Bibie wazee wanaangalia idadi ya ng'ombe
Ifike mahali kama bride price au mahari ni kuthaminisha unamiliki mtu au nakupa mwanangu, iondolewe kabisa.
Pia kuoa na kuolewa ifike mahali iwekewe vigezo kabisa ambavyo havitengenezwi kwa miezi mitatu kama maandalizi ya harusi, bali vigezo hivyo vinaandaliwa tangu mtu ana miaka sita.
Maana yake wazazi wa pande zote watahusika na maandalizi ya watoto hao kukidhi vigezo vya kuwa mke / mme. Na ambaye hatotimiza vigezo basi hatopata mke wala mme hata awe na pesa au awe hendisamu au biutifuli.
Hii ingejenga discipline ya hali ya juu kwenye jamii maana naamini hakuna mazazi anayetaka moto wake awe hohehahe ambaye yupoyupo tuu mtaani haoi, haolewi anawapa mimba tuu wasichana hovyo au anabeba mimba na wanaume tofauti tofauti.
Najua sio wote wangeingia kwenye ndoa wapo ambao wangepatikana wakaidi ila kwa wale waliolelewa na kukuzwa kwenye maadili na vigezo vya kumuandaa binadamu mwenye utu, utashi, hekima, busara, kujitambua, kujiamini kwenye manufaa, n.k. wa kufanana na hayo basi jamii yetu ingekuwa na kesi chache sana kama hizi za baba kumlala binti yake wa kumzaa, hata kama aligundua hao watoto wote sio wake bado anakuwa na utu na utashi wa kusitiri faragha ya watoto wale na kuwaacha waje kuishi maisha yao.
Jamii ya leo, wazazi hawana discipline, watoto wanaona baba yuko na mchepuko wake mtaani obvious nao wakikua wataona ndo maisha na jambo la kawaida. Watoto wanashuhudia mama analiwa na fundi chumbani kwa baba yao au muuza genge au anamahusiano na mfanyakazi mwenzie kazini ambao wanaleta mahaba yao hadi nyumbani na watoto wanaona au bosi wa mama yao. Hapo watoto wanajenga ufahamu kuwa mama kuchepuka ni jambo la kawaida.
Watoto wanashuhudia wazazi wanapigana na kugombana mbele yao, wanajawa na hulka ya ugomvi na ukorofi na wakija kuwa na ndoa zao hata wakipata wenzi wataratibu bado wataanzisha vurumai tuu sababu walikua kwenye mazingira ya ugomvi, matusi, ulevi, ukarofi na ustaarabu sifuri.
Kuna vitu unaweza kuvumilia kwenye mahusiano sababu hakuna mwanadamu mkamilifu, ila kuvumilia vipigo, kubakwa na manyanyaso kwa watoto ni mbaya sana maana inaharibu saikolojia nzima ya mtendwaji na washuhudiaji.
Hiyo ya kuangalia mali, ni tamaa tuu. Mtoto wa kike thamani yake ni kubwa mno saa ingine nawaza ningekuwa na binti nisingetaka aolewe maana binti huwa anajitoa sana kwa wazazi, sasa akiolewa anahamishia kujitoa kwenye familia alikoolewa. Ila kukiwa na discipline kwenye jamii ipandwe kwa watoto tangu wadogo na wazazi / walezi nao waishi hiyo discipline matatizo mengi sana ya jamii yataisha.
Kasinde.