Marafiki wanaoishi DAR... Sio kabisa

sasa kwa nin uwa wanatuzingua saaanaaa ssisi watu wa mkoa... Oooohh naishi dar..!! ukija wanakukimbia.. Thats Mental SLAVERY

Unalolisema ni la ukweli, wengine wanafikiria una Njaa, hata ukiwapigia simu utasikia niko busy, busy gani hiyo? Hata saa moja tu nalo litakukosesha mapato? Pengine wanaogopa labda hali walizonazo sio ndio maana hawataki mkutane. Acheni hizo.
 
Pole sana....kama walikupotezea hivyo....mbona jopo kubwa la JF lipo Dar....ungetumia fursa hiyo kuwatafuta.....Jf kuna watu wa ukweee....si kipolepole......
Ushauri mzuri sana huu, nadhani atauzingatia akija next time........

wameniboa saanaaa........ tatizo naondoka kesho.. siwezi wacheki watu wa JF.... may be next tym
Eishhh, sasa wakuboe wengine uje ulalamike JF? Si ungewatumia msg ya kuwalalamikia hao maswahiba zako?

Watu tunamitikasi yetu tuhangaike na Data wanini?? Usitupotezee wakati wewe watujua???

HA ha haa ha ha mweeeeeeeeeeee kalale na kesho uende zako
Khaa!

avatar yako iko tofauti na fikra zako...Sikumaanisha maarafiki wa JF... nilimaanisha marafiki wangu wa ukweli... nawajua,wananijua,, KAFUE NGUO!!!!!!!!!!!!!!!!
Ebo! Kweli umeumizwa, pole.
Ukija tena ubishe hodi kwa wanaJF, wageni huwa hawatuchoki.
bakini na mji wenu wa giza,mijasho,uchafu... Gizaa, to hell
Ishh! Kumbe ndo maana wanakukimbia.........! Au ndo yamekuwa kama anavyosema manajamii hapa chini?
Sizitaki mbichi hizi, Sungura akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua.

Karibuni Daslam. Ukizaliwa Daslam tayari unakuwa fomu siksi.
Mtusamehe bure, foleni zinatukwaza.
Sibirini barabara za hewani, tumeahidiwa kabla mkulu hajastaafu zitakuwa zimeshakamilika.
 
pole bwana, wanaotetea upumbavu huo nao ni walewale ulishasema ni jamaa zako wa karibu sana so ulitegemea sapoti hata kwa saa1 tu, sasa wengine mara oooh muda, toa tarifa ukija yanatoka wapi endelea na kilimo chako best hao hawana maana kazi yao kuichagua ccm tu
 
wameona so kwa sababu wanajua umeshawapiga gepu lakutosha tu kimaisha, wenyewe wanang'amg'ania daresalama mjini lakini ndo hivyo unakuta maendeleo yao ni kiduchu sana
 
wameona so kwa sababu wanajua umeshawapiga gepu lakutosha tu kimaisha, wenyewe wanang'amg'ania daresalama mjini lakini ndo hivyo unakuta maendeleo yao ni kiduchu sana
Endelea kujidanganya na kujipa moyo, maisha lazima yasonge mbele.
 
ndo zao kama ni wkdays wanasingizia ubusy oficn na foleni,ikiwa wkend utasikia ooh nina kikao cha arusi
 
We nawe una mbwembwe chuo mwaka mzima mnaonana hujatosheka? wengine wanaogopa kuwaleta kwao kwasababu si wpte wanamaisha mazuri.....................wanaogopa
 
Ndugu dar maisha magumu, foleni kibao, hussling ndo usiseme unakuta hata siku haikutoshi kuonana inaweza kuwa ngumu. Pia nyumba zetu za kupanga hizi chumba kimoja au ukijitahidi na kasebule, choo cha uani hakina hata paa, aibu kaka. Utamkaribishaje mshkaji wako ambaye kwenye facebook umemfanya aamini mambo yako super na kumbe reality ni tofauti. Hali inatisha mkuu..usiogope.
 

Kuna babu yangu mmoja anaishi Shinyanga. Aliwahi kunisumbua sana kwenye simu akinitaka niende Kariakoo kumnunulia spea za pikipiki kisha nimtumie kwenye basi. Huo muda sikuwahi kuupata, mpaka akaja mwanae kutosha huko, akanunua na akaondoka. Kwa kifupi, mjini maisha ni mchakamchaka. Foleni ndio usiseme. Halafu tatizo mtu akija toka mkoani, yeye anakuwa free wakati wewe uko bize, na wakati huo huo atakwambia kwamba anaondoka kesho....Sasa kuonana kwa ghafla ghafla namna hiyo kimjini mjini inakuwa ngumu!
 
....hivi, mnaosema muda hautoshi...mbona vikao kama hivi

...hamkosekani?...au "muda" wa ndugu jamaa na "marafiki" tu ndio hamna?
 
Watu wengi wanawatafuta "marafiki" zao wakati wakiwa na "pesa za kutumia" au kuwaonyesha "vitz" mitumba waliyonunua...
 
Reactions: Mbu
....hivi, mnaosema muda hautoshi...mbona vikao kama hivi

...hamkosekani?...au "muda" wa ndugu jamaa na "marafiki" tu ndio hamna?

He! hapa wapi tena!
Halafu mbona inaonekana ni mchana mchana!
 
Ubize ubize ubize gani huo tumekaa dar tukatoka lakini inapofika mida yakuonana na rafiki zako kutana nao kwanini umkwepe ikiwezekana mtafutane mida ya jioni.karibu na mazingira unayo fanyia kazi wengine roho mbaya,mzani tulioko mikoani tumepigika kivile maisha ni personal struggle and creativity of an individual kuwa dar,ar,mz.ni added value tu, kinachobaki ni wewe mwenyewe.karibuni rock city tuko full shangwe.
 
Watu wengi wanawatafuta "marafiki" zao wakati wakiwa na "pesa za kutumia" au kuwaonyesha "vitz" mitumba waliyonunua...

...sasa huo ndio "urafiki" wa mashaka alioimba jidee...!


He! hapa wapi tena!
Halafu mbona inaonekana ni mchana mchana!

...aaah, sisemi mimi...ngoja masaki atuambie...nisijesema hapa
nikaonekana nawalaumu "marafiki" wa Dar na ngalawa yao hapo.
btw; hii complex si ishauzwa hii kwa mmiliki wa botswana, au?
 
Huyu jamaa anaonyesha ni mtu wa lawama sana ndo mana washkaji wanakukimbia, cheki unavolalamika duh, pengine hata ungeonana nao ungewalaumu wamekutana na wewe mara mbili tu badala ya mara tano ha haa haaa.
 
Umesahau ule msemo eeh Mjini Akili, Nguvu shamba" sasa wewe wenzio wanaishi kwa akili mjini hapa unakuja na miguvu yako yako ulale kwa nani na majasho yako ya mkoani huko??? nenda zako kulee, ndio maana sikuja kukupokea Ubungo......(just kidding)
 
e bana kama wamekutangulia kidogo hawataona umuhimu wa kuonana na wewe,marafiki wengi wa sasa wanaangalia watafaidika na nini kuonana na wewe,tatizo lako umeleta mambo ya huko hapa dar,mambo mengi ndo maana hata kusalimiana sio lazima mshikane mkono,ila kama wanafanya makusudi sio busara
jifunze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…