Mapungufu ya Lady Jaydee na kosa la kumwita Mwana FA kuwa MwanaFatuma

Mapungufu ya Lady Jaydee na kosa la kumwita Mwana FA kuwa MwanaFatuma

Mkuu, umeonesha udhaifu mkubwa katika uandishi wako!

Na hii inaonesha umejisajili Jana tarehe 12/06 kwa sababu yakuja kuonesha/kutoa hisia zako kwa Judith Wambura!

Ungeandika na ya upande wa pili wa "Hamis Mwinjuma" ili nasi tuyajue kuona jamaa ni msafi kiasi gani hata ukatokwa na povu namna hiyo!

Mwisho naomba lete na ya upande wa pili wa "Swahiba" yako ili tuendelee kuchangia.

Usijali,ukitaka ya Mwana Fa pia nitaweka hapa,nimeweka ya jaydee kwa kuwa ndo kaanza,na Mwana Fa katulia mpaka saiv,hii ni dalili ya kuwa kamdharau jaydee kwa Kumuita MwanaFatuma.Sina chuki na jadee maana hata kwao musoma nilishafika kipindi cha nyuma.hii ilitokana na mm kuwa mpenzi wam uziki wake.Lakini katika hili sijafurahi kabisa,angejickiaje angeitwa Jike-dume??,ama kijeba,ama jina lolote ambalo ni chafu kama kumwita mwaume MwanaFatuma ama Mwanahamis??
Tusione aibu kumwambia mtu ukweli anapokosea!!,sifa za kijinga huwa sio nzuri kabisa.maana hata waliomsifia Dudubaya akati anampiga mr nice leo wanaandika humu kuwa anauz amkaa magu.
 
cha muhimu wewe kaa pembeni usikilizie tu maana mwisho wa siku wote wanapiga hela..

Na hicho mimi ndio nakiamini, hawa watu wameamua kuwatumia washabiki bila wao kujua ili watengeneze pesa. Subiri hizi show zao ziishe kama utawasikia tena.
Kama Harakati ni zile alizofanya Sugu kapiga potepote kuanzia kwenye media, majukwaani, nyimbo na mitandao ya kijamii na sapoti kubwa kutoka kwa wasanii wenzake bado hakufanikiwa kiivyo ije iwe hii ya Jd ambayo anaifanya kwenye blogs? watu ambao wapo nje na mitandao hawajui chochote kinachoendelea kuhusu yeye na Clouds.
Tukubali tukatae issue ya Jd na Clouds ni matatizo yao binafsi, ila kaamua kaamua kuyazungumzia matatizo yao kupitia njia nyingine ili apate sapoti.
 
itakuwa mkuu unawakubali wote mwanafatuma na joka anaconda ndio tabu yako cha muhimu wewe kaa pembeni usikilizie tu maana mwisho wa siku wote wanapiga hela..

Uko sahihi kabisa mkuu
 
Mkuu muwe mnafanya research kabla hamjaandika humu.
Uyo mwanaFA unayemtetea anatumiwa na clouds kushiriki kunyonya kazi za wasanii wa tanzania kwa kuzuga kama yeye ndo muwakilishi wa wasanii kumbe nia yake ni kufyonza kile kinachofyonzwa na clouds kutoka kwa wasanii wengine.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wanajamii mnaruhusiwa kuchangia lolote katika hili....
 
She has an arrogant and false sense of entitlement. Even worse, she thinks she is the shit when she ain't.

Her music is shitty and her attitude is woeful. She needs an attitude adjustment.

Uko sahihi
 
Mwanaume unapogombana na mwanamke lazima mwanaume aonekane ndiye mwenye makosa! FA kubali yaishe na ukae kimya usigombane na wanawake! mbona best yako wa damu AY ametulia na hana kashfa yoyote?
 
Usijali,ukitaka ya Mwana Fa pia nitaweka hapa,nimeweka ya jaydee kwa kuwa ndo kaanza,na Mwana Fa katulia mpaka saiv,hii ni dalili ya kuwa kamdharau jaydee kwa Kumuita MwanaFatuma.Sina chuki na jadee maana hata kwao musoma nilishafika kipindi cha nyuma.hii ilitokana na mm kuwa mpenzi wam uziki wake.Lakini katika hili sijafurahi kabisa,angejickiaje angeitwa Jike-dume??,ama kijeba,ama jina lolote ambalo ni chafu kama kumwita mwaume MwanaFatuma ama Mwanahamis??
Tusione aibu kumwambia mtu ukweli anapokosea!!,sifa za kijinga huwa sio nzuri kabisa.maana hata waliomsifia Dudubaya akati anampiga mr nice leo wanaandika humu kuwa anauz amkaa magu.

Mkuu, Judith kaonesha hisia zake kama vile wewe unavyoonesha kupitia JF.

Kwahivo heshimu hisia zake, nae akija hapa tutamuambia aheshimu hisia zako. CASE CLOSED
 
Mkuu, Judith kaonesha hisia zake kama vile wewe unavyoonesha kupitia JF.

Kwahivo heshimu hisia zake, nae akija hapa tutamuambia aheshimu hisia zako. CASE CLOSED

Inawezkana upo sahihi lakini nnavojua kuonesha hisia kwa kumdhalilisha mwenzako sio sawa.
 
Ooya nyie, hawa watu wanapiga promo tu hakuna cha bifu ya Jide na FA, wala clouds. Issue kama hizi ni maarufu sana kwenye muziki hasa marekani. Humu mnahangaika tu na kuShushiana heshima huku wenzenu wanajua wanachokifanya. Mimi hii kitu hakiniingi akilini kabisa.
 
Tuache kutetea ujinga jaman,sawa jide analalamika anaonewa lakini tatizo lake nae anadharau then hapend kushauriwa
 
Mimi ni mshabiki wa huyu jamaa, lakini nafaham kuwa ana mapungufu kwa kiasi kikubwa sana.
Ntawarudisha nyuma kabisa kipindi wanajitoa ECT, nilimsikia akihojiwa na EA radio
akimponda sana GK na kudai "anamdai laki tisa" wakati kila mtu anajua bila GK hakuna
FA wala AY aliwabeba sana mpaka tulipoanza kuwasikia.Baadye nikaja msikia Radio station
Akikanusha kusema hivyo.

Pili wakati wasanii wamekaa na kuunda TUMA, yeye na Boss wake Ruge wakaja na TFU yeye kama
Mwenyekiti, hili pia lilionesha jinsi jamaa alivyorahisi kurubuniwa, na iliharibu uhusiano
na wasanii wenzake kwa kiasi kikubwa hadi kupelekea kuchanwa na SUGU kwenye Antivirus VOl 2 eti "Ruge anamtumia kama Condom"
Baadaye nikaja msikia kwenye mikasi akijikosha na kuota kuwa ipo siku atasameheana na SUGU.

Sasa ndio hii ishu ya Anaconda, jamaa nadhani anatumika vibaya na mwenyewe analijua hilo, na baadaye atakuja
kutaka kupatanishwa na Jide. Katika hili ishu co kupiga show siku moja, ishu wao kama wasanii wakongwe walitakiwa wawe pamoja
Katika hili. Hata SUGU alishasema kama wenzio/mwenzio anaanzisha harakati kama hutaki kuwa sehem ya hizo harakati ni sawa, lakini
ukionekana unawasaidia wanaopinga hizo harakati basi wewe ni msaliti.

Kwa hizo facts hapo juu its safe to say MwanaFA = MwanaFatuma.

Boondocks.
 
Kwanza nakupongeza sana mdada kwa kufanya bidii katika muziki na kimaendeleo pia.mimi siko Tanzania kwa muda sasa lakini nafuatilia kwa karibu sana kila kinachotokea huko.Majuzi uliposti katika tweeter na kumwita mwana Fa mwanafatuma.Binafsi skufurahi kwa kuwa sioni sababu hasa ya wewe kumwita Mwana Fa mwanafatuma.Sababu hasa inayo sababisha wewe kumwita hivo ni kwamba unahisi kuwa karubuniwa na CLOUDS FM kukuhujumu kwa kuweka shoo yake siku na tarehe ambayo wewe pia ulikuwa na shoo.Lakini umesahau kuwa msanii hupangiwa shoo na promota lakini pia hutegemea ujira wake kutokana na shoo anazofanya.Ingewezekana vipi MWANA FA kukataa kufanya shoo tarehe 31,kisa wewe unafanya shoo???,kwani we ni nani hapa tz ampaka watu waahirishe mambo yao na kuweka atention kwako????.

Umesahau kuwa hata hayo maendeleo ulonayo umetoka huko ambako mwana fa anapigania kutoka ili miaka ijayo hata yeye awe na mgahawa wake kama wewe???,hakuna siku ambayo wewe umefanya shooo huku msanii mwingine nae anafanya sho mahala pengine??? Hata kama Ruge alihusika kupanga jabo hilo, mwana Fa inamhusu nini ugomvi wenu wewe na Ruge?? mpaka aahirishe kufanya shoo.?Kwa nini unalazimisha mawazo yako yafanane na ya watu wote??????,ugomvi wenu na Ruge usababishe kila kitu kismame??,kumbuka wewe sio mtu muhimu sana hapa tanzania japo una heshima kubwa sana katika muziki wetu.

Yafuatayo ni mapungufu yako jaydee.
1.Unadhani kwamba wewe ni mtu muhimu sana hapa tanzania kuliko wasanii wengine
2.Unaponzwa na kujiamini kusiko kuwa na tija na kudhani kuwa uko sahihi kwa kila unalolifanya
3.Umebweteka na sifa unazopewa na mashabiki katika mitandao ya kijamii na pengine
4 huna mahusiano mazuri na wasanii wenzako maana hata misibani umeanza kuonekana majuzi baada ya kushtukiwa kuwa huwa huendi
5.unashindwa kuamini kuwa sasa wakati wako umeisha na inabidi uwaachie akina recho na mwasiti kijiti
6.Umesahau kuwa na wewe pia ulitoka huko huko kwa Ruge na pia kama ni kuamrishwa ulikuwa unaamrishwa kama akina Fa

USHAURI-
1.Acha kujiona upo sahihi kwa kila jambo.
2.Shirikiana na wenzako katika kila hali sio kujitenga na kuwalaumu kuwa wanakusaliti kumbe wewe una umimi mimi tango kitambo.

3.Usilewe sifa za mashabiki ambao watakuponda baada ya muda ukisha poteza mwelekeo.
4.Nakushauri mwombe msamaha Mwana Fa haraka utavoweza.

wanajamii mnaruhusiwa kuchangia lolote katika hili....,
These accusations are so personal, hakuna kipya katika tuhuma hizi, same old beef, Let Jide be who she wanna be, let FA be who he wanna be, lakini linapokuja suala la msanii/mwanamuziki kujua kwamba mtu mwingine ananufaika zaidi na jasho lake na ubunifu wake bila ya kuwepo "terms' zinazoeleweka, It really sucks!
 
kakq umesema kweli ila watu watajifanya kubisha!!! jay dee hataki na wenzake wapate yeye alichopata!! angesema mwanzo ningemwelewa ila kwa leo hii hapana!
yeye anamuita mwenzake mwanafatuma cku na yeye akiitwa mgumba makengeza asinune!!

Ulishavuka mto ama!mpaji MUNGU
 
Tuache kutetea ujinga jaman,sawa jide analalamika anaonewa lakini tatizo lake nae anadharau then hapend kushauriwa

You are right!,hiki kitu nimekisema pia katika uzi wangu huu,lakini kuna watu humu ambao hawamjui vizuri jaydee zaidi ya kumwona kwenye magazeti na na kumsikiliza redioni,wanapinga hiki kitu.jaydee huwa hakubali kabisa kujishusha na hii inamponza sana.
Inawezekana kabisa mwana Fa ni mnafiki na msalizi kama wengi wanavodai humu,lakini tusimshabie jaydee hata kwa mabaya.
Kama ni muungwana alishindwa nn kumfuata Fa wakayaongea maana sisi hayatuhusu.
 
Join Date : 11th June 2013
Posts : 13
Rep Power : 303
Likes Received2
Likes Given0
 
Join Date : 11th June 2013
Posts : 13
Rep Power : 303
Likes Received2
Likes Given0

Kujiunga jana ama leo hii haisaidii,ni dalili ya kujitetea,ni bora ujenge hoja kuliko kuangalia profile yangu,maana haitasaidia kusema nimejinha leo ama jana,jenga hoja kijana
 
ni upuuzi mno kuanzisha id mupya ili uweze kumtukana mtu! shame on mawingu and your fellow culprits!
 
Back
Top Bottom