Marais Wastaafu na Viongozi wa Dini ni wajibu wenu kuandaa maridhiano baina ya CCM na Upinzani

Marais Wastaafu na Viongozi wa Dini ni wajibu wenu kuandaa maridhiano baina ya CCM na Upinzani

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Wadau nimekuwa nasikia Rais Mstaafu Mkapa ni mpatanishi huko Rwanda kati ya watawala na watawaliwa(baina ya vyama vya siasa) au Rais Mstaafu Kikwete ni mpatanishi burundi kati ya watawala na watawaliwa(baina ya vyama vya siasa) vinapokuwa vinazozana au kutokubaliana katika masuala yahusuyo siasa ,chaguzi au katiba za nchi zao na kupelekea machafuko na vita.

Tanzania tayari kunakutoelewana baina ya CCM na vyama vya upinzani kuhusu suala la katiba mpya na kamata kamata ya wapinzani inayofanywa na jeshi la polisi ,pia zuio la mikutano ya hadhara na ya ndani kwa vyama vya upinzani wakati CCM inafanya mikutano hiyo bila Polisi kuwazuia,pia suala la jeshi la polisi kubambikizia kesi wapinzani nalo limekuwa ni tatizo kubwa.

Ni wakati sasa kwa Marais Wastaafu na viongozi wa dini kuingilia kati suala hili ili kuleta maridhiano ya pande zote zinazoasimiana kama marais wastaafu walivyofanya katika nchi za Rwanda na Burundi. Kukaa kimya kwa Marais wastaafu na viongozi wa dini sio sahihi kwani ni wananchi wanaoteseka.
 
Haramu ukiishiriki kuikemea haiwezi kuwa rahisi tena. Pumzika kwa amani JKN:

IMG_20210707_084839_278.jpg
 
Mapatano mara nyingi yanatokea pale kukapokua na makundi yenye nguvu sawa au karibia na sawa lkn Hilo la chama kimoja kina jeshi,polisi,usalama, serikali vs chama kingine ambacho hakina hivyo vyombo Ni ngumu kufanya maridhiano maana mmoja anajiona mbabe na akiona mwenzake Ni dhaifu.
 
Maridhiano ili iwe nini? Sioni kama upinzani kwa sasa wanao ushawishi wa kisiasa wa kulazimisha Serikali iliyopo madarakani kuusikiliza upinzani.

Mama aliyumba tuu mara baada ya kuingia madarakani kiasi Ana akiba kidogo ya mambo ya kuwafurahisha upinzani bila kuitikisa kamati kuu ya CCM.

Tusubiri mazuri yanakuja, japo yatachelewa.
 
Mama alikuwa na lengo la kufanya maridhiano na wapinzani, lkn Mbowe na genge lake walivuruga mpango mzima wa maridhiano baada ya kuanza kwa kumtumia yule mnywa gongo na mnuka mdomo aanze kum challenge raisi kwa maneno yake machafu, lkn kama hiyo haitoshi Mbowe na genge lake wakaanza kuzunguka mikoa mbali mbali kufanya mikusanyiko isiyokuwa na ulazima wowote kwa sasa.

Kama Mbowe angekuwa na nia ya dhati na anayoyapigania basi angesubiri akutane na raisi na kumueleza kuhusu ajenda yao ya katiba mpya na endapo raisi angekataa hiyo ajenda baada kukutana nae hapo sasa ndo angeweza kufanya alichokuwa anafanya.

Sasa jamaa ameshika makali eti anajaribu kuvutana na alieshika mpini wa panga matokeo yake ndio hayo yeye ndo anachanika mikono.
 
Viongozi gani wa dini , hawa hawa ambao walikua wanamuunga mkono mama wakati wa chanjo ile ya BURE? msitegemee lolote , maana hata yule shehe ubwabwa aliyesema Magufuli chaguo la Mungu sasa anafuata upepo wa mama na alijifanya kufagilia chanjo eti kesho yake alikuwa anaupiga mwingi sana kwenye ndoa baada ya chanjo. Kuna vituko sana nchi hii nawaambieni
 
Alikuja vizuri, akawafutia kesi , akawarudishia pesa, mikutano ya ndani ikaendelea na kuahidi kukutana nanyi na akaomba muda suala la Katiba. Ninyi mkasema hamumpi muda na hamumsikilizi tena mnaendelea na yenu, sasa hayo maridhiano gani mnayotaka maana mlikataa wenyewe
 
Viongozi wastaafu unaowasema ni hawa waliopewa nyumba na Magufuli na ambao watoto wao ni viongozi kwa kubebwa au unawasema wastaafu wepi ?
 
Alikuja vizuri, akawafutia kesi , akawarudishia pesa, mikutani ya ndani ikaendelea na kuahidi kukutana nanyi na akaomba muda suala la Katiba. Ninyi mkasema hamumpi muda tena na hamusikilizi teba mnaendelea na yenu, sasa hayo maridhiano gani mnayotaka maana mlikataa wenyewe
Kwahiyo mtu kama ana mitizamo yake na ana imani zake juu ya uhuru haki na masuala ya kujieleza ndio mumbambikie kesi ya ugaidi , polisi waliambiwa wafute kesi za kubambika zaidi ya 200 wakamjibu Mkuu wa nchi wanaomba wapewe miaka miwili kwasababu ni kitega uchumi chao sasa na Mkuu wa nchi mwenyewe anacheka tu.

Hakuna kitu hapa Rais ambaye anajielewa kesho yake tu angefukuza woote pumbaf , mama kimsingi amekosa direction na wanaomkosesha direction ni wasaidizi wake mwenyewe na wengi wanataka ao nekane hawezi ili wapate wao huo ndio ukweli mchungu.
 
Alikuja vizuri, akawafutia kesi , akawarudishia pesa, mikutani ya ndani ikaendelea na kuahidi kukutana nanyi na akaomba muda suala la Katiba. Ninyi mkasema hamumpi muda tena na hamusikilizi teba mnaendelea na yenu, sasa hayo maridhiano gani mnayotaka maana mlikataa wenyewe
Karudisha Yeye au Mahakama?
 
Kwahiyo mtu kama ana mitizamo yake na ana imani zake juu ya uhuru haki na masuala ya kujieleza ndio mumbambikie kesi ya ugaidi , polisi waliambiwa wafute kesi za kubambika zaidi ya 200....
Upo Sahihi Kitendo cha IGP kukiri kuwa kuna KESI za KUBIKIZA Alipaswa AMFUKUZE KAZI
 
Kaka kuwategemea hawa wazee wastaafu wa CCM utazeeka, cha msingi movement iendelee na mataifa yote makubwa duniani yajue kwamba hakuna UGADI bali ni sisi watanzania tunadai KATIBA MPYA, katiba itakayotokana na sisi wananchi wenyewe.
 
Ukweli ni kuwa, ccm imeshapoteza ushawishi kwa umma, na inakaa madarakani kwa shuruti. Hapo ilipo ccm haiwezi kukubali majadiliano maana inajua fika majadiliano yataiweka kwenye mazingira ya kuheshimu uchaguzi, na uchaguzi kwao kwa sasa ni ngumu kushinda bila kufanya uhuni. Hao viongozi wa dini hawawezi kusikilizwa na ccm maana watataka ushindani halali, ambao ccm haiuutaki kwani inajua haina ushawishi tena kwakuwa ccm sio chama cha kizazi hiki.

Kwa sasa hao viongozi wa dini kuliko kupoteza muda wao kuandaa majadiliano ya wapinzani na viongozi wa ccm, ni vyema wakawaandalia maombi hao ccm wajue kila kizazi kina matakwa yake.

Ccm sio chama cha kizazi hiki, ndio maana kinalazimisha kukaa madarakani kwa shuruti. Hiyo ccm ni kama zilivyo bendi za sikinde na Ottu jazz, wanaimba nyimbo nzuri, lakini vijana wa kizazi hiki wanataka nyimbo za kina Ali Kiba, Diamond nk.

Mpaka ccm itakapokubali kuwa sio chama cha kizazi hiki, ndio tutapata maelewano ya kweli.
 
Wapinzani wanajichanganya tu wao wenyewe.
Wamejipa kazi ya kupambana na serikali.
 
Wadau nimekuwa nasikia Rais Mstaafu Mkapa ni mpatanishi huko Rwanda kati ya watawala na watawaliwa(baina ya vyama vya siasa) au Rais Mstaafu Kikwete ni mpatanishi burundi kati ya watawala na watawaliwa(baina ya vyama vya siasa) vinapokuwa vinazozana au kutokubaliana katika masuala yahusuyo siasa ,chaguzi au katiba za nchi zao na kupelekea machafuko na vita...
Marais na wastaafu wengi ni wachafu. Wanaogopa kuguswa maslahi yao yanakuwa hati hati. Wangekuwa wasafi kama Warioba wangejaribu lakini kwa sasa hiyo confidence hawana
 
Ukweli ni kuwa, ccm imeshapoteza ushawishi kwa umma, na inakaa madarakani kwa shuruti. Hapo ilipo ccm haiwezi kukubali majadiliano maana inajua fika majadiliano yataiweka kwenye mazingira ya kuheshimu uchaguzi...
CCM haipom. Mi siioni
 
Namshangaa sana huyo Kikwete yuko kimya kabisa kama vile hahusiki. Yule mwingine akili ilishaenda kwao anaweza kumuita Mama Siti na kumuuliza eti hapa tuko chato, Dar au Unguja? 😂😂😂😂
Wadau nimekuwa nasikia Rais Mstaafu Mkapa ni mpatanishi huko Rwanda kati ya watawala na watawaliwa(baina ya vyama vya siasa) au Rais Mstaafu Kikwete ni mpatanishi burundi kati ya watawala na watawaliwa(baina ya vyama vya siasa) vinapokuwa vinazozana au kutokubaliana katika masuala yahusuyo siasa ,chaguzi au katiba za nchi zao na kupelekea machafuko na vita...
 
Wadau nimekuwa nasikia Rais Mstaafu Mkapa ni mpatanishi huko Rwanda kati ya watawala na watawaliwa(baina ya vyama vya siasa) au Rais Mstaafu Kikwete ni mpatanishi burundi kati ya watawala na watawaliwa(baina ya vyama vya siasa) vinapokuwa vinazozana au kutokubaliana katika masuala yahusuyo siasa ,chaguzi au katiba za nchi zao na kupelekea machafuko na vita...
It is difficult for them to do so because they are beneficiaries of the situation.
 
Back
Top Bottom