Mara yako ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Mara yako ya kwanza kutongoza/kutongozwa ilikuwaje?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
Kila mtu ana Zamani yake.

Zamani yenye kufarahisha na Kuleta kumbukumbu ya kujicheka mwenyewe samytimez.

Miaka yetu tunabalehe, vijisimu vya goroka ndiyo vilikuwa vinachangamka, wale watoto wahuni tulikuwa tunavitumia kwa siri huku, wazazi wakipinga swala la mwanafunzi kumiliki simu.

Mtu wangu wa kwanza kumtongoza wakati naanza kupata ashki za kimwili...bahati mbaya hakuwa na simu.🤣🤣🤣 tupo kidato cha kwanza. Nakumbuka msichana huyo wa kwanza kumtongoza nilimuandikia barua, akanijibu YES, Shida ikaja kila nikimuona yule shuleni au mtaani, lazima nibadili njia. Yeye ndiyo akawa ananitafuta mimi.

Huyu mimi wa sasa mjanja mjanja najicheka nikikumbuka zamani yangu. #Enzi za ufala. Hebu share story yako hapa ilikuwaje mara yako ya kwanza?

1643195933176.png
 
Nilikua namfukuziaga kimoyo moyo mtoto mmoja hivi alikua kanizidi kidato, ye form 2 mi form 1

Alikua machine ya hatari kwa sasa wanaita pisi

Dada alikua mzuri balaaa halafu hakuwa na dharau yaani MTU wa watu, wengi walimchukulia kama anaringa kwa sababu ya uzuri wake, wengi walikua wanaogopa hata kupiga nae story,

Kwahyo mi nikawa namsubiria barabarani akipita kutoka tuition namsindikiza kwao huku tukipiga story za hapa na pale,

Washikaji wakawa wananiuliza vipi ushatupa ndoano?

Nikawajibu nishakula tunda kitambooo,

Walinisifia sana kwani demu alikua Chuma kweli kweli yaani mpaka Leo yule Dada hua hachuji,

Aisee ilipita mda mrefu sana nikifanya hii tabia ya kumsindikiza na kuwadanganya washikaji zangu kua namla yule mtoto,

Roho ilikuja kuniuma baada ya kusikia yule demu kaliwa na boya mmoja hivi ambae nilikua na bifu nae pale mtaani,

Nilikua na bifu nae kuanzia Kwenye micjezo yetu mpaka wazazi wetu pia kifupi bifu La kurithi,

Nikaona nijitutumue namimi nifanye kweli sasa,

Nakumbuka nilikuatana nae kama kawaida nikaanza kumsindikiza, nikaanza kujiuma uma na voko za kishamba akawa hanielewi akaniuliza kuna tatizo gani?

Nikamuuliza et Anna unanipenda, akajibu ndio, basi niliachana nae nikiwa na furaha kinyama,

Kesho yake nilipoonana nae nikawa namkomalia sasa anipe jibu langu,

Akiuliza lipi nikawa namwambia we jana. So tushakubaliana jamani tuwe wapenzi,

Alishamgaa sana et Haaaaaaaaah!

Aisee nilijiskia aibu sana maana tulikua tunaheshimiana,

Nikawa namkwepa sitaki hata kuonana nae daah bahati nzuri alihama shule ndio nikawa afadhari kwangu, loooh ile aibu sintokuja kuisahau
 
Nakumbuka kipindi nipo njuka kuna mdada mmoja mmachame alikuwa kidato cha 3 nilikuwa namkubali sana kiasi kwamba kila siku lazima nijitahidi nimuone tu hata kwa mbali. ( I was her secret admirer).

Halafu mrembo kinyama yani hata uwezo wa kumfata nimwambie sina kwanza sijawahi tongoza manzi enzi hizo na hata ningemfata nahisi angecheka tu kuwa utoto unanisumbua.

Uzuri kwenye darasa lao nilikuwa na ma bro tuliotokea mtaa mmoja kwahiyo nikawa naenda huko kila muda wa prepo kujidai kuomba kusaidiwa maswali kumbe lengo langu nimuone yule dada.

Yani mpaka leo hii sura yake na jina lake sijawahi sahau japo yeye sijui kama hata anajua kuna mtu anaitwa Chalii ana exist.

Nimtaje jina kama yupo humu ajue?
 
Umenikumbusha Shule ya msingi tulikua na dada mkuu pini ya maana kila mtu anashoboka mixer wakufunzi pia, sasa kidume ndo attempt yangu ya kwanza kutongoza na sijui niingie vp.

Nikamfata msela wangu kitaa yy aliacha skuli ili anipe maujanja, akaniambia ww mkonyeze tu ataelewa mchezo...Siku nimechelewa skuli kama ilivyo ada (Mchelewaji Maarufu) tukawa tumepigishwa magoti na madam mmoja mnoko kwl (RIP now) muda huo dada mkuu yupo pale, nikasema ndo chance hii kufanya mautundu yangu.

Nikamvizia kaniangalia tu nikamkonyeza, La haulaaa !!! muda nakonyeza na madam ndo anageuka, sijui alijua nimemkonyeza yy..aliamuru mateka wote waende huru akabaki na mm..Washua nilizikoga siku ile mpk nikasema ulaaniwe mdau kitaa huko ulipo, Baadae nimechill mida ya vipindi vya ziada nikapokea karatasi imeandikwa POLE.

Nikacheki imetoka wapi, kwa mchumba Dada mkuu...nikamwambia umeniponza, ila kuna kitu nilitaka nikwambie ila kwa bakora za leo naona Jau naweza kupata Double yake...akajibu siwezi kwenda kusema, Nikaandika I Love U...akajibu I love you too.

Kidume shangwe za kutosha, mtoto akasema alielewa kitambo, mambo ya perfomance yalinibeba sana, Likawa Goma langu mpk Secondary kwa utoto ule tunda liliwa tulivyoingia Secondary...ila Mwalimu mkuu aliniamshia pila alivyokuja kujua maana na yy goma alikua analitaka nusu anitimue shule mpk nikaleta mzazi.

Zama za Ujinga huwa najicheka sana.
 
Nilitongozwa kwa barua nikiwa kidato Cha tatu...
Na mwanadada mmoja hivi Mwenye jina la Jimbo moja huko USA maarufu kwa fukwe zake matata na mengine mengi...
Wiki nzima nilikuwa naitizama naisoma ile barua .. na ilinichukua wiki kuijibu..
Alikuwa Ni mwanamke wangu wa kwanza kumkiss aseh aseh aseh 😂
First love huwa Ni nyokoooo
 
Mimi nilimwambia " sitaki kukudanganya sijui nakuona kwenye glass au silali ila kwa kifupi tu L nakupenda sana kutoka moyoni".Na Kweli nilikua nampenda yaani nikimuona tu nahisi raha ajabu ,nikimuona hata na ndugu zake wakiume roho inauma na wivu Kama nyegere.Hiyo nipo kidato cha tatu yeye cha pili.Kumuomba mbususu nilikua naona Kama ntamkosea heshima.Rafiki yake mmoja alishawahi kukaleta homu niko mwenyewe akakaacha chumbani kwangu sikukafanya chochote ,hata kukumbatia tu.Kwa kifupi zilishatokea chances nyingi sana za kukala tunda kimasihara nikashindwa mwenyewe.Kalienda Sweden katoto kangu kazuri ka Kinyambo.Hakika penzi la L lilinitoa jasho
N:B Hatukuwahi kufanya matusi .
 
MTU wa kwanza kuanza kumtongoza alikuwa mume wa MTU,nilitafuta namba ya simu kwa watu wake wa karibu...nikaanza chat nae alivyonitambua akajisogeza zaidi...haikuwa shida sana I just confessed to him.Yaan ilikuwa kama alikuwa anasubiri nitamke sikuzote...nakumbuka alinijibu tu haraka tuonane....aisee mbona baadae nikajikanda na maji ya moto yenye chumvi.Sikumtafuta tena,ila nilimpenda kiukweli uchu wake ulimponza
 
Nilikua namfukuziaga kimoyo moyo mtoto mmoja hivi alikua kanizidi kidato, ye form 2 mi form 1

Alikua machine ya hatari kwa sasa wanaita pisi

Dada alikua mzuri balaaa halafu hakuwa na dharau yaani MTU wa watu, wengi walimchukulia kama anaringa kwa sababu ya uzuri wake, wengi walikua wanaogopa hata kupiga nae story,

Kwahyo mi nikawa namsubiria barabarani akipita kutoka tuition namsindikiza kwao huku tukipiga story za hapa na pale,

Washikaji wakawa wananiuliza vipi ushatupa ndoano?

Nikawajibu nishakula tunda kitambooo,

Walinisifia sana kwani demu alikua Chuma kweli kweli yaani mpaka Leo yule Dada hua hachuji,

Aisee ilipita mda mrefu sana nikifanya hii tabia ya kumsindikiza na kuwadanganya washikaji zangu kua namla yule mtoto,

Roho ilikuja kuniuma baada ya kusikia yule demu kaliwa na boya mmoja hivi ambae nilikua na bifu nae pale mtaani,

Nilikua na bifu nae kuanzia Kwenye micjezo yetu mpaka wazazi wetu pia kifupi bifu La kurithi,

Nikaona nijitutumue namimi nifanye kweli sasa,

Nakumbuka nilikuatana nae kama kawaida nikaanza kumsindikiza, nikaanza kujiuma uma na voko za kishamba akawa hanielewi akaniuliza kuna tatizo gani?

Nikamuuliza et Anna unanipenda, akajibu ndio, basi niliachana nae nikiwa na furaha kinyama,

Kesho yake nilipoonana nae nikawa namkomalia sasa anipe jibu langu,

Akiuliza lipi nikawa namwambia we jana. So tushakubaliana jamani tuwe wapenzi,

Alishamgaa sana et Haaaaaaaaah!

Aisee nilijiskia aibu sana maana tulikua tunaheshimiana,

Nikawa namkwepa sitaki hata kuonana nae daah bahati nzuri alihama shule ndio nikawa afadhari kwangu, loooh ile aibu sintokuja kuisahau
Saizi vipi, mnawasiliana? Anasemaje?
 
Back
Top Bottom