Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uhuru ni mshindi wa urais
Hiyo 42.40% sio sehemu ya kura zilizopigwa bali ni sehemu ya waliojiandikisha, huwezi kujua idadi ya watu waliopiga kura kama hujamaliza kuhesabu, ukitumia assumption ya kwamba 70% ndo ilikuwa turnout kwa hiyo kura zilizohesabiwa ni zaidi ya 50% ya kura zote zilizopigwa.
there is another assumption the candidates must score 25% of the vote from each consistuent so it not just victory. it all about about degree of acceptance from all parts of the Republic of Kenya, right?Mkuu MkamaP,
Inaonekana Mathematics inakupiga chenga Bro. Kulingana na maelezo yako kama kura za wagombea wengine ukijumlisha na za Odinga hazitafikia idadi ya kura za Uhuru maana yake ni kwamba Uhuru tayari ana above 50% ya kura zote kitu ambacho si sahihi kama wakirudia uchaguzi. Kama wakirudia uchaguzi maana yake hakuna aliyefikisha above 50% na kwa msingi Simple Mathematics inasema kama ukimuondoa mgombea yoyote (hata wa mwisho au wa kwanza) then ukajumlisha kura za waliobaki obvious zitakuwa zaidi ya 50%. Sasa ni vipi Odinga hatashinda uchaguzi kama uchaguzi ukienda second round??
Kuwa makini unapotoa comment zako Mkuu.
TUMBIRI (PhD In progress, CPA(T), MBA(UDSM), Bcom(UDSM), PCM(Mzumbe High School - 2[SUP]nd[/SUP] Overall Best Student in Form six National Exams),
tumbiri@jamiiforums.com
Nakala: Crashwise, Ndalo, Mwita Maranya, Ngongo
ME naona kama UHURU anachukua urais. Raila pole sana jamani, wakenya wengi wanakupenda ila kura hazitatosha.
Only time will tell!!!Hivi huyo Mlevi hapo TBCCM Clemence Mshana kwa nini asitoke hata kwa kutekwa Nyara.
Maamuzi mazito. Baada ya servers kufeli iebc imeamua kujumuisha matokeo manually. Je tatizo ni system hacking?
Maamuzi mazito. Baada ya servers kufeli iebc imeamua kujumuisha matokeo manually. Je tatizo ni system hacking?
Hapa kuna vitu vingi vinaweza kutokea ikiwa ni pamoja na hiyo system hacking. Au pengine ni mtandao kuwa slow, au pengine ni uwezo mdogo wa wataalamu wa IT hasa kwenye issue kama hii yenye changamoto lukuki.
Hili la mtandao kuwa slow linatia shaka. Safaricom network mbona imara tu. Rumours are circulating to effect that hackers have installed code that is churning fake results! Watch trend baada ya iebc kufanya majumuisho manually.
Kenyata anaingia ikulu kwa hali hii.
there is another principle; that prospective winner candidates must score 25% of the votes from each constituency so it not just a simple victory. it all about about the degree of acceptance from all parts of the Republic of Kenya, right?
Mkuu,
hii thread ni non-partisan in terms of politics.
Sisi tuna-critic hawa IEBC na jinsi walivyoandaa hizi kura na ukiangalia thread nyengine nime-post hapo
juu, watu walikua washatoa warning about their inability to carry out such an important task kitambo
lakini watu wakapuuza.
Now here we are.
Tiba, siyo 50%+1?Wakuu, kuna new development hapa ambayo iko likely kumzuia Uhuru kupata ushindi kwenye hii round ya kwanza. Wachunguzi wa mambo wanasema ili mtu ashinde inabidi apate at least 51% ya kura zote zilizopigwa. Hii ina maana ya kwamba even spoilt votes inabidi zipewe percentage hapo kabla ya kuamua mshindi ni nani. Endapo kura karibu 500,000 zilizoharibika zitaongezwa hapo na kupewa % ya kura zote zilizopigwa, ina maana % ya Uhuru itashuka kuwa chini ya 53% alizonazo kwa sasa.
Suala lingine linalotia shaka ni kwamba kura nyingi za Nairobi hazijawasilishwa kwenye tume ili ziongezwe kwenye total votes tally. Sasa unaweza kujiuliza ni kwa nini kura za Garissa, Wajir, Kisumu, Kisii huko pembezoni zimewasilishwa kwenye tume ila za Nairobi bado ambako hata kwa mguu mtu naweza kutembea mpaka hapo Bomas to kupeleka hiyo fomu ya matokeo inayoitwa number 34.
Kuna tetesi vile vile kuwa IEBC imesitisha kupokea matokeo ya kura electronically si kwa kuwa devices zimeshindwa kufanya kazi, bali wanajaribu kuepuka hackers wasivamie hiyo system ya tume na kuingiza kura feki.
Kwa sasa ni kama mambo yamesimama, lakini mwenyekiti wa IEBC alihaidi jana kwamba atatangaza matokeo leo ingawaje sheria inampa siku saba za kufanya hivyo.
Tuendelee kusikilizia.
Tiba