March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

demokrasia ni ghali sana kuigharamia,pengine uchaguzi utaenda round ya pili!mudavadi angebaki jubilee mambo yangekuwa yashaisha tayari!

Na wakienda round two unadhani Mudavadi atarudi kumuunga mkono Kenyata au atarudi kwa swahiba wake wa zamani Agwambo??
 
Matokeo yako hivi.
Suala la Uchaguzi limepelekwa Mahakani kupinga matokeo haya.
Wanataka mfumo wa dijitali utumike pia sehemu
nyingine kura zimepogwa nyingi kuliko waliojiandikisha.

Source: Citizen tv live broadcasting.
 
YA SASA HIVI NI KAMA IFUATAVYO
UHURU 5,060472
RAILA 4,512490
MUDAVADI 368,959
wengine wote wana kama 160,000
SOURCE k24 tv

hapo raila sasa anaombea duru la pili, la kwanza keshashindwa, ndio maana anataka kwenda mahakamani. ni mapema mno kusema lakini uchaguzi wa kenya unaonesha wazi kuwa uhuru na ruto wanakubalika kuliko Odinga, siasa wanaijua vizuri, Nafikiri ODINGA akiwa waziri mkuu ameshindwa kuwa fair wakenya wamkubali, hiyo alitegemea umaarufu wa mwaka 2007. anyway wapiga kura wameamua UHURU ANAONGOZA, SASA UHURU ANAITAJI KURA LAKI TANO TU ACHUKUE NCHI
 
Gap liko laki 6, naona Jubilee wanataka lifike laki 7 wamalize ubishi.
 
Mkuu Arushaone Mudavadi alikosea sana hesabu ila nadhani kajifunza sana, maana za wa nyumbani kwake kagawana na raila!
Eh huu uchaguzi sasa basi jamani, wamalize tu tujue moja!
Unajua mama D huyu Mudavadi hata kama kungekuwa na sheria ya kwamba anaweza kuamua kumpa kura yeyote anayemtaka kati ya hao wawili na yeye akaamua kumpa jirani Raila bado mvua ya mawe ya Uhuru na Ruto ingesiwaacha hata kama ya mawe ingewakosa basi wangepambana na rasharasha ya kuanzia saa kumi usiku hadi saa tano asubuhi, si unajua mvua ile inasababisha watu wa mjini wakose kwenda kazini na sisi wa mashambani tushinde njaa kwa sababu kuni zimelowa?
 
Huyo atakuwa mwingine, mimi Masuke ndo first name yangu.
 
Nadhani a lot will depend wangapi walipiga kura.., kama registered ni 14m; na sidhani kama wote walipiga kura.., na tukiondoa zilizoharibika nadhani jamaa akigonga kwenye milioni tano na nusu atakuwa amepata nusu ya kura zote plus one vote (assuming number ya waliopiga kura ni around 11m)
 
Mkuu imani yako sio ya kuhamisha milima tu bali mito na maziwa na bahari kabisa, kwa nini mwenye nyingi tusimwone kama mshindi badala yake unataka kutuaminisha kwamba mwenye chache ndo atashinda?
kwanini useme ameshinda wakati hajatangazwa wala hawajamaliza kuhesabu? Mpira dakika 90. mwanzo si ulijua masaa 24 baada ya uchaguzi Rais atakakua kashatangazwa?. Ndo maana nasema tulia uone maajabu ya kenya. mia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…