Mapumziko garden

Mapumziko garden

Ila kwa wale tutakaokuwa tuna date wanawake tunaruhusiwa???

Unisamehe bure, tendo la ndoa kinyume cha sheria si vizuri kulifanyia sehemu ya mapumziko ya public. kwa sababu wanakimbia kumbi za mjini kwa sababu ya vituko wanavyoviona sehemu hizo.
 
mkuu Malila,
fikiria jinsi ya kuweka wanyama wadogo wadogo,kama simbilisi,jamii ya swala,panya buku ,sungura etc,si unajua kwa wale wenye watoto wa primary unaweza kukuta mtoto anajua wanyama ktk video tu,hajawahi hata kumuona ostrich ,
hivi kufuga Tausi unahitaji kibali? ingependeza pia ukaweka tausi ,siku hizi hawapo tena.

Nitajitahidi kuweka vitu adimu, lakini haitakuwa zoo,mbuzi wa kukamua maziwa tayari. Mutensa alilemaa mimi nimewasomba wote.Simbilisi na pimbi nitawaweka kidogo, unajua mbolea ya simbilisi ina nguvu sana bro !!!!!. Kituo cha daladala tayari kinajulikana.
 
Malila mapumziko garden vipi ishakamilika?
 
Last edited by a moderator:
Hi
Jijini Dsm kuna upungufu mkubwa wa sehemu nzuri za kupumzikia familia ( yaani mahali ambapo wewe na familia yako unaweza kwenda bila kigugumizi),mahali ambapo unaweza kuyaona mazingira yenye heshima ya Kiafrika. Naamini familia nyingi zingependa kwenda mahali ambapo ni free fro alcohol, free from uzinzi,free from kiti moto, bali kuna juice ya matunda,ugali wa dona,kuku wa kienyeji,maziwa ya mbuzi,muziki laini kwa sauti ya chini kabisa.

Bustani itakuwa na vyumba vizuri kwa bei nzuri ambayo MKESHA HOI/LAT/KAKA KIIZA wa JF anaweza kumudu bila maumivu na akatamani kurudi tena.Bustani itakuwa na mboga za majani kama mnafu na nyinginezo. Michezo ya watoto wetu itawekwa.

Nahitaji michango ya huduma gani zaidi ziwepo ili kupafanya pawe bora zaidi. Eneo lipo,linafikika kwa daladala,lina maji na ni kubwa kama eka kumi. Hili eneo sitaki kuliharibu, nataka libaki na uasili wake kwa kuitunza miti niliyo ikuta pamoja na nyasi zake. Nitaongeza miti ya matunda tu.

mkuu Malila, hata neno 'garden' pia futa delete kabisa...tumechoshwa na huu uzungu uzungu....kazini corporate, starehe corporate...kiasili zaidi
 
mkuu malila hili wazo liko juu sana. kuna mtu amefanya kila kama hiki kule Arusha maeneo ya njilo ( hajaweka wanyama) anakula pesa sana. Wazo la kwako litakuwa bomba zaidi kwani unataka kuweka vitu vingi. usisahau bembea ya watoto. Nyimbo za kuabudu kwa mbali kwa ajili ya kumsifu Bwana na ili wote watakaofika hapo wajue kuwa wamefika mahali patulivu na panapohitaji utulivu wa hali ya juu.

Bila shaka mimi nimeipenda sana hii. Nitaiga mfano wako uko mbeleni. Ngoja nipambane kwanza na Nguruwe wangu kwani nimepata taarifa kuwa mmoja anaumwa huku nikachanganyikiwa.
 
Malila mapumziko garden vipi ishakamilika?
Tayari hatua za awal. Mbuzi wa nyama na kuku aw kienyeji, na Samaki nimewapeleka kwa majaribio. Master plan imekamilika tayari. Swimming pool ya bata tayari. Njoo unitembelee.
 
Tayari hatua za awal. Mbuzi wa nyama na kuku aw kienyeji, na Samaki nimewapeleka kwa majaribio. Master plan imekamilika tayari. Swimming pool ya bata tayari. Njoo unitembelee.

kweli mkuu? nitakuja aisee.
 
mkuu malila nakukubali kwa michango yako, hasa sie wageni tumevutiwa kujiunga. Galawani ndio wapi huko? Tuje kukutembelea?
 
mkuu malila nakukubali kwa michango yako, hasa sie wageni tumevutiwa kujiunga. Galawani ndio wapi huko? Tuje kukutembelea?

Galawani iko kijiji cha Msorwa wilayani Mkuranga. Ukitoka pale Mkuranga wilayani fuata njia ya Kisiju mpaka ufike Mbezi, kisha pale Mbezi ingia kushoto, fuata barabara mpaka Msorwa, utavuka daraja la kwanza, la pili ndio Galawani, la Tatu ni Mduzi. Ukienda mbele zaidi utafika Shungubweni mpaka beach safi ya Boza na kisiwa cha Kruti.

Mduzi na Galawani ni mito ya kudumu, karibu tulime na kufuga mkuu. Ila mafisadi wanamaliza ardhi yote.
 
Ni idea nzuri sana na hasa nilipotaka kuongezea tayari umeweka SAMAKI ukiwa na bwawa basi mtu anavuliwa na anachagua atengenezeweje choma, chemsha au kaanga!
 
nahisi sahv pamechangamka sana.

Tayari pana jina la kituo cha daladala kabisa, wewe ukikwea daladala Mbagala ukaomba ushushwe pale, bus umeshafika. Tuna kimbizana na Mamba, kila siku anatembelea dimbwi letu. Karibu sana.

Jamaa wameshauri, huyu Mamba awe sehemu ya bustani.
 
Mkuu Malila, hayo maeneo bado yananunulika kwa kilimo? na bei zipoje mkuu?
 
Mkuu Malila, hayo maeneo bado yananunulika kwa kilimo? na bei zipoje mkuu?

Bado yananunulika, bei zinacheza kt ya laki tano mpaka laki nane kando ya mito, lakini unaweza kupata mpaka laki nne kama shamba liko nje ya mto. Zipo eka 18 pembeni ya shamba langu zafaa kwa kilimo na ufugaji, bei ni laki sita bila chenga.
 
Galawani iko kijiji cha Msorwa wilayani Mkuranga. Ukitoka pale Mkuranga wilayani fuata njia ya Kisiju mpaka ufike Mbezi, kisha pale Mbezi ingia kushoto, fuata barabara mpaka Msorwa, utavuka daraja la kwanza, la pili ndio Galawani, la Tatu ni Mduzi. Ukienda mbele zaidi utafika Shungubweni mpaka beach safi ya Boza na kisiwa cha Kruti.

Mduzi na Galawani ni mito ya kudumu, karibu tulime na kufuga mkuu. Ila mafisadi wanamaliza ardhi yote.

Nashukuru kwa maelekezo yako mkuu Malila, nimekulewa vizuri. Nina maswali mawili matatu. Kuna umbali gani toka Mbagala rangi 3 mpaka hapo Galawa kwa gari binafsi? Njia ikoje ni gari ya 4WD tu inapita au gari aina zote? Je shamba lilo jirani na kwako maji yako umbali gani? na mwisho kilimo cha zao gani waweza kulima kwa maoni yako. Usinichoke mkuu kwa usumbufu wangu.
 
Kutoka Tazara pale mataa ni km 60 mpaka Galawani na km 65 mpaka Mduzi, mito yote hiyo ni ya kudumu, barabara ni za kibongo, ukiwa na 4wd ni nzuri zaidi. Shamba lipo jirani na langu, mto upo shambani hapo hapo, ila mamba wapo pia. Mazao jamii ya mboga mboga yanafaa kulimwa sababu soko lake linaanzia Mkuranga kule kule. Karibu sana.
 
Akhsante mkuu tuombe uzima in shaa Allah.
 
Back
Top Bottom