Mara ya kwanza kuangalia mpira wa Ulaya ilikuwa mechi hii

Mara ya kwanza kuangalia mpira wa Ulaya ilikuwa mechi hii

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Nilikuwa bado shule ya msingi Kule kijijini hakukuwa na TV. Tulisafiri km 50 na dingi kwa baiskeli kwenda kumwangalia David Beckham. Ilikuwa ni 1999 fainali kubwa Man Utd na Bayen Munich.

Nilikuwa nashangaa tu,sielewi kitu. Jamaa wanazi wajuzi wa kandanda wakaja kunisimulia baadae kwamba Man U kashinda goli 2 ndani ya dakika 2 za nyongeza.

Kumbe bana katika maisha usikate tamaa. Tuambie wewe ipi ilikuwa mechi yako ya kwanza

#Bring back our Billionaire Mo Dewji
 
Nilikuwa Sinza kwa Remmy naishi na bro. Wakati huo DSTV ina channel mbili tu, supersport na Mnet tena Mnet inaanza kuoneka saa kumi na mbili jioni. Ikianza na kipindi cha Oprah, halafu hawakuwa na dish. Mechi ya kwanza LIGI za ulaya kuziona live shukrani ziwaendee DTV enzi zile 1996 yaani mmekaa sebuleni ghafla mnamsikia Tyler Perry anawaambia welcom to stamford bridge where Chelsea is playing against Newcastle, Faustino Asprilla is on the bench today, Keegan has decided to start Les Ferdinand and Allan Shearer upfront, the blues plays on the unchanged side that thrash Manchester United masterminded by master class man Gianflanco Zola. Hahaha raha tupu ilikuwa buree tukishuhudia mitanange ya nguvu. Euro 96 yoyote buree. Bidae wakapokea channel ten nao .
 
Juventus vs ajax uefa champion league final 1996 ...
Usinikumbishe ile squad ya Ajax, ikiongozwa na Patrick Kluivert, kushoto kuna finidi George, kulia kuna winger teleza Tijani Babangida katikati centre forward yupo Nwankwo Kanu. Mid fielders Edger David's akina de boer hii timu ilikuwa balaa. Tisa kumi yote timu yangu JUVENTUS TORINO bibi kizee kulikuwepo na akina gianluca Viali, fabrizzio Ravanelli, Zinedine Zidane, Lilian thuram, Atillio Lombardo sisi waitaliano tukibeba kombe siku hiyo. Huyu Viali akahamia Chelsea baada ya kuchomeka kombe na ikawa mwanzo wa mie kuipenda CHELSEA
 
France [emoji632] vs Senegal [emoji1211]
Kombe la dunia mwaka 2002
 
Nilikuwa bado shule ya msingi Kule kijijini hakukuwa na TV. Tulisafiri km 50 na dingi kwa baiskeli kwenda kumwangalia David Beckham. Ilikuwa ni 1999 fainali kubwa Man Utd na Bayen Munich.

Nilikuwa nashangaa tu,sielewi kitu. Jamaa wanazi wajuzi wa kandanda wakaja kunisimulia baadae kwamba Man U kashinda goli 2 ndani ya dakika 2 za nyongeza.

Kumbe bana katika maisha usikate tamaa. Tuambie wewe ipi ilikuwa mechi yako ya kwanza

#Bring back our Billionaire Mo Dewji
West Germany Vs Argentina World cup,1990,Ruud voller,Jurgen klinsmann,Thomas hasler,Diego maradona,
Nlikuwa nachungulia Video kwa Ngarama pale Shinyanga,Mtaa wa Majengo,nlikuwa shule ya Msingi,alikhwa Peke yake Mwenyewe Video Mtaa Mzima,Mzee yule wa Kihaya! Baada ya Hapo ikaja 1994 Mataifa huru ya Africa, kalusha Bwalya,na Kombe LA Dunia Marekani,Rashid yekin,Robert baggio,1994!
 
Usinikumbishe ile squad ya Ajax, ikiongozwa na Patrick Kluivert, kushoto kuna finidi George, kulia kuna winger teleza Tijani Babangida katikati centre forward yupo Nwankwo Kanu. Mid fielders Edger David's akina de boer hii timu ilikuwa balaa. Tisa kumi yote timu yangu JUVENTUS TORINO bibi kizee kulikuwepo na akina gianluca Viali, fabrizzio Ravanelli, Zinedine Zidane, Lilian thuram, Atillio Lombardo sisi waitaliano tukibeba kombe siku hiyo. Huyu Viali akahamia Chelsea baada ya kuchomeka kombe na ikawa mwanzo wa mie kuipenda CHELSEA
Sir Nwanko Kanu
 
Mimi nimeanza kuangalia soccer nyumbani nikiwa bado mdogo sana na sina kumbukumbu mechi yangu ya kwanza ya ulaya kuitazama timu gani zilikuwa zinacheza, kipindi hicho nilikuwa naangalia angalia tu,
 
Juventus vs ajax uefa champion league final 1996 ...

mimi juventus vs madrid.. uefa final 1997/1998 season.. via itv kupitia cfi.. kabla ya hapo kuna mechi nyingi niliangalia sikuwa na uelewa mkubwa.. world cup ya 1998 niliangalia yote najua mpira vizuri na hapo nilikuwa la 5
 
France Vs Brazil 1998 Final World Cup Hapohapo Naipenda France Mpaka Leo
United Na Bayern
 
Ilikuwa mewcastle na timu pinzani siikumbuki.kipindi hicho cha alan shearer.ndo mchezaji aliyenishawishi kuipenda Newcastle.
 
Mechi ya kwanza kuangalia ni fainali ya Brazil Vs Italy 94 World Cup ila RECORDED. Niliangalia mwaka 2001 huko mkoa fulani nyanda za juu kusini. Hatari sana.
 
Cameroon vs England kombe la Dunia mwaka 1990
 
Back
Top Bottom