Elections 2010 Marando kuibomoa CCM

Elections 2010 Marando kuibomoa CCM

Nsololi

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2007
Posts
298
Reaction score
80
Tuesday, 31 August 2010
Geofrey Nyang'oro

KADA wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando ametamba kuitikisa CCM na serikali yake kwa hatua yake ya kuwahusisha viongozi wa nchi na ufisadi wa Akaunti ya madeni ya nje (Epa)uliofanyika Benki Kuu.

Lakini CCM wamesema bado wanatafakari kauli hiyo kwa makini ili kuona hatua inayofaa kukichukulia chama hicho cha upinzani.

Juzi, Marando alirudia kauli hiyo na kusema bado anaamini kuwa mafisadi wa kweli hawajafikishwa mahakamani.

Alisema hayo kwenye mkutano uliofanyika katika viwanja vya Bunju Dar es Salaam kuzindua kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chadema, Halima Mdee.

Katika mkutano huo Marando alisisitiza kuwa watu waliofikishwa mahakamani si mafisadi, bali ni matawi ya ufisadi.

Huku akishangiliwa na umati wa watu Marandu alisema " Jana (Juzi) nilipozunguzia hili (TBC) walikata mitambo yao,sasa leo narudia tena na hapa hukuna mitambo siju watakata nini,"alisema Marandu na kucheka.

"Niliwaambia kumfunga Liyumba, kumshitaki Maranda na wengine ambao kesi zao ziko mahakamani kwa sasa siyo suluhisho la ufisadi hapa nchini, nasema hivyo sababu wale waliofikishwa mahakamani ni matawi tu na mafisadi ni mti mkubwa ambao unatakiwa kung'ongewa"alisema Marando.

Mafisadi hali ni wale waliotajwa na Dk Slaa waziwazi katika viwanja vya Mwembe Yanga, alitaja majina yote na kuonyesha Watanzania wote kuwa kumbe wizi uko hata (Bot) mahali ambapo Watanznaia hata siku moja hamukuamini kama kuna wizi unafanyika,"alisema.

Akifafanua maana ya ufisadi alisema "mafisadi maana yake ni viongozi wanaotumia nafasi zao kuchota fedha za umma zilitengewa kwa ajili ya ujenzi wa huduma za kijamii kama shule ,Zahanati,barabara n.k na kuzitumia wao binafsi na marafiki zao.

Katika mkutano huo pia Marando aliwaasa wakazi wa Kawe kutochagua wagombea wa CCM na NCCR Mageuzi kwa kuwa hawatakuwa na msaada wa kimaendeleo kwenye jimbo hilo.

Kuhusu Mgombea Ubunge kupitia NCCR Magezuzi James Mbatia Marando alisema ndiye aliyesababisha yeye kukihama chama hicho.

"Mimi ni mkazi wa jimbo hilo, maendeleo ya jimbo hili yananihusu, nilimwambia Mbatia kama atagombea Ubunge katika jimbo nitakihama chama hicho kwa kuwa yeye hana uwezo wa kuongoza na amekiua chama hicho"alisema Marando.

Alisema amekihama sababu anajua mgombea huyo kupitia NCCR Mageuzi hana uwezo wa kuongozi kutokana na kushindwa hata kufuatilia matatizo makubwa ya ardhi yaliyowakumba wakazi wa eneo hilo huku akiwa kama mwenyekiti wa chama hicho na mkazi wa Jimbo hilo.


Kwa upenda wake mbunge wa zamani wa Jimbo la kishapu kupitia CCM Fred Mpendazoe ambaye kwa sasa anawania Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chadema alikitabiria kifo chama chake cha zamani aliposema kifo hicho kinatokana na kukumbatia rushwa na ufisadi.

Akizunguza wakati wa uzinduzi huo Mpendazoe ambaye alikuwa msemaji wa kwanza kwenye kampeni hizo alisema kitendo cha CCM kukumbatia mafisadi ni dhambi na hukumu ya dhambi ni mauti.

"CCM haitapasuka tu bali itakufa kabisa sababu imekumbatia rushwa na rushwa ni dhambi malipo ya dhambi ni mauti"alisem Mpendazoe

Katika mkutano huo Mpendazoe aliwataka wakazi wa Bunju na Watanzania kwa ujumla kutochagua CCM kwakuwa serikali inayotokana rushwa haina uwezo wa kufanya maamuzi magumu kama kushughulikia mafisadi
 
Marando naona kaamua,ila kama sina imani nae vile asije akawa kaja kuspy.
Ila Dr aminia kama kaja spy atamstukia soon
 
KUMBE DAWA YA TBC NI KUTOWAITA KWENYE MKUTAnoi si mnaona kule bunju mambo yameenda safi wala tbc hawakukata mitambo tena.................KWELI NAAMINI HAKI HAIPATIKANI KWA SIKU MOJA.....
 
Huyu Marando ataibomoa CHADEMA, kuweni makini sana na huyu jamaa haaminiki
 
Marando naona kaamua,ila kama sina imani nae vile asije akawa kaja kuspy.
Ila Dr aminia kama kaja spy atamstukia soon

Haya mawazo ya u-spy yanapandikizwa na CCM kwa makusudi kwa sababu wanafahamu kuwa Marando hana breki katika kufichua jambo lolote analolijua. Ni mtu shupavu asiye na chembe ya woga. Huyu ni mpiganaji wa ukweli! Endelea kamanda Mabere Marando, tupo nyuma yako.
 
Marndo wa ukweli bwana, anaspy nini huyu ameamua kujifunga mabomu na kwenda sambamba na Dr Slaa.Pipooooooooooooooos Pawaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Haya mawazo ya u-spy yanapandikizwa na CCM kwa makusudi kwa sababu wanafahamu kuwa Marando hana breki katika kufichua jambo lolote analolijua. Ni mtu shupavu asiye na chembe ya woga. Huyu ni mpiganaji wa ukweli! Endelea kamanda Mabere Marando, tupo nyuma yako.


I wish wa-tz wangefunuliwa na kupewa maamuzi niliyonayo mimi!
Tuitose ccm, wakae benchi alafu tuwape nafasi akina Slaa watuonyeshe njia!
 
CHADEMA wakae wakijua Marando ni spy wa CCM kwa hiyo kazi kwao tumekwisha wapa angalizo siku nyingi sasa kama wanamng'ang'ania shauri lao.
 
CHADEMA wakae wakijua Marando ni spy wa CCM kwa hiyo kazi kwao tumekwisha wapa angalizo siku nyingi sasa kama wanamng'ang'ania shauri lao.

Acha uongo! Marando ni mtu makini na muadilifu hawezi kuwa wa double standards. Mtu ambaye nina wasiwasi naye ni Shibuda, wasimwamini sana kwa sababu alishadai kwamba yeye ni rafiki wa karibu wa JK!
 
Acha uongo! Marando ni mtu makini na muadilifu hawezi kuwa wa double standards. Mtu ambaye nina wasiwasi naye ni Shibuda, wasimwamini sana kwa sababu alishadai kwamba yeye ni rafiki wa karibu wa JK!

Ni kweli uyasemayo, wana ccm wanampaka matope kwa kuwa M Marando amekuwa mwiba kwao!
 
Back
Top Bottom