Marando atangaza kulitetea MwanaHalisi bure


Mkuu FMES,

Narudia kusema kuwa bado sisi ni marafiki na kama nilivyosema kuwa nitaendelea kukupa heshima kama mwanzo I meant that. Labda ningesema kuwa PM zako nyingi zilikuwa za kunitia moyo hapa hasa baada ya watu kutoa sexist comments kuhusu mie (ninakuwa fair and balanced ya NBC sio ya FOX NEWS).

Usijekunitosa mkuu kwenye sherehe nyingine mtakayopanga maana kama sikosei baada ya mafanikio ya ile ya NY, makubaliano yalikuwa ni kufuata ushauri wa Mwawado na kupanga bash nyingine.

Otherwise tuzidi kupingana bila kupigana au kupondea JF!
 
Otherwise tuzidi kupingana bila kupigana au kupondea JF!



Mkuu mimi kuipondea JF? are you serious? Kama ni kweli nisingekuwa ninawatumia viongozi ishus za hapa mkuu, na nisingewavuta viongozi wengi ambao wapo hapa kila siku silently,

Kwenye hilo mkuu, la kuipondea JF hukunitendea haki mkuu, maana sidhani kama lina ukweli ndani yake, maana ni mimi siku zote nimekuwa mstari wa mbele kukataa kuwa hpa akuna matatizo serious huwa ninasema kuna some isolated ishu ambazo ni za kawaida katika demokrasia, na wewe unajua in details jinsi nilnavyokataa kila siku kujiunga na forum zingine na unajua jinsi zamani nilivyokuwa nikikataa kutoka BCS kuja huku, maana ni tabia yangu ku-stick na one place at a time, ndio maana hata nilimkatalia Marehemu Chachange, kuingia kule Tanzanite,

Kwenye kuipondea JF, hujanitendea haki mkuu!
 
field marchall kweli unaipenda sisiem. wewe ni kati ya wale vijana wa sisiem ambao kila kukicha wanaongea pumba tupu? mbona hauko systematic katika argument zako? poleni sana.
 
1.
Mushobozi
Senior Member

-----------------------------------------------------------------

fild marchall kweli unaipenda sisiem.

Kama wewe unavyoupenda upinzani mkuu.


2.
wewe ni kati ya wale vijana wa sisiem ambao kila kukicha wanaongea pumba tupu?

Unajua kuongea pumba, ni pamoja na kuongea pumba huku ukifikiri unaongea hoja, kumbe ndio pumba yenyewe hasa unayoisema na kujinyooshea kidole wewe mwenyewe huku ukidhani unawanyooshea wengine!

3.
mbona hauko systematic katika argument zako?

Duh, ni lini siasa ya taifa letu na ya dunia tunayoiongela hapa iliwahi kuwa systematic, the day itakapokuwa systematic naomba unifahamishe ili nami nanze kuwa systematic, otherwise I stay the same un-systematic ili niwe on top of the game inayochezwa kwenye un-systematic system ya dunia!


4.
poleni sana.

Pole ikurudie mkuu maana ni clear nani kati yangu na wewe anaihitaji zaidi!

Ahsante mkuu, tuendeelee kukata ishus bros!
 
 
kama ni pumba elezea ni ipi niliyoiongea. ila wale vijana wa ccm ni mara nyingi wamefanya vile hata wanachikitetea hawajui, utasikia hoo! mkataba wa buzwagi hauna matatizo.baadaye inagundulika unayo, mara hoo...mgomo chuo kikuu sio halali, baadaye vyuo hivyo na serikali ya sisiem inakubali hoja yao kwa kutimiza masharti, tatu angalia tunachokiongelea na hoja unazozijenga, hamna kipya bali tu kunakili yaliyoisha semwa. si o pumba hizi?

nisingekuwa ninakuelewa kupitia makala zako hapa forum, ningedout uwezo wako, ila kwa muda mrefu ninakubaliana na wale watakaosema unafanya makusudi ili kuvuruga hoja zisijadiliwe vizuri.

naomba kuwasilisha hoja.
 
 
1.
Habari mukulu,

a)Ningeomba kujua maana ya busara ni nini? Tapeli au jambazi akianza kazi yake hiyo tangu utotoni akifikisha Miaka 72, atakuwa na busara ya kujua mbinu bora za kuiba au atakuwa na busara wa kujua kuwa kazi sio nzuri?

Mkuu Nyangumi,
Heshima mbele mkuu,

Ingawa argument yako sio clear, lakini nitajaribu kuielewa na nikikosea nirekebishe, wewe ninakuamini kwa kichwa makini, Malecela, ametuhumiwa kwa mengi ya uongo na kweli, lakini wizi au ujambazi, halijawahi kuwa one of them, bunge letu lenye upinzani na CCM, ndilo linalotakiwa kutoa maamuzi muhimu ya taifa, lakini kwa sababu ya ujinga wa wabunge tunaowachagua sisi wananchi kila wakati, matokeo yake leo ni waziri mkuu ndiye anayeamua maamuzi ya bunge ndani ya bunge,

Kawawa, ndiye aliyekuwa the first makamu wa CCM, under Mwalimu, lakini sijawahi hata siku moja kusikia kwanza akilaumiwa under utawala wa Mwalimu, kuwa ndiye aliyekuwa akitoa uamuzi mbaya ya siasa za ujamaa zilzoturudisha nyuma kiuchumi for 100 years back, au kwa sera za maadili mema ya viongozi, maana wote tunajua kuwa kinara wa maamuzi kwa mujibu wa katiba yetu alikuwa rais wa nchi, yaani Mwalimu. Sasa nashangaa sana leo tunajifanya kuwa hatujui hilo kuwa kisheria zetu, muamuzi wa mwisho bado ni rais na sio makamu wa ccm, otherwise nilisema huko nyuma kuwa kwenye hii forum huwa kwenye maisha tunapenda kuwaongelea watu au viongozi tunaowapenda sana na sidhani kama kuna doubt kwenye hilo la Malecela kupendwa na hii forum.

2.
b)Je kuna tofauti ya kuwa na busara na kuitumia? Kama unabusa na huitumii kuna haja ya kuitwa kuwa ni mtu mwenye busara? Kama jibu ni ndiyo,je haimaniishi kuitumia busara hiyo negatively ni kuwa unafavour your own interest?

Labda hapa the argument, inapaswa kuwa namna ya kuitumia busara kwa faida ya taifa, wananchi, au siasa tu, maana busara inaweza kutumika kwa faida ya wananchi lakini sio wote, isipokuwa msema kweli anakuwa matokeo ya kura za uchaguzi, kama nani kati ya upinzani na watawala, ambao busara zao zinakubalika na wananchi zaidi, busara hizo kuwa nzuri au mbaya, nafikiri inategemea na zinamuhusu nani au nani anahusika nazo, au?


3.
Mie nilidhani busara ya akina Malecela ingeweza kutumika katika kukirekekisha chama na sio kufuata mikumbo?

Chama cha CCM, kiko fine na wewe unajua vyema hilo, je ni busara za nani ninaamini ni busara za wanachama wote wa ccm, je ccm haina matatizo binafsi? Yes, inayo tena mengi so is upinzani pia, je ccm inahitaji kurekebishwa hilo ni swali ambalo sidhani kama ni interest yetu hapa forum, au taifa, sisi tatizo letu hapa forum linatakiwa kuwa viongozi wa taifa, na sio wa vyama vya siasa, unless hao vyama wamevunja sheria zetu za taifa then yes, ccm hata wakiamua kumpa Makamba, ingwa siku zote huwa tunapiga kelele sana hapa, lakini ukweli ni none of our business, yanayojiri ndani ya vyama vyetu vya siasa!

Sijui kama nimekusaidia mkuu, Heshima mbele mkuu!
 
1.
Mushobozi
Senior Member
-----------------------------------------------------------------

kama ni pumba elezea ni ipi niliyoiongea. ila wale vijana wa ccm ni mara nyingi wamefanya vile hata wanachikitetea hawajui,

Maneno ya pumba ni yako mkuu sio yangu, mimi sio hao vijana wa CCm unaowasema, ninajua ninachokisema na ninachokitetea na nisichokitetea, ila sitetei ujinga hata siku moja regrdless umefanywa na nani ccm au upinzani, maana ujinga ni ujinga, na sijawahi kuwa bendera fuata upepo, ingwa juhudi nyingi zimefanyiak na zinaendelea kufanyika kunifanya niwe hivyo, I remain independent

2.
utasikia hoo! mkataba wa buzwagi hauna matatizo.baadaye inagundulika unayo,

Suala la mkataba wa Buzwagi, sijawahi kuwa na sura mbili hata siku moja, na hata suala zima la mafisadi, ninaaamini kuwa wewe ni mgeni hapa maana ungekuwa mwenyeji, then ungekubali kuwa viongozi wa ccm wanaojitokeza sasa hivi wanaiga maneno yangu sana, maana mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuleta orodha ya mafisadi hapa, na nilikuwa wa kwanza kupambana na Mgonjwaukimwi on the ishu, yeye alisema hakuna ushahidi mimi nikasema wanahitaji kwenda mahakamani kwanza kujua kama upo au haupo, je leo viongozi wengi husikii wakiimba hupo wimbo wangu? Waombe Mods wakupe hiyo thread ya hiyo ishu ilipokuwa mbichi kabisa mkuu naona unadandia tu, uliza kwanza mku,

Na mimi pia ndiye niliyekuwa wakwanza hapa kuleta ripoti ya Hosea na Richmond, na nikafanya utafiti wa kina na kuutoa hapa kuhusu exactly what happened na waliohusika na huo mkatba, pia waombe mods wakupe hiyo tread, acha kurusha accusations bila facts.


3.
mara hoo...mgomo chuo kikuu sio halali, baadaye vyuo hivyo na serikali ya sisiem inakubali hoja yao kwa kutimiza masharti,

Yaaani uantaka niongelee wanafunzi walioenda kwa rais Kikwete, huku wamevaa uniform za CCM? eti unasema waligoma? Waligoma nini?


4.
tatu angalia tunachokiongelea na hoja unazozijenga, hamna kipya bali tu kunakili yaliyoisha semwa. si o pumba hizi?

Mkuu mimi ninanakili maneno ya mtu hapa? are you serious? Pumba? Hilo ninawaachia wananchi hapa forum, kuwa mimi na wewe nani anyeongea pumba so far?

5.
nisingekuwa ninakuelewa kupitia makala zako hapa forum, ningedout uwezo wako, ila kwa muda mrefu ninakubaliana na wale watakaosema unafanya makusudi ili kuvuruga hoja zisijadiliwe vizuri.

Mzee nenda kule kwenye closed topics, utakuta topic ya mimi kutimiza post 2000, please ninaomba uniletee any post inayosema kazi yangu ni kuja hapa kuvuruga ishus, you have facts twisted mkuu, nani kati yangu na wewe sasa hivi anyetaka kuuvuruga huu mjadala mkuu?

6.
naomba kuwasilisha hoja.

Kwenye hii post yako hoja iko wapi mkuu? hivi ni kweli unajua maana hasa ya hoja au? Yaaani mkuu nimewahi ku-debate na watu wengi humu forum wasiojua kinachoendeela kwenye hii forum na taifa letu kwa ujumla, ila sidhani kama kuna anayekuzidi mkuu!

Ahsante Mkuu, tuendelee kukata ishus!
 
Duh hii thread inasemaje?....kila ninavyozidi kusoma post za watu nashindwa kuelewa thread inasema vipi
 
Ok,suppose Marando haaminiki,what about Tambwe,what about Akwilombe?What about WASSIRA,What about NSANZUGWAKO,What about Walid Kaburu?So many names,so little time and space.In fact,at least tunaweza kumwamini Marando kwa vile he's got everything to lose and nothing to gain in the case.Lakini hao political prostitutes sio tu hawapaswi kuaminika lakini pia ni mzigo kwangu na kwako coz wanaendelea kutafuna fedha za walalahoi kwa kisingizio cha "kuwaumbua wapinzani."

Ok,suppose Marando ni Usalama wa Taifa,ina maana kuwa kila mtu wa system ana-enjoy kuona nchi inavyotafunwa?Naamini wapo wenye uchungu na nchi yao na huenda ndio hao wanaowapa nyaraka nyeti akina Slaa.Hata huko BOT kwenye ufisadi kuna wasioridhishwa na wizi wa Balali et al.

Ok,may be wanaomjua Freeman wanaweza kusema hajawahi kuwa mpinzani.Mie simjui kwa kukutana nae bali namjua kama mmoja wa wanasiasa mahiri wa TZ,KWA MATENDO YAKE.Na kwa mtu ambaye sio mpinzani hata siku moja sidhani kama angethubutu kwa mfano kuandika zile makala zake kwenye Tanzania Daima.

Bravo Marando kwa uamuzi wako huo wa kishujaa.Bora wewe unayeweka reputation yako on the line of fire kwa kutetea BURE gazeti pekee lililoripoti ufisadi kuliko hao akina Mkono,IMMA,etc wanaolipwa mamilioni ya dola za walalahoi kutetea mafisadi.
 
Mlalahoi
JF Senior Expert Member
-----------------------------------------------------------------
Ok,suppose Marando haaminiki,what about Tambwe,what about Akwilombe?What about WASSIRA,What about NSANZUGWAKO,What about Walid Kaburu?So many names,so little time and space.In fact,at least tunaweza kumwamini Marando kwa vile he's got everything to lose and nothing to gain in the case.Lakini hao political prostitutes sio tu hawapaswi kuaminika lakini pia ni mzigo kwangu na kwako coz wanaendelea kutafuna fedha za walalahoi kwa kisingizio cha "kuwaumbua wapinzani."



Mkuu Heshima mbele, maneno yako ni mazito na ni kweli tupu, But, hawa juu ni reflection tu ya character zetu sisi wananchi wa bongo, au?
 
Ndugu wanaJF
Lazima tukumbuke kuwa kuna political mathematics ambazo watu wanafanya kutoka na malengo fulani. Sasa hizo hesabu zinaweza kuwa kwa personal gain au kwa manufaa ya kundi. Definition ya opposition literary maana yake ni kupinga, lakini kwenye siasa nadhani tuna maana ni kuwa kwenye upande usio wa serikali ukiwa kwenye harakati za kujaribu kuingia serikalini ili kuingia serikalini na kukalia dola na kurekebisha mambo yanayokwenda ovyo. Ukiangalia definition hiyo utagundua kuwa baadhi ya watu ambao Tanzania wanajiita wapinzani si wapinzani kweli.
Marando aliingia kwenye upinzani ili kuwa neutralize wakati serikali ikiwa ovyo kupita wakati wowote ule wa historia ya Tanzania, so as kina Mapalala, na Jafu wote hao ni maofisa usala wa taifa ambao walifanya kazi zao za kuwavuruga upinzani vizuri.
Lakini wapinzani wanaotaka kurekebisha maovu ndani ya serikali, nadhani wako kote, nje ya CCM, Nje ya serikali, ndani ya CCM na ndani ya serikali, na hapo ndio kunakuwa na strong and constructive opposition for the better of our country, nadhani hapa cha muhimu ni nchi yetu.
Ndio maana sina imani na watu kama kina Marando, kama lengo lao hasa ni kusaidia au kubomoa. Sasa hivi ni wazi kuwa nchi yetu iko njia panda, scandals zinaibuliwa moja hadi nyingine, kuna posibility kuwa zinaweza kuwaua watu kisiasa, sasa inategemea lengo halisi la hao wanaojidai kuwa wanania ya kusaidia.
 
Can Marando be truested? Huyu jamaa mission zake ni wazi kabisa, ni ofisa usalama wa taifa ambaye huwa anatumiwa na CCM kurekebisha mambo yao. Siquestion uwezo wake wa kazi ila naQ intetion yake. Just opinion

....this fool AKA amabere marando cant be trusted na ni mbaya kuliko mafisadi maana jinsi alivyorudisha upinzani nyuma god know,i've no respect to this man he deserve NO THANK YOU kutoka Mwanahalisi...this fool is the big traitor!
 

Nakuunga mkono Mkuu
 
Wakili Mabere Marando anawakilisha Gazeti la Mwanahalisi na pia Mkurugenzi wa Hali Halisi Bw. Saed Kubenea. Je, sasa wana mpango gani baada ya kujikuta wanafungiwa kuchapisha gazeti hilo kwa muda wa miezi mitatu?

Aliyefungia gazeti hilo ni Waziri wa Habari, utamaduni na Michezo Mhe. George Mkuchika. Je alifanya kosa kulifungia gazeti hilo? NI kwanini basi hakuyafungia magazeti mengine ambayo yaliandika habari zinazoshabihiana na zile zilizosababisha gazeti la Mwanahalisi kufungiwa.

Wakati huo huo Kijarida cha "Cheche" nacho kiko mitaani; What a wednesday Eh?

Kupata majibu ya yote hayo sikiliza kidokezo hiki:

http://www.klhnews.com/images/podcasts/maberemkuchikaintro.MP3
 


Lakini si tumeambiwa habari za Mkuchika zisiripotiwe kwa muda wa siku 90?
 
Waziri huyu anajazba kwelikweli! Inaonyesha ametumwa na boss! Amenisisimua sana pale aliposema wamepata simu nyingi sana kuwapongeza kwa kulifungia Mwanahalisi! Najaribu kuwa list kichwani hao waliopiga simu... sjapata mzalendo hata mmoja! Huyu Mh. walikuwa wanasema/wanatuamisha siku nyingi kuwa ni mtu makini, lakini kwa mahojiano haya nadhani wengine tumejipatia uhakika kuwa tumekuwa tunalishwa sumu juu ya sifa na hulka yake! Kama amesoma sana literature na yeye anasoma sna habari kwa sababu ni waziri wa habari basi naamini hata hapa JF yupo! Mh, kumbe uwaziri mgumu, afadhali ungeendelea kuwa Mbunge tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…