwani pale ni pahali pa know how and why!!! Hivyo wapo sawa kabisa maprof wetu.
 
mmh so unawa support maprof kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundisha/kujifunzia?
 
mmh so unawa support maprof kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundisha/kujifunzia?

Unavyosema maprofesa una-generalize sana, ingekua busara zaidi endapo ungesema baadhi ya maprofesa. Hata hivyo, sikubaliani na wewe kwamba kitu kama hicho kinafanyika kwenye vyuo vyote ulivyovitaja
 

Usipende ku generalize mambo,
be specific kwa kusema maprofesa wa chuo unachosoma/ulichosoma wanatumia kiswahili kufundisha....

Wengine mpk tunamaliza chuo hatukuwahi kusikia kisw Ebo!
 
Kuna vyuo umevitaja sijui kama kweli maprofesa wanaonekana huko zaidi ya majina yao kwenye makabrasha.
 

ningekuona wa maana sana kama na wewe ungetoa "thread" /uzi huu kwa umombo /kiingereza tena kilichokwenda shule ili uwe mfano ulio hai juu ya ukisemacho, kumbuka wengine hapa ni "prescriptivist" ...kuliko kubwabwaja bwabwaja kwa kiswahili tena hapo hapo unakiponda, ishi katika uhalisia wako.
 
Ivi lengo nikujua english au kuelewa kinachofundishwa.eng ni luga km kisw embu tujitambue km wachina tujivunie luga yet
 
Minaona wapo sahihi kabisa, inasaidia kuongeza uelewa, nenda Japan, China na German uone kama wanatumia icho kiingereza unachokitukuza, izi nchi zinafanya makubwa katika technology, aya wewe uliefundishwa kwa kiingereza umefanya kipi cha maana mpaka sasa?
 
mmh so unawa support maprof kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundisha/kujifunzia?
Tena hata secondary kuna mahali ni LAZMA kufundisha kwa kiswahili
kuna shule zipo vi jijini watoto Kiswahili tu hawajui wanaongea lugha zao hadi darasani
hicho kiingereza si nitakuwa najifundisha mwenyewe?
 
Sio mbaya wakitumia lugha ya taifa kuwapa ufahamu wanafunzi wao, chuo ni mahala pa kuelewa na kutenda na wala sio pa kukariri kama shule za sekondari. Then next time fanya utafiti vizuri usipende ku generalize sana..

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

Uongooooo! Mbona SUA majamaa yanakandamiza tangu mwanzo mpaka mwisho kiingereza tu! Labda utueleze uko chuo gani wewe?
 
Tungeendelea kutawaliwa na Ujerumani pengine Tatizo na mjadala kama huu usingekuwepo. Mjerumani alijikita sana katika kukiendeleza Kiswahili. Huenda mambo yote sasa hivi yangekuwa katika Kiswahili. Tatizo, Bahati mbaya kwetu ni pale Uingereza ilipoingia. Ninailaani siku ambayo Uingereza iliingia kuitawala Tanganyika! Walitujengea hulka ya kutojiamini, wakaua Kiswahili na mambo kibao! Ingewezekana kufuta (delete) Historia ningependekeza tufute kuanzia siku Uingereza ilipoanza kuitawala Tanganyika!
 
Mwenye akili ya kuelewa ataelewa unachokimaanisha
 
Nimesoma Udsm kampasi ya Mlimani sijawahi muona Mhadhiri anatumia kiswahili kufundishia.....nimefundishwa na Wahadhiri kama Prof. Baregu, Prof. Chaliga, Prof. Max muya, Prof. Benedeta Killian, Bashiru Ally, Dr. Rwaitama, Dr. Bruce, Dr. Kitila Mkumbo nk kuwa specific ni Maprofessa gani kwa majina maana binafsi nawajua baadhi ya wahadhiri hata kiswahili hawakijui
 

Kumbe wanaojitambua wako wengi. Hongera mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…