Mara nyingii nyakati za usiku nimekuwa nikiota ndoto nikiwa naongoea na watu waliokufa hasa baba yangu mzazi

Sasa ulitaka nani awaote kama sio wewe mkuu?
 
Kuna kipindi baba mkubwa alikuwa anaumwa sana kalazwa hospitali.Baba aliota yupo na babu ambae kwa wakati huo alikuwa marehemu,walikuwa baba,babu na baba mkubwa wamekaa,baada ya muda baba aliondoka na baba mkubwa akamwacha baba .Haikupita wiki baba mkubwa alifariki
 
Ukiona unaota hizo ndoto za watu waliokufa hao ni mizimu wanawasiliana na wewe kukupa ishara fulani mara nyingi huwa wanamaanisha ufanye maombi au ujikinge kutokana na matatizo au vikwazo mbalimbali vya maadui.
Na kuota uko shule unafanya mtihani maana yake mambo yako yatarudi nyuma maana yake inaweza ikawa kufilisika au kupata janga la aina yoyote hivyo unapewa ishara ili ujipange
 
Pole sana,ndoto juu ya wapendwa wako hao ni kwa sababu ni watu uliotumia muda mwingi nao,lkn ni watu walioushiba moyo wako haswa,kujirudia kuwaota ni kwakua kila dakika/sekunde akili yako hujenga taswira zao.
Kuota upo kwenye mitihani ambayo hujajiandaa au upo shuleni unasoma ilhali ulishamaliza shule ni ishara ya kurudi nyuma/kurudishwa nyuma kwenye jambo fulani.
Tenga muda wako na rasilimali kidogo kulingana na uwezo wako,waombee kheri wapendwa wako hao huko walipo,tekeleza baadhi ya ahadi zao mf. anaweza kuwepo aliyekua akidhamilia kuunganisha ndugu/udugu,kujenga au kukarabati nyumba ya ibada,kusaidia watoto yatima n.k,timiza azma yao/zao kwa niaba yao.
Mwisho na Muhimu,fanya ibada na jiombee mwisho mwema ww binafsi.
 
Mimi nilikua namuota mdogo wangu mtoto wa mama mdogo ambao wote marehemu ,namuota Mara Ana furaha Mara uzuni Mara ananipa ujumbe Mara ya mwisho alikua ananilalamikia kwanini hatujamjengea nikawaambiwa wakubwa tukaenda makaburini kaburi lake bahati mbaya hatukuliona niliumia lkn hakuna jinsii kilichofata nikatafutiwa dawa za kihaya nikanyweshwa na Kuna maneno nikawa naongea tangu siku hiyo sijawai kumuota tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…