Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kama vile ujenzi wa kuficha paa ulivyo mashuhuri sikuhizi, kwa wengi kuficha paa kunaokoa gharama za mabati. Sinza combine ilikua ni muokozi wa gharama za mabati miaka ya 1990.
Ujenzi huu ukianza kuwa maarufu baada ya askari wetu walikokwenda kusaidia harakati za ukombozi za Frelimo huko Msumbiji kurudi salama. Huu ulikua ujenzi maarufu uliotumiwa na Wareno huko Msumbji.
Ndani ya nyumba kulikua na sebule, chumba cha kulia chakula, jiko, bafu na choo na nyumba vitatu vya kulala. Wachache waliweka en-suite kwenye master’s room.
Changamoto za ujenzi wa paa la aina hii unakuja unapotaka kuvuna maji ya mvua. Inabidi uweke gutters zinazojitegea kwa kila upande.