Balqior
JF-Expert Member
- Jun 8, 2021
- 2,406
- 8,039
Habarini,
Kwa baadhi ya watu humu kama mnavonijua humu jukwaani, mimi sio mtu wa mambo ya kiroho, ni mkristo, ila ni mkristo jina, kanisani siendagi kabisa dhambi ninazo nyingi sana, sisomagi biblia Wala sio mtu wa maombi, ila kuna kitu kimeanza nitokea hivi karibuni kimeanza kama miaka 2 iliopita, ambacho sijawahi kuki-experience tangu nizaliwe.
Mara nyingi naota ndoto tofauti tofauti, lakini ndoto zote zikiwa na theme moja "Mungu" au "Yesu"
1) Kipindi nlikuwa sina kazi wala hela na nlikuwa nimefulia, usiku nliota Mungu amesimama mbele yangu, sikumuona uso lakini nlivoona uwepo tu huo, kitu ndani mwangu kiliniambia kuwa huyo ni Mungu Muumba wa mbingu na nchi, kwenye maisha ya mchana huwa nasemaga siku nikimuona Mungu cha kwanza ntakachomuomba ni hela nyingi, lakini nlivyomuona ndotoni siku hiyo, wazo la kumuomba hela halikuwepo, nilipiga magoti mbele yake na kulia nikimwambia kuwa nimemfelisha, hakujibu chochote ndoto ikaishia hapo.
2) Siku nyingine nikilala naota natembea na Mungu k.v Abraham kwenye biblia alivokuwa anatembea na Mungu, huku tunaongea.
3) Siku ingine nikilala naota kimoyomoyo naomba, siku nyingine naota roho yangu inaimba na kumsifu Mungu, ilhali kiuhalisia muda wa mchana siwezi omba hata dakika moja, na mchana huwa sina desturi ya kumuimbia Mungu.
4) Siku nyingine naota roho yangu inaniambia inabidi nijenge mahusiano mazuri na Yesu.
5)Siku nyingine naota naondoa machukizo kanisani.
Hizi ndoto zimekua zikijirudia kwa nyakati tofauti tofauti, kuna mtu mwingine ameshawahi pitia hii hali?
Nikikaa mahali nikiwaza dunia ilivyo tamu, nafadhaika, lakini moyoni ukweli naujua kwamba natakiwa niachane na anasa za dunia, niishi maisha matakatifu nimfate Mungu, hapa nilipo nahesabu gharama za kumfata Mungu, ili nikianza nisiishie njiani.
Kuna mtu ishawahi mtokea hii hali, naamini si mimi tu ninaepitia hii. hali, wapo wengine wanapitia hii hali ila kwa namna tofauti.