Mara paaap ushuru wa kuagiza magari 2024 umeshuka

Mara paaap ushuru wa kuagiza magari 2024 umeshuka

Ushuke na pesa ya uchaguzi tutatoa wapi?
Wanasiasa wana ruzuku za vyama vyao na miradi yao kedekede. Watuache tuishi, tujenge nchi, mikungu ya ndizi inaharibikia shambani magari shamba hakuna ushuru mkali sana.

Huku Tukuyu Gaia tunabebana kutoka Ngujubwaje kuja Tukuyu mjini ila bei yake sasa haikamatiki yaani ushuru sometimes mkubwa kuliko bei ya gari. Mbona ni kama tunakomoana!?
 
Kabisa mkuu. Ila kila nikicheki ushuru ni 50% ya bei ya gari yaani Mjapani Nampa usd 4000 na TRA 4000 nakata tamaa. Huu ushuru ni mkali sana. Gari sio anasa ni kifaa cha kuleta maendeleo, washushe huu ushuru.
wewe ushuru ni 100%
 
Kabisa mkuu. Ila kila nikicheki ushuru ni 100% ya bei ya gari yaani Mjapani Nampa usd 4000 na TRA 4000 nakata tamaa. Huu ushuru ni mkali sana. Gari sio anasa ni kifaa cha kuleta maendeleo, washushe huu ushuru.
Kodi hukokotolewa kwa kuzingatia thamani ya gari kwenye soko la dunia, gharama ya usafirishaji na bima. Ikiwa gari limenunuliwa kwa fedha za kigeni kiwango cha kubadilisha fedha cha siku husika kitatumika na sio ya wakati wa kuagiza gari hilo hivyo huenda ikatofuatiana na kiwango cha kikokotoo wakati wa kuagiza.

Umri wa gari unaweza kusababisha kodi ikaongezeka kutokana na uchakavu, kwa magari yaliyotengenezwa zaidi ya miaka 8 lakini haifiki miaka 10 kodi ya uchakavu ni 15% na gari lenye umri kuanzia miaka kumi na kuendelea tangu limetengenezwa kodi ya uchakavu ni 30%.
 
Back
Top Bottom