Marafiki wa kiume hatuambiani tunapendana kama wanawake lakini maisha yetu tunayoishi ndio kielezo tosha

Marafiki wa kiume hatuambiani tunapendana kama wanawake lakini maisha yetu tunayoishi ndio kielezo tosha

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Ni nadra sana kukuta mwanaume anamwambia mwenzako kwamba anamjali.

Ukiwa na shida utapewa msaada kwa utani au kadhihaka fulani hivi, Kwa nje ni kama huwa hatutaki kusaidiana ama kujaliana lakini kwenye mioyo yetu kwa ndani huwa tunamaanisha.

kwenye kuomba tu msaada Kuna kaujeri kidogo, utasikia "we fala nitoe 10 hapo" nae anaetoa msaada atajibu "achia ulofa wewe pimbi, haya nitumie namba hio"

Kwa wale ambao wamefika 40 hivi ujana umeanza kuwakimbia kidogo huwa na busara katika maneno 😂😂 "Mzee mwenzangu nazalilika, embu fanya nipate laki mbili jioni nitakueleza yaliyonikuta tukiwa kijiweni" majibu: " Punguza dogodogo na mapresha hayo hutoboi 70, mtume kijana aje".
 
Wa matusi ni vijana 25 and below.

Tabia ya kubebana inaenda mpaka kwenye utu uzima wetu, na mara nyingi tunabebana bila hata mke kujua sababu ukimwambia atakuona unajali marafiki na unatapanya pesa kumbe sivyo, utasikia "Mzee mwenzangu nazalilika, embu fanya nipate laki mbili jioni nitakueleza yaliyonikuta tukiwa kijiweni".

Majibu: " Punguza dogodogo na mapresha hayo hutoboi 70, mtume kijana aje".

Ukikaa ukatafakari ni ajabu sana bond ambayo wanaume tunaweza kuwa nayo.
 
Binafsi sijawahi kuwa na urafiki wa kuitana pimbi,fala,bwege n.k,lazima heshima iwepo,tumia neno braza,dogo n.k ,kinyume na hapo sikuelewi
 
Hua kuna vipindi nachacha kbsa. Napauka nje ndani sina hata mia. Af n ka weekend uko area unashangaa mama chanja anakuja na claim.kibao, mara gas imeisha, sijui sukari imekata .nk
Hapo hua naaga tu kua subiri noende town nkatafte.
Nkitoka nje namchek mshkaji wangu chao anasawazisha kianzio, nkirud sio mikono mitupu.
Hua laaziz anauliza, hua unatoa wap? Naishia kumwambia tuna chama cha wanaume kinatupa dividend kila mara
 
Sasa hao kina mama, utasikia udugu wangu, kipenzi changu na kila neno zuri zuri lakini ajabu ni mahasimu wakubwa na wakipeana mgongo wanazomeana.
 
Naruhusiwa kuchangia au Ni Uzi wa wanaume tu?
 
Back
Top Bottom