Mara: Watu wawili wafa maji Ziwa Victoria wakitokea kwa mganga wa kienyeji

Mara: Watu wawili wafa maji Ziwa Victoria wakitokea kwa mganga wa kienyeji

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Watu wawili wamefariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria katika Kijiji cha Burere wilayani Rorya mkoani Mara huku wengine wawili wakiokolewa.

Tukio hilo limetokea juzi Jumapili Septemba 29, 2024 saa 11 jioni wakati watu hao wakiwa wanatoka Kijiji cha Busanga walikokuwa wamekwenda kutibiwa kwa mganga wa kienyeji wakiwa wanaelekea Kijiji cha Busimbiti wilayani Rorya.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku 14 tangu kuzama kwa mtumbwi katika Kijiji cha Igundu wilayani Bunda na kusababisha vifo vya watu sita huku 14 wakiokolewa.

Soma Pia: Uokoaji wa miili ya watu 5 ziwa Victoria wasitishwa kwa muda kutokana na hali mbaya ya hewa na kukosa vifaa

Akizungumzia tukio hilo jana Jumatatu Septemba 30,2024 mjini Musoma , Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amesema baada ya mtumbwi huo kuzama watu wawili waliokolewa wakiwa hai muda mfupi baada ya tukio hilo, huku miili ya watu wawili ikiopolewa jana.
======
Kwahiyo tuseme kwamba walikosea mashariti ya mganga wa kinyeji?
 
Back
Top Bottom