Mara: Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka minne

Mara: Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kulawiti mtoto wa miaka minne

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
Maiga Maginga (18), amehukumiwa kifungo cha maisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Serengeti baada ya kukiri kumlawiti mtoto wa miaka minne.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 31, 2019 na Hakimu Mkazi, Adelina Mzalifu baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kulawiti.

Hakimu Mzalifu amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 154 (1) (a) (2) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Faru Mayengera ameieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 25, 2019.

Amesema alimkuta mtoto huyo akichunga mifugo jirani na nyumbani kwake, alimchukua na kumlawiti.

Amesema mtoto huyo alipiga kelele na mshtakiwa alimuachia lakini alipoulizwa aliyemfanyia kitendo hicho alimtaja mshtakiwa huyo na alipokamatwa alikiri kufanya kitendo hicho.

Mayengera amesema hata alipofikishwa katika ofisi ya Kijiji na polisi alikiri kufanya kitendo hicho, “pia alipoulizwa na hakimu mara tatu kama amefanya kitendo hiki alikiri.”

Baada ya mshtakiwa huyo kukiri kosa, mwendesha mashtaka huyo aliiomba mahakama kutafsiri sheria kulingana na kosa alilotenda.

1572593432422.png
CHANZO: Mwananchi
 
Huyo ana miaka [emoji725], nafIkiri hastahili kifungo cha maisha kutokana na umri wake.
 
Wangechinja tu huko mbeleni anaweza kuja kupata msamaha kwa bahati akaja akafanya tena
 
Hawa ******* wana nini lakini???😡😡😡😡😡😡
 
Wanaume wa mkoani wameanza kua mapimbi sasa.

Ngoja wa dar tuandae makoo-Tips mida mida kidogo.
 
Kwanini leo kesi za ubakaji na ulawiti ni nyingi sana
 
kifungo cha maisha?! noop Haitoshi

Auliwe kwa kuachwa chumba kisicho na chakula Afe taratibu huku akikumbukia aliyotenda

Asinyongwe/ ashukuru mungu mimi sio mtoa hukumu
 
Unaona alichofanya ni sawa?umemfikiria huyo mtoto alielawitiwa? Na miaka 18 ni mtu mzima kwa mujibu wa sheria
Unanjibu mm mkuu alosema ajatendewa haki kwa kifungo cha maisha
 
Back
Top Bottom