Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia,
alitoka siku moja, porini kutembelea,
akayaona matunda, mtini yameenea,
mtini yameenea, sungura nakuambia............
........................................
..................................
Sungura karuka ruka, mtini akarukia,
mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
kwenye mti akatoka, pembeni akasogea,
pembeni akasogea, sungura nakuambia!
Dah!! e bana nimesahau muendelezo wa hili shairi; wadau naomba mnikumbushe basi!! Au kwenye vitabu vya watoto wa siku hizi hamna hili shairi? manake nataka nifikie pale ambapo baada ya mzee sungura kuruka sana na kushindwa kuyapata matunda; mshikaji ikabidi aponde "sizitaki mbichi hizi!"