Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kuwa na rafiki haimaanishi ndio unamwambia kila kitu chako. Mimi pia niko hivyo, kuna vitu huwa vinabaki kuwa vya kwangu binafsi halafu kuna vile ambavyo nashirikisha watuSinaga yule wa kushibana sana,kwasababu napenda kuwa msiri sana,kwahiyo sipendi mtu anijue hadi taarifa zangu ambazo natakiwa kuulizwa mimi ndiyo nitoe,yeye awe nazo.Nakaa kimachalechale.Hata mtu niliyenaye kwenye mahusiano,sipendi anijue vizuri,kwasababu naamini atawahadithia watu wengine.Kuwa kivyangu nainjoi,since my childhood.
Huu wa kazini sio urafiki ule kushirikiana sana dereva wa pale ndo nashirikiana nae sana maana Kuna Chocho za 💸💸 hua napata tukifanya manuverMimi kazini ndio sijawahi kuwa na rafiki sijui ni nature ya kazi nilizofanya
MmojaHabari za wakati huu,
Rejea swali hilo hapo juu...katika maisha ya ukuaji, masomo, utafutaji huwa tunajikuta tunakutana na watu wengi... wengine wanabaki kuwa tu watu tunaofahamiana nao na wengine wanakuwa marafiki tena wengine huwa tunashibana kiasi cha kuwa kama ndugu.
Nakumbuka shule ya msingi nilikuwa na rafiki yangu mmoja anaitwa A ..ni hulka yangu kuwa na rafiki mmoja tu wakizidi sana wawili. Of course wanaweza kuwa wapo na wengine ila wa karibu huwa ni mmoja.
Huyu tumekua wote hadi chuo lakini baada ya hapo kila mtu alipoingia kwenye kutafuta maisha tukajikuta tunakuwa mbali, mawasiliano yakapungua kama sio kukatika kabisa.
Kila mtu ana namba ya mwenzie ila tuna miaka zaidi ya mitatu hatujawasiliana, hata tukipigiana simu hatuna stori.
Huo ni mfano mmoja tu ila wapo niliokutana baada ya hapo , tulikuwa karibu sana ila sasa hivi tumekuwa total strangers.
Nilichogundua ili watu muwe na muendelee kuwamarafiki lazima kuna vitu muwe mnafanana, mazingira yaliyowakutanisha yakibadilika tu kila kitu kinabadilika.
Mfano mlikutana mkiwa single mmoja akiwa na familia urafiki kwa vyovyote utakufa tu.
Mlikutana hohehahe mmoja akifanikiwa urafiki utakufa au unabadilika kutoka urafiki hadi uchawa...labda yule aliyefanikiwa awe na moyo wa kumuinua mwenzake.
Mkikutana hamna ajira mmoja akipata kazi anakutana na marafiki wapya.
Au nyie wakuu mnaonaje? Niwatakie jioni njema
Huwa naachana nao tukishamaliza tu..na siondokagi na namba ya mtu hata shule nlikua hivyohivyo 😃Yaani hujawawahi kuwa na rafiki!
Uzi bila picha.....[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Picha ya status au ya kuchungulia [emoji1787]