Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Wakuu, kuna jambo kuhusu lugha ya Kiswahili limekuwa likinifanya nifikirie kwa kina.
Nakumbuka nikiwa shule ya msingi, mwalimu wetu aliwahi kumsahihisha mwanafunzi mwenzetu aliyesema, “Nionyeshe kalamu yangu ilipo.”
Mwalimu alieleza kuwa neno “onyesha” lina mzizi tofauti na “onesha”, akihusisha la kwanza na neno “onya” na la pili na “ona”.
Tangu wakati huo nimekuwa nikijiuliza: Je, mwalimu alikuwa sahihi kisarufi, au kuna mambo kuhusu mizizi ya maneno ambayo hatukuyafahamu vizuri?
Wewe kama mdau wa lugha, una maoni gani kuhusu hili? Je, kuna maneno mengine tunayoyatumia kila siku bila kuelewa asili na maana yake kwa usahihi?
Hebu tupeane maarifa kidogo wakuu