Mara ya kwanza kuangalia mpira wa Ulaya ilikuwa mechi hii

Mara ya kwanza kuangalia mpira wa Ulaya ilikuwa mechi hii

Chelsea 2-1 Arsenal 2008
Ilikuwa pasaka hii siku Didier Drogba aliwaua Arsenal baada ya Bacary Sagna kutangulia
 


Nilikuwa bado shule ya msingi Kule kijijini hakukuwa na TV. Tulisafiri km 50 na dingi kwa baiskeli kwenda kumwangalia David Beckham. Ilikuwa ni 1999 fainali kubwa Man Utd na Bayen Munich.

Nilikuwa nashangaa tu,sielewi kitu. Jamaa wanazi wajuzi wa kandanda wakaja kunisimulia baadae kwamba Man U kashinda goli 2 ndani ya dakika 2 za nyongeza.

Kumbe bana katika maisha usikate tamaa. Tuambie wewe ipi ilikuwa mechi yako ya kwanza

#Bring back our Billionaire Mo Dewji

kumbe wewe ni kijana mdogo sana aisee !
 
West Germany Vs Argentina World cup,1990,Ruud voller,Jurgen klinsmann,Thomas hasler,Diego maradona,
Nlikuwa nachungulia Video kwa Ngarama pale Shinyanga,Mtaa wa Majengo,nlikuwa shule ya Msingi,alikhwa Peke yake Mwenyewe Video Mtaa Mzima,Mzee yule wa Kihaya! Baada ya Hapo ikaja 1994 Mataifa huru ya Africa, kalusha Bwalya,na Kombe LA Dunia Marekani,Rashid yekin,Robert baggio,1994!
Nadhani tulikuwa pamoja ila hatujuani, mwaka huko naliangalia WC pale bwalo la Polisi Shy mjini.
 
Ilikua Brazil vs Turkey wedikapu 2002, Turkey anakufa goli 2

Hii mechi ndo ilinifanya niupende mpira wa miguu

-upande wa vilabu nilivutiwa sana na Didier Drogba na mourinho, huu ukawa mwanzo wa kuipenda Chelsea.
 
Simba na Yanga uwanja wa Amani
Yanga 2 Simba 0
Mwaka 1975
Fainali kombe la klabu bingwa Africa Mashariki na Kati
Wafungaji .. Marehemu Gibson Sembuli na Sunday Manara
 
Write your reply...ilikuwa mchana mmoja wa 2009 pale nilipo lipa shilingi 300 kuiona timu yangu pendwa ya Man utd kwa mara ya kwanza tulicheza dhidi ya Liverpool, daah sitomsahau Torres a.k.a 'El nino' sema mwisho wa siku nimebaki nakumbukumbu hiyo.
 
Wapi fabrizo ravaneli enzi zake
Usinikumbishe ile squad ya Ajax, ikiongozwa na Patrick Kluivert, kushoto kuna finidi George, kulia kuna winger teleza Tijani Babangida katikati centre forward yupo Nwankwo Kanu. Mid fielders Edger David's akina de boer hii timu ilikuwa balaa. Tisa kumi yote timu yangu JUVENTUS TORINO bibi kizee kulikuwepo na akina gianluca Viali, fabrizzio Ravanelli, Zinedine Zidane, Lilian thuram, Atillio Lombardo sisi waitaliano tukibeba kombe siku hiyo. Huyu Viali akahamia Chelsea baada ya kuchomeka kombe na ikawa mwanzo wa mie kuipenda CHELSEA
 
World cup 1994 ila nilikua sijui kitu. Mwaka 1998 ndo nilianza kufatilia rasmi na Michael Owen ndo alikua kivutio kikubwa na ndo mwanzo wa kuishabikia Liverpool mpaka leo
 
Back
Top Bottom