Marafiki 'pingapinga' hawaungi juhudi wala hoja yoyote ya maendeleo

Marafiki 'pingapinga' hawaungi juhudi wala hoja yoyote ya maendeleo

Kichwamoto

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2019
Posts
3,403
Reaction score
4,692
Wasalaam kwenu nyote!

Hii dunia ni hatari, kuna marafiki vibwengo hatari jambo lolote la kimaendeleo ukimwambia anapinga na atakosoa vikali na atakwambia mimi nimefanya sana hio, mfano wazo lolote la kilimo cha mazao anapinga, uchuuzi wa mazao anapinga, ufugaji anapinga, biashara anapinga na kukatisha tamaa, cha ajabu kila alichopinga anachukua wazo anafanya yeye kimya kimya.

Kuna watu ni nyoko dadadadeki aina hii si mchawi sasa kwanini aendelee kuwa rafiki yako.

Mungu si athumani hata "Shanta Shanta" pia ana Mungu pamoja na kupingwa kukatishwa tamaa unafanya wazo lako na unavuna matunda, unamsimulia kuhusu matunda anawaka mkuu vipi mbona hukusema.

Ntakwambiaje tena nilijilipua mwamba, kiunyonge unamwambia ila na wewe si umefanya kimyakimya, anaruka kama mvumo wa buzza.

Nina hasira halafu sio fundi wa simulizi.

Nadhani ujumbe umeeleweka, wenye visa vya namna hii karibu kwa visa vyenu.

Nawahi kutembelea shamba la iliki sehemu.

Tupambane jaribu jaribu usiogope usiogope Mungu ni wetu sote nena nena tena kwa sauti hata neno moja ni ushindi.

Jangala kuzuri

Tusome kitabu cha Mwanzo 3:15
 
Kujieleza sana ni dalili ya unyonge, onesha vitendo tu.
Ni ile hali unampenda rafiki na unataka wewe upate na yeye apate lakini kumbe yeye anapenda apate yeyetu, akiwa juu wewe uwe chini ndio raha yake, unakuwa na rafiki anashindana na wewe bila wewe kujua, inaogopesha sana!!
 
Back
Top Bottom