Mara: Mgambo achomwa kisu na kufariki kituo cha Polisi, alimzuia aliyemchoma kumfanyia fujo mkewe

Mara: Mgambo achomwa kisu na kufariki kituo cha Polisi, alimzuia aliyemchoma kumfanyia fujo mkewe

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Askari mgambo Fred William (47), mkazi wa Kijiji cha Mkengwa, Rorya mkoani Mara, amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu shingoni akiwa katika kituo cha polisi Mkengwa, wakati akimzuia aliyemchoma kisu kutomfanyia fujo mke wake aliyekimbilia kituoni hapo kuomba msaada.

SOURCE: EA Radio
===

Rorya:Mgambo wa Kijiji cha Mkengwa katika Kisiwa cha Kibuyi wilayani hapa amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu shingoni alipokuwa akijaribu kumzuia mtu mmoja asifanye fujo katika kituo cha polisi.

Tukio hilo limetokea Agosti 30, 2022 baada ya mgambo huyo kumzuia mtu huyo kuingia ndani ya kituo cha polisi kwa lengo la kumpiga mke wake aliyekimbilia kituoni hapo, kutokana na kumtishia kumuua.

Shuhuda wa tukio hilo, Nico Azaria aliliambia Mwananchi kuwa mke na mume walifika kituoni wakiwa wanakimbizana, jambo lililowashtua watu waliokuwepo kituoni muda huo na kumlazimu askari mmoja kutoka nje ili kumzuia mwanamume huyo asiingie ndani ya kituo.

“Mimi nilikwenda kumtolea dhamana ndugu yangu, sasa wakati askari mmoja akichukua maelezo kutoka kwa ndugu yangu huyo, ghafla wakaja mke na mume wakiwa wanakimbizana.

“Askari mmoja alipoona hivyo alitoka nje na kumwambia yule mwanamke aingie kituoni haraka. Baada ya kuingia mwanaume naye akawa amefika akataka kuingia kituoni, askari akamwambia ishia hapo hapo,” alisema Azaria.

Aliendelea, “Lakini yule mtu alikaidi amri hiyo akaendelea hadi alipofika mlangoni na kukutana na mgambo aliyekuwa amesimama kumzuia asiingie na kisha kumshika kwa nguvu kama watu waliokumbatiana.

Azaria alisema kuwa baada ya mgambo huyo kumshika hivyo mtu huyo alimng’ata bega la kulia ndipo mgambo akamuachia na kisha mtu huyo kuchomoa kisu na kumchoma mara mbili shingoni upande wa kulia.

“Hakuna mtu aliyeweza kumsogelea jamaa, hata askari wote wawili waliokuwepo kituoni pamoja na mgambo mmoja ambaye hakujeruhiwa walishindwa kwa sababu hawakuwa na silaha hivyo jamaa alikimbia na kutokomea kusikojulikana,” alisema.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkengwa, Rajabu Obure alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumtaja marehemu kuwa ni Fred William (47) mkazi wa kijiji hicho.

“Aliyefanya tukio hili namfahamu kwa jina la utani la Njiwa, siyo mkazi wa hapa, huwa anakuja na kujishughulisha na uvuvi kisha kuondoka, ni mkazi wa Kijiji cha Kyangasaga, Wilaya ya Rorya,” alisema.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom