Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Kanisani mara nyingi Padre anayeongoza ibada huweka msisitizo wa kuiombea dunia nzima. Hukataza ile aina ya maombi yenye kunihusu mimi na watu wa familia yangu pekee. Huwa anasema tupunguze zile 'yangu' kila tunapoongea na Mungu. Kazi yangu, mume wangu, mke wangu, watoto wangu, nyumba yangu, jirani yangu. Padre kwa lugha ya kinabii kabisa amekuwa akikataza sala binafsi zenye ubinafsi mwingi ndani yake.
Anasisitiza kuombea walio wengi na hayo maombi yangu yawe ni sehemu tu ya nia pana. Namuelewa Padre kadri anavyorudia mahubiri yake pale katika mimbari ya kanisa, ni ujumbe wa upendo unaojali walio wengi. Lakini katika kuzama kwenye tafakuri naona kabisa kuwa maneno yake yanazisuta nafsi za mamilioni ya wanaolitumia hili jukwaa kwa nia mbalimbali haswa zile za kupanua uwezo wa mawazo yetu.
Naamini nia inayomsukuma Mgombea Urais mpaka akachukua fomu na kuilipia shilingi milioni moja kisha akazunguka nchi nzima kutafuta wadhamini, ni kuleta mchango wake katika mabadiliko chanya ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Naamini hiyo ndio nia ya kwanza kabisa ya Mgombea Urais, ikiwa anakabidhiwa ilani na kulazimika kuitekeleza kurasa baada ya kurasa hilo huwa ni suala la pili lakini la mwanzo kabisa ni kutumia kila alichonacho kwa faida ya wengine.
Nchi yetu imeshaongozwa na Marais sita mpaka dakika hii na wote hawa lengo lao kuu ni moja tu, na kizuri kwao ni kwamba wote wanatoka CCM wanatekeleza sera zile zile. Tofauti inaweza kuwa kwenye maarifa na utendaji kazi binafsi lakini wote wanayo nia moja kutoka ndani kabisa ya mioyo yao, kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya mtanzania mmoja mmoja kadri inavyowezekana.
Inashangaza kusoma humu namna baadhi yetu tunavyotamani kutoana macho kwa ushabiki tu wa hawa marais, wote hawa ni watekelezaji wa ilani ya CCM, ndio wanayokabidhiwa kama rejea yao baada tu ya mchakato wa kuapishwa na Jaji Mkuu.
Anachoweza kufanya Rais wa Awamu ya Kwanza hukifanya na yule wa Awamu ya Pili huendeleza pale anapoishia. Anachoweza kuendeleza wa Awamu ya Pili hukiendeleza mpaka pale atakapoishia na muendelezo wake anamuachia wa Awamu ya Tatu. Uhalisia umekwenda hivyo mpaka imefika awamu ya sita. Hivi ndio Tanzania inavyojengwa na chama kimoja cha CCM.
Hii mikwaruzano ni siasa za upambe ule ule unaodumu miongoni mwetu ambazo kwa kweli zinatuchukulia muda na akili bila ya sababu ya msingi. Marais wote sita ni watekelezaji wa ilani ya CCM, wanaachiana vijiti na kuendeleza anapoishia mtangulizi. Hajawahi kuingia miongoni mwao akatoka CHADEMA na kuingiza sera tofauti na zile zilizotimizwa na Mwasisi wa Taifa Julius Nyerere.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.