Marcelo Galardo,kichwa kingine bora kabisa kutoka Argentina

Marcelo Galardo,kichwa kingine bora kabisa kutoka Argentina

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Baada ya Fulltime kuwaletea makala inayozungumzia Derby kali kabisa ya Amerika Kusini katika ya Boca Juniors na River Plate , basi tunawaletea na namna wanavyocheza tunaanza na River Plate hasa chini ya kocha Marcelo Gallardo…

Klabu ya soka ya River Plate kutoka Argentina wamethibitisha kwamba kocha wao wa sasa Marcelo Gallardo ndio bora kabisa katika historia ya klabu yao , yes huyu ndiye aliyechaguliwa na Leo Messi kua moja ya makocha bora kabisa kwa mwaka 2019 . Ni muendelezo wa dunia kuzidi kupata walimu wa mpira ambao ni vichwa haswaa , achana na huyu Gallardo yupo Julian Nagelsmann wa RB Leizpig Eddie Howe wa Bournemouth Frankie Lampard na Chelsea Steven Gerrard na Rangers hata Mikel Arteta anakuja kuja , hawa vijana ndio wanavuruga kina Mourinho na mifumo yao ya kizamani …

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa kbalu za River Plate , Monaco , PSG , D.C United , Nacional na timu ya taifa ya Argentina . Tokea aichukue timu kutoka kwa mzee Lamon Angel Diaz 2014 mpaka sasa amechukua makombe kumi yakiwemo mawili ya klabu bingwa America Kusini , ila kombe la ligi kuu Boca Juniors amekamia shoo hana masihara . Kikubwa ni swala la mbinu na falsafa za Gallardo , nyota yake imeshindwa kukataa kung’aa kabisa hasa mbinu zake , sawa bara la America Kusini vinatoka vipaji vya soka saana lakini soka lao ni pasua kichwa sanaa , Derby yao dhidi ya Boca Junior ni pasua kichwa hata ile ya Corithians na Palmeiras ya pale Brazil ni pasua…

Marcelo Gallardo ameamua kumuunga mkono Victor Maslov muasisi wa mfumo wa 4-4-2 ila nae anauboresha kivyake vyake , kwa sasa anapasua mawimbi na mfumo wa 4-3-1-2 (four four two diamond) , kuna muda anakuja na 4-3-2-1 au 4-1-3-2 au 3-4-2-1 au 3-1-4-2 . Achana na mingine yote kipenzi chake ni 4-3-1-2 hapa ndo roho yake ilipo , kumbuka lengo la hawa makocha wanaopenda huu mfumo akiwemo Brendan Rodgers lengo lao ni kutengeneza pembe tatu nyingi , uwepo wa pembetatu yaani baina ya wachezaji huwapa machaguo mawili ya kupiga pasi , pia inatoa uwanda mpana wa kupata Half spaces hapa mpira unapigwa eneo la wazi na mchezaji hukimbia eneo la wazi tukutane mbele (through pass/pasi mipenyezo).

Bwana Gallardo akikutana na vibonde basi anapandisha mmoja juu na kua 4-2-2-2 anakua na viungo washambuliaji wawili na kutumia viungo wakabaji wawili , hapa huongeza uzito katika eneo la kiungo na huleta numerical advantages . Kama tujuavyo mfumo wowote wa 4-4-2 hukusanya viungo wengi sana ivyo basi Gallardo anakua na nguvu kubwa ya kukaba eneo la kiungo , hapa hubadilika na kuwa 4-2-3-1 anaipress timu saana eneo la kiungo…

River Plate pindi wakipata mpira wanaanza na mipira mirefu kama Sean Dyche sema yeye anaisubiri timu ipande , lengo la kufanya ivi ni kuanza build up eneo la mpinzani , hapa anatengeneza timu inayokaribiana sanaa kama Arigo Sacchi na Ac Milan na lengo kubwa na kupata mianya ya kupiga pasi fupi fupi kwa wingi . Marcelo Gallardo huyu jamaa ni kocha anaependa kushambulia (attacking minded coach) , River Plate asili yao ni kumiliki mpira kwa nguvu ivyo kama walivyo Barcelona na Man City ni bora saana katika takwimu za kushambulia . Jamaa wana udhaifu mkubwa saana hasa katika kukaba , pia makosa binafsi ni mengi saana…
 
Thank you so much kamanda wangu...moja ya vilabu navikubali sana sana, I'm Boca labombonera and The Millionaires) La Banda (The Stripe) Las Gallinas (The Hens-River Plate fan 👈

Hawa wahuni wa America ya kusini acha kabisa, by Style na falsafa yao kiasi flani imefanana na Barcelona and Man city....
 
Back
Top Bottom