Marais wa Afrika waliofariki wakiwa bado Madarakani

Marais wa Afrika waliofariki wakiwa bado Madarakani

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Ni kumbukizi ya miaka miwili tangu Kifo cha aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, maarufu kama JPM au Chuma.

Aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, ambaye sasa ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alitangaza kifo cha Hayati Maguli Machi 17, 2021 kilichotokea saa 12 jioni katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam baada ya kupata shida kwenye Mfumo wa Umeme wa Moyo, tatizo ambalo alikuwa nalo kwa takriban miaka 10.

Mazishi yake yalifanyika Machi 26, 2021 nyumbani kwake Chato mkoani Geita.

Hayati Magufuli anakumbukwa kwa misimamo yake mikali kwenye usimamizi wa maagizo yake pamoja na uwezo wa kuchukua maamuzi magumu hasa kwenye masuala yaliyokuwa yakionekana kukosa ufumbuzi.

Kama Mwananchi unamkumbuka kwa lipi kiongozi huyu?

Hapa kuna orodha ya Marais waliofariki wakati bado wakiwa Madarakani.

1999 - Mfalme wa Morocco, Mfalme Hassan II alifarikiwa akiwa na miaka 70 kwa Homa ya Mapafu.

1999 - Rais wa Niger, Ibahim B. Mainassara alifariki kwa kuuawa.

2001 - Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Laurent Dessire Kabila aliuawa kwa kupigwa Risasi na Mlinzi wake akiwa miaka 61.

2002 - Rais wa Somaliland, Mohammed H.I. Egal alifariki bila sababu za kifo chake kutajwa akiwa na miaka 73.
2005 - Rais wa Togo, Gnassingbe Eyadema alifariki kwa Mshtuko wa Moyo akiwa na miaka 69.

2008 - Rais wa Zambia, Levis Mwanawasa alifariki kwa tatizo la Kiharusi akiwa na miaka 59.

2008 - Rais wa Guinea, Lansana Conte alifariki kwa matatizo ya Moyo na Kisukari akiwa na miaka 74.

2009 - Rais wa Gabon, Omar Bongo alifariki kwa Saratani ya Utumbo akiwa na miaka 72.

2009 - Rais wa Guinea Bissau, aliuawa kwa shambulio akiwa na miaka 69.

2021 - Rais wa Tanzania, John Joseph Magufuli alifariki kwa tatizo la Mfumo wa Umeme wa Moyo akiwa na miaka 61.
2010 - Rais wa Nigeria, Umaru M. Yar'Adua alifariki kwa matatizo ya Moyo akiwa na miaka 58.

2011 - Rais wa Libya, Moammar Gadhafi aliuawa baada ya kupinduliwa na Waasi akiwa na miaka 69.

2012 - Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika alifariki kwa Mshtuko wa Moyo akiwa na miaka 78.

2012 - Rais wa Ghana, John Ata Mills alifariki kwa tatizo la Saratani ya Koo na Kiharusi akiwa na miaka 68.

2012 - Rais wa Zambia, Meles Zenawi alifariki akiwa na miaka 57 bila sababu za kifo kutajwa.

2012 - Rais wa Zambia, Michael Satta alifariki akiwa na miaka 77 bila kutajwa sababu za kifo chake.

2020 - Rais wa Burundi, Perre Nkurunziza, alifariki kwa Mshtuko wa Moyo akiwa na miaka 64.
 
Yaliyotokea Zambia uenda yakajitokea TANZANIA 2025. Yaani raisi anafia madarakani, then Makamu anashika hadi uchaguzi KISHA upinzani unashinda uchaguzi mkuu dalili uonyesha.
 
Eti Meles Zenawi rais wa Zambia! Halafu kuna wengine hapo wemekufa kwa Covid 19 wakasingizia matatizo ya moyo.
 
Masahihisho kidogo japo historia sijasoma sana Zambia haijawahi kutawaliwa na rais Meles Zenawi. Period [emoji23][emoji119]
Meles Zenawi Asres alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa wa Ethiopia kipindi toka 1991 to 1995 na akawa waziri mkuu wa Ethiopia toka 1995hadi kifo chake mwaka 2012.
 
2012 - Rais wa Zambia, Meles Zenawi alifariki akiwa na miaka 57 bila sababu za kifo kutajwa.

2012 - Rais wa Zambia, Michael Satta alifariki akiwa na miaka 77 bila kutajwa sababu za kifo chake.

2020 - Rais wa Burundi, Perre Nkurunziza, alifariki kwa Mshtuko wa Moyo akiwa na miaka 64.
Meles ametisha aliongoza Ethiopia na Zambia kumbe!
 
2012 -Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi alifariki akiwa na miaka 57 bila sababu za kifo kutajwa.
 
2012 -Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi alifariki akiwa na miaka 57 bila sababu za kifo kutajwa.
Kwa Zambia ni Levy Patrick Mwanawasa aliyefariki tarehe 19 August 2008 akiwa madarakani umri miaka 59 chanzo cha kifo kilitajwa kuwa ni stroke
 
Africa ndio tuna vifo vya hovyo, inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom