Mapungufu ya klabu yangu ya Yanga

unajifariji tu ila kagoli kamoja kanauma mno!

Huu ni mwaka wetu wananchi mikia kubalini tu tumewazidi uwezo! hata wangecheza wote wenye majerubi bado tungewapasua tu , ili Simba iifunge Yanga lazima Yanga wacheze pungufu! Hakuna namna mtapigwa tu!
Iwe pungufu ama kuwepo na mgogoro na baadhi ya wachezaji na kuchukua mlungura vinginevyo Simba kumfunga Yanga ni kazi mno Kama alivyotabiri kaduguda
 
Msimu huu ktk mechi 4 walizokutana
YANGA kashinda 2
Simba hajafunga hata goli la offside
Mafanikio pekee kwa simba ni kumzuia Mayele asiteteme ×3 ktk derby
Makambo ktk mechi 2 za mwisho na ya leo kaonyesha ana vitu vya kutupa kama tukimpa muda wa dk zisizopungua 45
Diarra heshima anayoipa Yanga ni kubwa
Beki za Yanga zimetulia sana hakuna mashaka...

Ukiniuliza kuhusu Simba,jibu langu ni fupi tu "simba ilifika ktk kilele cha ubora, sasa kikos nimechoka kimeisha makali, kinatakiwa transformation kubwa kuanzia mabeki, viungo na washambuliaji" lazima wakubali kupoteza msimu mmoja zaid kama Yanga ili waweze kusuka kikosi...
 
Manula naye huwa anatunguliwa za mbali, Bocco kwisha habari yake, Chama pumzi huwa inamwishia mapema kwenye deby.

Morrison kasaini Yanga.
Mkude na kapombe angalau hao sawa na Yanga kumkosa Saidoo na Yacouba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…