Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hoja yako hapo juu unamaanisha huyo mzee Mohamed Said alizaliwa Gerezani na kukulia hapo tokea kichanga hadi kikongwe miongoni mwa Waislamu tu bila kukanyaga hata Upanga kwa Wahindi - sembuse majigambo yake ya kusafiri mabara karibia yote duniani ? Mzee ambaye anadai kasoma shule ya wamisionari Saint Joseph's School? Halafu unaandikaje taazia ya mtu ambaye anakiri mwenyewe hawakufahamiana kihivyo sababu tu ni Muislamu wa Gerezani? Mfano mdogo, walimu wake enzi hizo Masista wa Kizungu wa St Joseph's School, nadhani wengi kama siyo wote, watakuwa washafariki zamani lakini sijawahi kuona akiwakumbuka kwa mchango wao katika elimu yake.
Historia ya Wazee ndiyo ipi hiyo? Unaanzia wapi kwanza? Familia? Mtaa? Ukoo? Kabila? Dini? Nani ni "mzee", na nani siyo "mzee" wa Historia?Wewe kwanini huandiki Historia za Wazee wako ambao Mohamed Said hawaandiki?
Sent using Jamii Forums mobile app
Historia ya Wazee ndiyo ipi hiyo? Unaanzia wapi kwanza? Familia? Mtaa? Ukoo? Kabila? Dini? Nani ni "mzee", na nani siyo "mzee" wa Historia?
Mkapa kamchana Iddi Simba kuhusu uzawa, kwenye kitabu chake Mkapa.Allah ampe kauli thaabet Mwamba katika Miamba ya Jiji la Dar es salaam
Huyu Gwiji Barua yake ya Kujiuzulu Mkapa alimkubalia kwa Masharti kuwa kujiuzulu kwake kuanze baada ya kwenda kuwakilisha Nchi kwny Mkutano wa Mabeberu huko Ng'ambo
Mzee Mkapa sio mzuri wa kuhudhuria Misiba n ukiomuona kahudhuri jua kaguswa na akagusika
Zengwe la kashfa ya Sukari alisukiwa na Genge la Wasaka Urais ambao hawakuupata
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuuliza "Historia ya Wazee" ndiyo nini lakini?Kwa hiyo huandiki historia ya Wazee wako kwa kuwa hujui mambo kadhaa uliyouliza?
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkapa kamchana Iddi Simba kuhusu uzawa, kwenye kitabu chake Mkapa.
RIP Iddi Simba.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuuliza "Historia ya Wazee" ndiyo nini lakini?
Utaandikaje taazia ya Marehemu ambaye ulikuwa hauko karibu naye sababu tu ni Muislamu wa Gerezani?Kama hujui maana yake upo kimakosa kwny Thread hii
Na sio kuwa hujui bali unakwepa swali nililokuuliza, nguvu unayotumia kumshambulia Mzee Mohamed Said kwanini usitumie kuandika Historia ya hao ambao anakwepa kuwaandika
Anza kwa kutuletea Taazia ya Nsa Kaisi maana Mohamed Said hajamuandika
Sent using Jamii Forums mobile app
Nafikiri amejibu vyema kuwa huwa ananena maisha yake na si vinginevyo.3 Angels,
Haya usomayo kutoka kwangu ndiyo mazingira niliyokulia katika Dar es Salaam ya 1950s kuelekea 1960s.
Dunia yangu yote ilikuwa Mtaa wa Kipata, Livingstone, Kiungani kwa bibi, shangazi na wajomba.
Hizi ndizo kumbukumbu zangu nyingi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi wazee wa upande wa pili wa kikristo huwa huna story zao??
Utaandikaje taazia ya Marehemu ambaye ulikuwa hauko karibu naye sababu tu ni Muislamu wa Gerezani?
Hoja yangu ni kwamba huna hoja. Kalaghabaho!
Sikuandika kwamba Mkapa anamkubali Iddi Simba katika kila kitu.Ikisemwa Fulani ni Rafiki Mkubwa wa Fulani au anamkubali fulani haimaanishi anamkubali kwa kila kitu
Mkapa alimkataza hadharan JPM kutumia Serikal ya JPM sijui ya tano alimtaka atumie maneno serikali ya ccm lakin hajatii lakin bado Che Nkapa anamkubali JPM
Sent using Jamii Forums mobile app
In the book My Life, My Purpose.....View attachment 1382192
Hivi wazee wa upande wa pili wa Kikristo huwa huna story zao?
aaah kumbe hata lile hall la sekondari ya wazazi ya Meta pale jijini Mbeya linaitwa Idd Simba kumbe ndio mwenyejina hilo!!MARA YANGU YA KWANZA KUMTIA MACHONI IDDI SIMBA 1980s
Ilikuwa miaka ya 1980 tuko nyumbani kwa marehemu Bi. Mruguru bint Mussa, mama yake Ally Sykes Mtaa wa Lindi.
Pametokea msiba Bi. Mariamu, shangazi yake Bwana Ally Sykes amefariki.
Watu wamejazana mtaa umefungwa wanasubiri muda wa mazishi.
Bwana Ally mwenyewe kakaa jamvini kazungukwa na jamaa zake wa Gerezani, wamekukuja kuungananae katika msiba wa shangazi yake.
Watu ni wengi sana.
Bwana Ally yeye mwenyewe ni mzishi sasa leo limemfika ndugu zake wamemwitika kwa wingi sana, wamekuja kumzika.
Bwana Ally kuniona ananita nende nikakae nae mbele.
Basi nanyanyuka pale nyuma nilipokuwa kwa unyonge maana umma mzima unaniangalia watu wanajiuliza huyu anaeitwa mbele pale ana umuhimu gani?
Katika lile jamvi alokuwa Bwana Ally ni “nani aliye nani katika mji wa Dar es Salaam,” Waingereza wanasema “Who is Who,” wenyewe watoto wa Gerezani na Dar es Salaam wametanda.
Iddi Simba alikuwa amekaa jirani ya Ally Sykes.
Amevaa nguo zilizomkaa vyema kapendenza na miwani yake.
Sasa Bwana Ally anawanadia watu, “Nyie mnamjua huyu? Mtoto wa Said pale Kipata mwandishi hodari sana…”
Utambulisho umekwisha nakaa pembeni Ally Sykes na Zuberi Mtemvu wanashambuliana kwa maneno.
Bwana Ally kalalamika kuhusu hali ya nchi mambo hayendi vyema.
Zuberi Mtemvu kadakia anawashahidisha watu, “Jamani mnasikia Ally analalamika ati mambo hayendi sawa…”
Mtemvu anaangua kicheko cha kejeli huku akitingisha kichwa.
Watu sasa weshakuwa hadhir wanasubiri Mtemvu atasema kitu gani?
“Huyu Ally na marehemu kaka yake Abdul (Mungu amrehemu) walikuwa wanashirikiana na Nyerere kukipiga vita chama changu kife, leo Ally huyu huyu keshageuka ati nchi imeharibika…”
Wasikizaji wanacheka wengine wanamuunga mkono Bwana Ally wengine Zuberi Mtemvu.
Bwana Ally hakubali kushindwa anarudisha kombora, “Ala kumbe Congress bado mko hadi leo nilidhania tulishakumalizeni.”
Vicheko.
Mzee mmoja kwa mbali anaita, “Ally sikiza bwana, Congress tupo sana. Congress ni mwamba usiovunjika.”
Vicheko vinaendelea.
Hii “Congress ni mwamba usiovunjika,” ni maneno yaliyokuwa katika nyimbo ya Congress wakati wa harakati za kudai uhuru.
Watu wametulia Bwana Ally akafahamu kuwa Mtemvu alikuwa hamjui Iddi Simba na pale akawatambulisha.
Nilishangaa sana vipi miamba hii yote ya Gerezani isifahamiane.
Hapo nami ndipo nikamfahamu Iddi Simba ingawa jina lake lilikuwa maarufu katika vyombo vya habari kila inapotajwa East African Development Bank iliyokuwa na makao makuu yake Kampala Uganda.
Kuanzia hapo Mzee Iddi Simba kila tutakapokutana atakuwa na la kunieleza.
Mzee Iddi Simba alikuwa na kawaida kila akimaliza kusali Dhuhr Msikiti wa Manyema hatoki atakenda kukaa nyuma ya msikiti na jamaa zake watamfuata pale.
Nami hii ndiyo ilikuwa fursa yangu ya kusalimiananae kila nikiswali Msikiti wa Manyema na hapo utamkuta kakaa na rafiki yake kipenzi Muharam Kocha.
Napenda kuhitimisha kwa kueleza kisa kimoja.
Anur Suleiman alipata kuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza katika miaka ya 1970/80.
Huyu bwana alikuwa anajenga msikiti sikumbuki kama ni kwao Bukoba au Mwanza.
Akaleta vitabu vya risiti kwa ajili ya kuchangisha nami nikapewa kimoja nichangishe hapa Dar es Salaam.
Basi siku hiyo nikamkuta Mzee Iddi Simba kakaa kwa Daddy huyu alikuwa fundi cherehani maarufu Kariakoo karibu na Saigon ya zamani, Mtaa wa Sikukuu.
Katika maisha yangu hadi hii leo sijawahi kuchangisha kitu chochote nikapata fedha nyingi kama nilizopata katika mchango huu kiasi hata yule aliyenipa kitabu kile alipigwa na butwaa.
Nikamfuata Mzee Iddi Simba kakaa pale kwenye benchi na vijana wa Saigon mtu akikwambia ukubwa wa mtu huyu na hadhi yake utakataa utajiuliza pale anafanya nini?
Mzee Iddi Simba akanisikiliza kisha akabaki kimya hakunambia chochote nami nikaondoka.
Nilidhani hakutaka kunipa mchango.
Baadae kidogo akanifanyia ishara nimfuate.
Fedha alizonipa kama mchango wake wa msikiti zilinishtua na naamini wale waliokuwa wakitaka kuchanga wanataka kwanza waangalie nani na nani washachanga bila shaka mchango ule uliwatia motisha angalau na wao watoe kingi wamkaribie Iddi Simba.
Allah amfanyie wepesi mzee wetu safari yake na amsamehe.
Amin.
View attachment 1356331
PICHA: Mzee Iddi Simba na Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu katika futari ya Saigon mwaka wa 2010
..mliokisoma kitabu cha Mzee Mkapa mmekipenda?
..kuna kitu chochote kipya au is Mzee Mkapa setting any record straight ktk kitabu chake?
Muhimu kukisoma kwa sababu jamii yetu hii, mambo mengi hayana maandishi.
Ameonyesha njia. Wengine wakijiunga naye kuandika, basi tunaweza kuwa na jamii ya uwajibikaji I guess.
..I dont feel like he is offering anything that is not known, or he is setting any record straight.
..sina uhakika kama kitakuwa kizuri kama kitabu cha Mzee Mtei au Conrad Mselle ambao ni watata kidogo na walikuwa na "makaburi ya kufukua."
Cc Kiranga