Mara moja moja tembelea CTC, utanishukuru

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Ndiye siye, siye ndiye!

Ukiwa na ratiba ya kutembelea maeneo haya kuna namna itakukumbusha jinsi ya kuishi, sio kwa maana ya unyanyapaa bali kujilinda na kuwalinda wengine.

Pamoja na elimu utakayoweza kuipata ukiamua kuuliza wahusika, pia itakusaidia kurejea kazi ya macho yako.

Huku utaweza kupata marafiki ambao unapishana nao mitaani bila kujua. Sio kwa sura wala sio kwa shepu na hata tabasamu usoni.

Hakika, USIPIME kwa MACHO.
 
CTC ndo wapi huko mkuu?
 
Kijana mbona kama unaweweseka.
shida ni nini hasa?
tulia ulete ujumbe unaoeleweka hapa mbele ya wanaume.
 
Umeongea point sana, kwa ambao hawajawahi kwenda hawawezi kukuelewa, nakumbuka niliwahi kufata PEP kule, ebana kuna pisi za shule ya msingi na sekondari zinakula njugu, kuna pisi under 30 ukiziona mtaani unajua umepata tena unawaambia masela hii pisi nakula kavu niifaidi, naipakia na mkongo kumbe unajikaanga kwa mafuta yako. Mungu atulinde tu kwa kweli.
 
Uzi unalengo zuri ila umekaa kichochezi chochezi😁
 
Wenyewe hawapendi uwaseme HIVYO
 
Mambo mengine tujifunze kwa kushuhudia na wala si kwa kusimuliwa.
Wengi walikuwa wanajidai sana kutafuna Pisi kali, kumiliki ma sponsor wa maana mjini
 
Hahaaa.,...eti unaipakia mkongo
 
Vipi mkuu ulitembelea kuchukua vidonge?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…