Mkuu sijui kama umewahi kushiriki kuhesabu kura. Kama umewahi, basi haukuwa makini kuangalia ni kitu gani kilifanyika. Huwezi kuanza kuhesabu kura kabla ya kujua idadi ya kura zote zilizopigwa kwenye kituo. Hatua ya kwanza kwenye zoezi la kuhesabu kura, ni kujua idadi ya kura zote zilizopigwa bila kujali kama zimeharibika au vinginevyo. Mkiishajua idadi ndio mnakwenda kuhesabu per candidate na vile vile kujua ni ngapi zimeharibika. At the end of the exercise, idadi ya kura alizopata kila mgombea zinajumlishwa ili kuona kama idadi ile inaendana na jumla ya kura zote zilivyopigwa. Kama ulikuwa hujui hii, basi leo umepata nafasi ya kujifunza.
Tiba