Ila kwa wale tutakaokuwa tuna date wanawake tunaruhusiwa???
mkuu Malila,
fikiria jinsi ya kuweka wanyama wadogo wadogo,kama simbilisi,jamii ya swala,panya buku ,sungura etc,si unajua kwa wale wenye watoto wa primary unaweza kukuta mtoto anajua wanyama ktk video tu,hajawahi hata kumuona ostrich ,
hivi kufuga Tausi unahitaji kibali? ingependeza pia ukaweka tausi ,siku hizi hawapo tena.
Hi
Jijini Dsm kuna upungufu mkubwa wa sehemu nzuri za kupumzikia familia ( yaani mahali ambapo wewe na familia yako unaweza kwenda bila kigugumizi),mahali ambapo unaweza kuyaona mazingira yenye heshima ya Kiafrika. Naamini familia nyingi zingependa kwenda mahali ambapo ni free fro alcohol, free from uzinzi,free from kiti moto, bali kuna juice ya matunda,ugali wa dona,kuku wa kienyeji,maziwa ya mbuzi,muziki laini kwa sauti ya chini kabisa.
Bustani itakuwa na vyumba vizuri kwa bei nzuri ambayo MKESHA HOI/LAT/KAKA KIIZA wa JF anaweza kumudu bila maumivu na akatamani kurudi tena.Bustani itakuwa na mboga za majani kama mnafu na nyinginezo. Michezo ya watoto wetu itawekwa.
Nahitaji michango ya huduma gani zaidi ziwepo ili kupafanya pawe bora zaidi. Eneo lipo,linafikika kwa daladala,lina maji na ni kubwa kama eka kumi. Hili eneo sitaki kuliharibu, nataka libaki na uasili wake kwa kuitunza miti niliyo ikuta pamoja na nyasi zake. Nitaongeza miti ya matunda tu.
Tayari hatua za awal. Mbuzi wa nyama na kuku aw kienyeji, na Samaki nimewapeleka kwa majaribio. Master plan imekamilika tayari. Swimming pool ya bata tayari. Njoo unitembelee.
Njoo ujionee mwkweli mkuu? nitakuja aisee.
mkuu malila nakukubali kwa michango yako, hasa sie wageni tumevutiwa kujiunga. Galawani ndio wapi huko? Tuje kukutembelea?
Njoo ujionee mw
nahisi sahv pamechangamka sana.
Mkuu Malila, hayo maeneo bado yananunulika kwa kilimo? na bei zipoje mkuu?
Galawani iko kijiji cha Msorwa wilayani Mkuranga. Ukitoka pale Mkuranga wilayani fuata njia ya Kisiju mpaka ufike Mbezi, kisha pale Mbezi ingia kushoto, fuata barabara mpaka Msorwa, utavuka daraja la kwanza, la pili ndio Galawani, la Tatu ni Mduzi. Ukienda mbele zaidi utafika Shungubweni mpaka beach safi ya Boza na kisiwa cha Kruti.
Mduzi na Galawani ni mito ya kudumu, karibu tulime na kufuga mkuu. Ila mafisadi wanamaliza ardhi yote.
Nashukuru kwa maelekezo yako mkuu Malila, nimekulewa vizuri. Nina maswali mawili matatu. Kuna umbali gani toka Mbagala rangi 3 mpaka hapo Galawa kwa gari binafsi? Njia ikoje ni gari ya 4WD tu inapita au gari aina zote? Je shamba lilo jirani na kwako maji yako umbali gani? na mwisho kilimo cha zao gani waweza kulima kwa maoni yako. Usinichoke mkuu kwa usumbufu wangu.
Kutoka Tazara pale mataa ni km 60 mpaka Galawani na km 65 mpaka Mduzi, mito yote hiyo ni ya kudumu, barabara ni za kibongo, ukiwa na 4wd ni nzuri zaidi. Shamba lipo jirani na langu, mto upo shambani hapo hapo, ila mamba wapo pia. Mazao jamii ya mboga mboga yanafaa kulimwa sababu soko lake linaanzia Mkuranga kule kule. Karibu sana.