Mapungufu yetu kama Taifa yalianzia hapa 1984 tulipobadili katiba ya Zanzibar

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,322
Reaction score
3,648
MAPUNGUFU YETU KIMAADILI YALIANZA KWENYE MICHAKATO HII

Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1984 na 1992 upande wa Jamhuri pia Uandishi wa Katiba ya Zanzibar mwaka 1984 na mabadiliko yalofuatia mwaka 2002.

Mwaka 1984 tuliona mabadiliko kwenye katiba ya Tanzania na Zanzibar,kama leo hatuitaki katiba ya 1984,tusemeje hapo!kwamba wakati uliwadia, na fursa ikajitengeneza kwa kundi ambalo siku zote limekuwepo likiwa na madai yake maalum, lilitumia fursa hiyo (seized the moment) kujinyanyua fursa ya kurekebisha ama kutengeneza katiba,je hali hiyo haitajirudia kwenye katiba mpya tunayoitaka hivi sasa!?

Katiba ya Warioba;-

Kumbukumbu zinatuambia,Bunge la Katiba lilivunjika kwa sababu pande mbili hazikuafikiana na ukitazama sababu zenyewe tunarudi pale pale hoja zote hazikuzingatia UTU wetu bali tofauti zetu - Tuliishia Patupu.

Suala la kuingia Ikulu tutaliwekaje kwenye hiyo katiba mpya tunayoitaka?

Mwaka 2015 kipaumbele kiiikuwa ni kuingia Ikulu,CCM kuingia Ikulu na Chadema kuingia Ikulu,kila upande focus kubwa ilikuwa kuingia Ikulu sio kuwatumikia Wananchi. Na hili limekuwa likisemwa na vyama vyote kwamba nia na dhamira ya vyama vya Siasa ni kuingia Ikulu.

Nitoe mfano,Chukulia Hayati Magufuli ambae aliiba itikadi na Sera za Chadema akaenda nazo kwenye uchaguzi mwaka 2015 na alivyoshinda akaanza kutekeleza sera za Chadema, lakini yeye ndiye akawa adui namba moja wa Chadema toka anaapishwa! Halafu Chadema walokuwa wakipinga Ufisadi katika uchaguzi huo wa 2015 wakamchukua Hayati Lowassa na kumpa sifa zote!

Mfano mwingine,ACT wanaojiita Wajamaa na Wazalendo leo wanapigania Uzanzibar!

Tusiandae ukumbi bila kujua sherehe itakuwa vipi, mshereheshaji ataleta sherehe iliyosheheni burudani hata watoto wadogo wakaziona tukiwa tumejisahaulisha kuwa zilikuwepo chinichini miongoni mwetu tokea uhuru.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Shamba darasa la Uongozi,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effects of microfinancing on poverty reduction.
 
Respect kwa vile Tume ya Nyalali (1991), Tume ya Kisanga (1999),iliyoleta Katiba ya Warioba.
 
Ikulu ndio inaamua kila kitu Tanzania.
Kufikiria katiba mpya ndio itaiwezesha CHADEMA kuingia Ikulu ni kukiri CCM haiko Ikulu tena kwa ridhaa ya watu wengi bali ujanja ujanja tu wa dola.
 
MAPUNGUFU YETU KIMAADILI YALIANZA KWENYE MICHAKATO HII

Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1984 na 1992 upande wa Jamhuri pia Uandishi wa Katiba ya Zanzibar mwaka 1984 na mabadiliko yalofuatia mwaka 2002.

Mwaka 1984 tuliona mabadiliko kwenye katiba ya Tanzania na Zanzibar,kama leo hatuitaki katiba ya 1984,tusemeje hapo!kwamba wakati uliwadia, na fursa ikajitengeneza kwa kundi ambalo siku zote limekuwepo likiwa na madai yake maalum, lilitumia fursa hiyo (seized the moment) kujinyanyua fursa ya kurekebisha ama kutengeneza katiba,je hali hiyo haitajirudia kwenye katiba mpya tunayoitaka hivi sasa!?

Katiba ya Warioba;-

Kumbukumbu zinatuambia,Bunge la Katiba lilivunjika kwa sababu pande mbili hazikuafikiana na ukitazama sababu zenyewe tunarudi pale pale hoja zote hazikuzingatia UTU wetu bali tofauti zetu - Tuliishia Patupu.

Suala la kuingia Ikulu tutaliwekaje kwenye hiyo katiba mpya tunayoitaka?

Mwaka 2015 kipaumbele kiiikuwa ni kuingia Ikulu,CCM kuingia Ikulu na Chadema kuingia Ikulu,kila upande focus kubwa ilikuwa kuingia Ikulu sio kuwatumikia Wananchi. Na hili limekuwa likisemwa na vyama vyote kwamba nia na dhamira ya vyama vya Siasa ni kuingia Ikulu.

Nitoe mfano,Chukulia Hayati Magufuli ambae aliiba itikadi na Sera za Chadema akaenda nazo kwenye uchaguzi mwaka 2015 na alivyoshinda akaanza kutekeleza sera za Chadema, lakini yeye ndiye akawa adui namba moja wa Chadema toka anaapishwa! Halafu Chadema walokuwa wakipinga Ufisadi katika uchaguzi huo wa 2015 wakamchukua Hayati Lowassa na kumpa sifa zote!

Mfano mwingine,ACT wanaojiita Wajamaa na Wazalendo leo wanapigania Uzanzibar!

Tusiandae ukumbi bila kujua sherehe itakuwa vipi, mshereheshaji ataleta sherehe iliyosheheni burudani hata watoto wadogo wakaziona tukiwa tumejisahaulisha kuwa zilikuwepo chinichini miongoni mwetu tokea uhuru.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Shamba darasa la Uongozi,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effects of microfinancing on poverty reduction.
Mgombea huru ndiyo kianzio cha demokrasia ya kweli TZ
 
Back
Top Bottom