Mara nyingii nyakati za usiku nimekuwa nikiota ndoto nikiwa naongoea na watu waliokufa hasa baba yangu mzazi

Arch Barrel

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2024
Posts
434
Reaction score
1,126
Habari za usiku wanaJF , ndugu zangu naomba nipate msaada kutota kwenu.

Mara nyingii nyakati za usiku nimekuwa nikiota ndoto nikiwa naongoea na watu waliokufa hasa baba yangu mzazi na mdogo anaenifuata. hawa wote ni wafu,
Mdogo wangu alitangulia kufarikiriki December 2010 kipindi hicho mimi ndio nilikuwa nimemaliza form 4 nilikuwa nasubiri matokeo, babaangu alifariki 2017 wakati ambao nilikuwa namalizIa UE.

Muda wote nikiwa nao kwenye ndoto zangu nimekwa nikiota tukiwa wote kwenye wakati wa furaha. Nimekuwa nikiyaona yale maisha ambayo nimekulia, nimekuwa nikimuona babaabu halisi. Mdogo wangu mara nyingi nimekuwa nikishirikiana nae kwenye hizi hustle za kila siku . Nina ndugu wengi wengi sana lkn mara nyingi nimekuwa nikiomuota BABA na MDOGO WANGU,

Lakn pia kuna wakati naota kufanya mitihani ya shule ambayo sikujiandaa. kwenye ndoto hii mara nyingi huwa nakuwa na mshituko, hata ninaposhituka lazima mapigo ya moyo yabadirike.

Huu ni ukweli ninaowaeleleza. Haiwezi ikapita wiki moja sijaota nikiwa na Babaangu au mdogo wamgu .

Hii ina maana gani?
 
"Dreaming of a test where you're unprepared or you're performing poorly usually means that you feel anxious and underprepared about a situation in your waking life."

Kuota unafanya mitihani ambayo haujajiandaa maana yake ndio hii....jitathmini sasa wewe mwenyewe haujajiandaa katika nini.
 
Hiyo ni sababu tu ya zile kumbukumbu nzuri mlizokuwa nazo na inaonekana kuwa huwa hata ukiwa macho huwa unawawaza na kuwakumbuka mara kwa mara hivyo unapolala ubongo wako unakuwa kama una deduct matukio na mawazo/fikra ya siku nzima katika subconscious mind ndio unahisi kuwa ni ndoto.
 
"Dreaming of a test where you're unprepared or you're performing poorly usually means that you feel anxious and underprepared about a situation in your waking life."

Kuota unafanya mitihani ambayo haujajiandaa maana yake ndio hii....jitathmini sasa wewe mwenyewe haujajiandaa katika nini.
Truly, what can i do.
 
Ni ndoto tuu hizo zitakwisha zenyewe. Ni wazi vifo hivyo bado vinakugusa sana kwenye maisha yako, yaani unafikiria sana kuhusu hilo, sasa linakujia ya ndoto. Endelea na maisha bwa mdogo.
 
Hizo ni kumbukumbu tu mkuu zile best moments za ndugu yako na mzee wako.

Mimi pia mara nyingi naota naongea na mama, tunapiga stori na hua nikiota hivyo asubuhi nikiamka siku yangu inakua nzuri sana.

Napenda mara zote niwe naota nikiwa na marehemu mama yangu tukizungumza ama hata kumuota tu nimemuona najisikia vizuri sana na siku yangu hua nzuri sana.

Binafsi mdoto ya kumuota mama yangu hua ndoto nzuri zaidi nayoipendelea kuiota kuliko zote.

Endelea kupumzika kwa amani mama. Kijana wako naendelea kupambana na sitakuangusha.
 
Mimi mwenyewe ndoto za walioshatangulia zinanisumbua wastani haipiti wiki 2 sijaota ndoto aina hiyo, nyingi ni za baba yangu kunipa maelekezo ya maamuzi au tahadhari ya mambo fulani kwenye maisha yangu au familia kwa ujumla, sometimes zinachosha why me??? Hata ndugu wa mbali nao nawaota hasa waliofariki miaka ya hivi karibuni
 
Bado watu wa mambo ya ulimwengu wa rohoni hawajatia mguu. Subiri tu waje. Mpaka utaogopa yaani. Andaa na sadaka ya shukrani na maungamo kupeleka kwa mtumishi atakayekwenda kukuombea ili uweze kuondokana na ndoto hizo maana vita unavyopigana katika ulimwengu wa kiroho ni kubwa 😁😁😁

Screenshot_20240629_043811_Gallery.jpg
 
UKIOTA KEMEA KWA JINA LA YESU UTALETA MREJESHO HAPA KAMA YATARUDIA
 
Bado watu wa mambo ya ulimwengu wa rohoni hawajatia mguu. Subiri tu waje. Mpaka utaogopa yaani. Andaa na sadaka ya shukrani na maungamo kupeleka kwa mtumishi atakayekwenda kukuombea ili uweze kuondokana na ndoto hizo maana vita unavyopigana katika ulimwengu wa kiroho ni kubwa 😁😁😁

View attachment 3028719

Habari za usiku wanaJF , ndugu zangu naomba nipate msaada kutota kwenu.

Mara nyingii nyakati za usiku nimekuwa nikiota ndoto nikiwa naongoea na watu waliokufa hasa baba yangu mzazi na mdogo anaenifuata. hawa wote ni wafu,
Mdogo wangu alitangulia kufarikiriki December 2010 kipindi hicho mimi ndio nilikuwa nimemaliza form 4 nilikuwa nasubiri matokeo, babaangu alifariki 2017 wakati ambao nilikuwa namalizIa UE.

Muda wote nikiwa nao kwenye ndoto zangu nimekwa nikiota tukiwa wote kwenye wakati wa furaha. Nimekuwa nikiyaona yale maisha ambayo nimekulia, nimekuwa nikimuona babaabu halisi. Mdogo wangu mara nyingi nimekuwa nikishirikiana nae kwenye hizi hustle za kila siku . Nina ndugu wengi wengi sana lkn mara nyingi nimekuwa nikiomuota BABA na MDOGO WANGU,

Lakn pia kuna wakati naota kufanya mitihani ya shule ambayo sikujiandaa. kwenye ndoto hii mara nyingi huwa nakuwa na mshituko, hata ninaposhituka lazima mapigo ya moyo yabadirike.

Huu ni ukweli ninaowaeleleza. Haiwezi ikapita wiki moja sijaota nikiwa na Babaangu au mdogo wamgu .

Hii ina maana gani?
Hata mimi kuna kipindi zilikuwa zinanijia mara Kwa mara, lakini Kwa sasa zimepungua. Nadhani ni kawaida kuwaota watu uliowapenda sana. Hapo inasikitisha lakini pia ni kama unapata faraja maana uliwamis na hakuna sehemu unayoweza kukutana nao tena isipokuwa kwenye ndoto.
 
Jini maiti...🤔. (au bas hamkawiagi kutuona maostadh n wachawi🚶🚶
 
Mimi mwenyewe ndoto za walioshatangulia zinanisumbua wastani haipiti wiki 2 sijaota ndoto aina hiyo, nyingi ni za baba yangu kunipa maelekezo ya maamuzi au tahadhari ya mambo fulani kwenye maisha yangu au familia kwa ujumla, sometimes zinachosha why me??? Hata ndugu wa mbali nao nawaota hasa waliofariki miaka ya hivi karibuni

Itafute maana yake, lazima ina ujumbe flani na ukiupata tu hautakaa uote tena.....tena mbona kama ipo wazi kuwa ina maelekezo/ tahadhari.
 
Ni kweli zinanisaidiaga lkn naona km ni too much kwanini mimi tu ndiye naota, misiba ikikaribia naonyeshwaga sana, km wa ndg yangu niliota mwaka jana live kabisa nilipomwambia kumpa tahadhari akaniambia nina malaria imepanda kichwani mwaka huu kaondoka, huo ni mfano tu zipo nyingi za aina hiyo mpk sasa nikihesabu ni vifo kama 5 kwenye familia niliota kabla havijatokea

Ndugu wa kiafrika tunajuana kwa fitina ikitokea kuna wananipangia ubaya naoteshwa, au kuna ambae ana jambo lake juu yangu liwe baya au zuri si mara zote basi nitaota.......
 
Back
Top Bottom