Broken soul
JF-Expert Member
- Oct 24, 2013
- 459
- 131
Hapa kwa kweli mulugo mnamuonea
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wana jf kuna kituko nimekutana nacho leo hii ingefaa mnijuze kama na nyie mnakutana nacho na pia tushauriane kuhusu dawa ya jambo husika. Ishu ni kuwa mwanangu anasoma darasa la pili shule binafsi VIBE kinyerezi na tegemeo ni kuingia darasa la tatu wakifungua; cha ajabu nimekabidhiwa ripoti ya mtoto inayosema shule ikifunguliwa atarudia darasa na kusoma hilo hilo la pili kwa kuwa hakufikisha wastani wa marks 70 walizojipangia. Imeonyeshwa nafasi yake darasani ni wa 16 na kwa maana hiyo nusu ya darasa watakuwa wanarudia kwa kuwa darasa lina wanafunzi karibia ya thelasini. Sasa hii maana yake nini ni kwamba sasa tujiandae kuona watoto wanamaliza la saba wakiwa na miaka 20 au 21 umri sawa na ule wa wale wanaokaribia kumaliza chuo kikuu. Hapo sasa na umri huo apate bahati ya kuingia sekondari na hizo rudiarudia atapoteza miaka mingine 12 hapo umri utakuwa miaka 33; sasa aende chuo aje kuingia kwenye maisha atakuwa ameshakuwa m-babu wa miaka 50. Hivi hii wizara ya elimu kazi yake nini hadi kila mjinga mwenye vijihela vya kufungua shule anaanzisha ujinga anaoujua yeye? Hivi hawa kina MULUGO na elimu zao za kuungaunga ndio wamekuwa majanga kiasi hiki? huyu mtoto wangu yuko bright na namkubali hata faili lake lina marks kuanzia 80 kwenda juu lakini sizo zilizowekwa kwenye ripoti; na hapa nyumbani anategemewa na watoto wenzake tena wa darasa la tano wa shule za serikali anawafanyia hesabu, na kuwajibia masomo mengine pia lakini yeye arudie mwaka wakati wanafunzi wake wanasonga mbele kuingia la sita. Hivi hapo darasa la saba si wanafanya mitihani ileile ya kwenda sekondari? na utaratibu wa kurudia madarasa si ni darasa la nne na form two? hii ya kurudishwa nyuma darasa lolote ili watu wavune pesa imeidhinishwa na nani? MULUGO? hebu nijuzeni wenzangu!
Highest degree ya ujinga.....ebu kajipange we mtoa post c vizuri kuzihirisha ujinga wako kwa watu wanaofikiri....
safi sana,imekaa vizuri hiyo!Ni utaratibu wa shule hiyo -- si wa Wizara au waziri, ambao kama mzazi ulipaswa uufamu na kuuridhia wakati mwanao anajiunga na shule hiyo! Na hili si jipya, shule nyingi tu za binafsi zina wastani wao ambao mara zote huwa juu ya ule wa Wizara
Hahahahahaha!Mtoto wa darasa la pili afundishe darasa la tano? Tena hesabu?
Hesabu za darasa la pili ni kujumlisha, kutoa (za kukopa kidogo), kugawanya (njia fupi au ndefu bila baki) na kuzidisha.
Darasa la tano tayari tunazungumzia hesabu za sehemu, decimali, masaa, maumbo kama msitatili, mraba, pembe tatu. Bila kusahau ankra, asilimia, vipeo na vipeuo. Sasa dogo wa la pili anagusaje hapa? Darasa la tano ni mziki mwingine wewe, usitudanganye.
Kwa kawaida darasa la kwanza na la pili ni darasa la maksi mia mia, ukifeli sana 90 (hapa umefeli kweli), maana unaweza kuwa na wastani wa 90 hafu kwenye 20 bora haumo, sasa mwanao kashindwa kufikisha 70% unalalama eti mwanao ni kichwa, tupa kule.
Kama vipi mtafutie shule nyingine ambayo haina mitihani!
Mulugo unamuoea bure hapa, hiyo ni shule ya kibiashara wanatafuta survival kupitia pesa zenu mnazowalipia watoto kama ada, unategemea lipi watoto wote wakifaulu na wakati huo huo udahili umeshuka kutokana na ushindani na ongezeko la utitiri wa shule zinazoanzishwa Kila kukicha? Na hii ni ulimbukeni kwa wazazi kusomesha shule za binafsi hata kama shule yenyewe haina sifa, shule itaitwa VIBE unatarajia nini? Cha msingi tafuta shule nyingine mwanao akasome!
Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
Pure Math gani hiyo mzee ya backhouse au? naongelea pure and applied maths for your info; kwa wale wa enzi ya mordern maths form six wa mikondo ya science tofauti na pcm wanatumia kitabu hicho hicho kinachotumiwa na form three wanaochukua additional maths sasa kuna shida gani hapo kipanga wa form three kuwakalisha chini hao mabundi wa kupasua vyura? Mpaka hapo nimekupa uwezekano ule unaoitwa one-o-one si kwa watu waliokuwa wanashusha namba hata za madarasa matatu mbele kwa unyama wao binafsi wa kuzaliwa. Sijaona propaganda hapo aisee bali naona tu taswira ya kilaza fulani hivi. Sasa bosi wangu kama leo hii nimeweza ku rediscover all the great laws of mordern science and technology you still dont figure am a person of higer mind? [QUATE]
Unaonekana ni mwelewa na mjuzi a mambo bt as a "reasonable and prudent" father u culd have applied diligently some efforts kujua taratibu za shule husika hasa wastani ambao mgt ya shule imejipangia kwa mwanafunzi kuvuka darasa bfr admiting ua son. And by so knowing ungefuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mwanao kuona kama anakidhi matakwa ya 70% katika mitihani yake hata kama anawakalisha std V.
U still remain with some options either arudie au ahesabike amefail to suit the academic standards of that school na hivyo mpeleke shule nyingine inayopokea wastani wa below 70% japo mwisho wa siku wote watafanya the same National exams. Mwanao anaweza kuwa ana uwezo lakini hakufanya vizuri mitihani husika kwa kipindi husika na sidhani kama wanatumia mfumo wa continuous assesment.
Na kuhusu ushahidi wa kwamba una papers zake ambazo amescore vizuri is much better uwaone wahusika wakueleze na kama kuna hila zilifanyika ureport kwa MULUGO akishindwa kuchukua hatua ndipo umlaumu.
Umeongea vizuri kama mlokole ila hujasema lolote kuhusu umri wa kuanza shule na umuhimu wake ikiwa watoto watakuwa wanarudia madarasa kirejareja; si watahitimu wakiwa vibabu? na je hiyo imo kwenye sera za elimu kitaifa? mimi najua kurudia ni form two na std four pekeePure Math gani hiyo mzee ya backhouse au? naongelea pure and applied maths for your info; kwa wale wa enzi ya mordern maths form six wa mikondo ya science tofauti na pcm wanatumia kitabu hicho hicho kinachotumiwa na form three wanaochukua additional maths sasa kuna shida gani hapo kipanga wa form three kuwakalisha chini hao mabundi wa kupasua vyura? Mpaka hapo nimekupa uwezekano ule unaoitwa one-o-one si kwa watu waliokuwa wanashusha namba hata za madarasa matatu mbele kwa unyama wao binafsi wa kuzaliwa. Sijaona propaganda hapo aisee bali naona tu taswira ya kilaza fulani hivi. Sasa bosi wangu kama leo hii nimeweza ku rediscover all the great laws of mordern science and technology you still dont figure am a person of higer mind? [QUATE]
Unaonekana ni mwelewa na mjuzi a mambo bt as a "reasonable and prudent" father u culd have applied diligently some efforts kujua taratibu za shule husika hasa wastani ambao mgt ya shule imejipangia kwa mwanafunzi kuvuka darasa bfr admiting ua son. And by so knowing ungefuatilia kwa ukaribu maendeleo ya mwanao kuona kama anakidhi matakwa ya 70% katika mitihani yake hata kama anawakalisha std V.
U still remain with some options either arudie au ahesabike amefail to suit the academic standards of that school na hivyo mpeleke shule nyingine inayopokea wastani wa below 70% japo mwisho wa siku wote watafanya the same National exams. Mwanao anaweza kuwa ana uwezo lakini hakufanya vizuri mitihani husika kwa kipindi husika na sidhani kama wanatumia mfumo wa continuous assesment.
Na kuhusu ushahidi wa kwamba una papers zake ambazo amescore vizuri is much better uwaone wahusika wakueleze na kama kuna hila zilifanyika ureport kwa MULUGO akishindwa kuchukua hatua ndipo umlaumu.