March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

je ICC ikiamua Uhuru na mwenzie wenye kesi wahukumiwe huku wakiwa washindi wa uraisi uchaguzi mwingine utaitishwa?nauliza tu wakuu
 

Kwa nini usikubali tu kwamba ulichopost hakikuwa sahihi? Au ukugundua kosa lako lilikuwa wapi? Na kwa nini unafikiri bado ninapashwa kubisha hata palipo na ukweli? Ukipost kilicho sahihi nitakubali, ukipost kisicho sahihi sitakubali.

Tiba
 
sasa mbona mambo ni yale yale? Au hackers wameingilia hadi manual work?

Hii ni kuihakikishia jamii ya kimataifa kuwa wanachofikiria wao sio kinachofikiriwa na wananchi na matwakwa yao sio matakwa ya wananchi na hii ni kwa nchi mbalimbali na katika kupunguza hasira zao utaona vikwazo vya kiuchumi na kuporomoshwa kwa shilingi ya Kenya ili kuwakomoa wakenya kuwa walifanya chakuo lisilo sahihi lakini. hawa vijana wanatakiwa wajitahidi sana na kama watawaona wamarekani na waingereza wanawazingua wao yajishikize na nchi za China,korea, south Amerca,Japani na Urusi, na kuongeza uhusiano na Mkubwa na Irani. basi hapo watatoboa tu. na wanatakiwa wakomae kama Mugabe mpaka sasa naona mwingereza kasilimu Amri anajirudisha mwenyewe.

Afrika inatakiwa tupate viongozi walio imara na wenye uwezo wa kusimama na kusimamia mataifa yao bila kuendeshwa na mataifa yaliendela

We angalia Umoja wa Afrika tangu nikiwa mtoto nausikia lakini sijui nini cha maana unafanya kila siku naona machafuko katika bara la Afrika na wanokuja kusaidia ni hayo mara utasikia sijui uropean union mara utasikia sijui marekani kumbe wao ndio wanasababisha machafuko katika bara hili kwasababu ya Rasilimali zilizoko.

Kwa kumchagua Uhuru kwangu Kenya watakuwa wamefanya chaguo sahihi kabisa kwani hawajamchagua mtu kwa kufwata shinikizo la kimataifa bali kwa kufwata utashi wao.

Na hata kama Uhuru atawaingiza kwenye matatizo ya kiuchumi kutokana na vikwazo vya kimataifa hiyo ni sawa kabisa ili waweze kutumia akili zao na Rasilimali zao katika kujikwamua na matatizo yaliyozoeleka katika bara hili, na wasirudi nyuma wala wasijilaumu kwa uchaguzi walioufanya kwani naamini kwa katiba yao utawala utakuwa bora na Raisi ataisimamia na kuilinda katiba na kutekeleza matakwa ya wakenya kwa kufwata katiba na ya kenya na si kwa kufwata matakwa ya wanyonyaji marekani na washirika wake.

MAY GOD OF MY HEART BLESS KENYA NA WATU WAKE, AMENI
 

Mkuu Mwakalinga, sijabishia matokeo halisi hata kidogo. Rudia kusoma alicho report huyo Bwana na pia rudia kusoma kwa makini my observations ndio utaelewa nilikuwa na maana gani. Sikuwa na maana ya kutokubali matokeo ya tume hata kidogo!!!

Tiba
 
Matokeo ya uchaguzi wa Kenya nani anaeongoza kwa kuwa na kura nyingi?
 
Mbona tofauti ya kura kwa manual inaelekea kuwa ile ile na ya digital? na imekaa mda mrefu. Ama software ya ku-manipulate kura na kuwa tofauti ya constant ya laki tano na sita imekuwa installed kwa hardware ya mikono ya wanaohesabu?

Wakenya dungu zangu kuweni makini na mataifa ya magharibi, hata hizo kura zinazosemakana kuharibika naaamini ni simulation tu ya wana-magharibi. Maana ni nyingi zaidi ya mara tatu ya wagombea sita wengine walizopata, walitegemea akina Mdavadi watakuwa na kura za kutosha ili 50+1 isifike, sasa wanachofanya ni kuharibu kura nyingi zaidi ili zipungue zaidi.
 
Mwana wa mfalme anazidi kukimbiza,hakamatiki,hili ni pigo kwetu wafuasi wa Raila
 
je ICC ikiamua Uhuru na mwenzie wenye kesi wahukumiwe huku wakiwa washindi wa uraisi uchaguzi mwingine utaitishwa?nauliza tu wakuu

Mkuu Eyoma kwa siasa za ukabila za Kenya Mungu tu ndiye ataweka mkono wake.
 
Last edited by a moderator:
Wakenya wanahasira sana na wamerekani kwani obama alipochaguliwa kuwa Raisi walikesha wakifurahia na walitarajia atawafanyia makubwa kinyume chake Obama hana muda nao na nchi yaki inaonekana kuwatishia kuchagua baadhi ya watu hivyo wanataka kuidhiirishia dunia kuwa kenya ni independent and sovereign state
 
je ICC ikiamua Uhuru na mwenzie wenye kesi wahukumiwe huku wakiwa washindi wa uraisi uchaguzi mwingine utaitishwa?nauliza tu wakuu

Mkuu Eyoma kwa siasa za ukabila za Kenya Mungu tu ndiye ataweka mkono wake.
 
Last edited by a moderator:
BBC dakika chache zilizopita wanasema CORD hawakubalian na matangazo ya tume kwa ivo wanajiandaa kwenda mahakaman kusimamisha zoez la manual count.
Ukweli nikwamba wao wameshajumlisha kura nchi nzima na wamegundua jamaa kashinda first round.
Angalia kwanza walisema et electronic count imeweka pamanent gap sasa wanasema matokeo ni doctored. Gap lipo palepale lak tano na ushee
Uhuru anaandaa ukumbu wa kutoa speech ya ushindi kesho mchana ingawa wenyewe (ruto) anasema watatoa spich hatakama wameshindwa.
,NOT YET UHURU
 

nasikia obama yuko kwa hot line na wale vijana wa kaz wako kazin nairob
 
Masuke,uko na evidence gani juu ya hii mambo? Mashtaka ya hii mambo iliandaliwa na Moreno Ocampo pamoja na timu ake. International Tribanal haiko na rushwa kama vile unavyodhani wewe,acha sheria ifwate njia ile iko na haki na siyo maneno ya urongo kama iyo,
 
Last edited by a moderator:

Anajiandaa kwenda mahakamani, hakubaliani na digital yani software na hakubaliani na hardcopy yani akili na mikono. Ha ha ha ha
Nafikiri ICC watagundua mtata ni nani ktk uchaguzi huu.
 
But remember around 40% of total votes tallied,so usisherekee mno, mambo ni bado
 
Mkuu inawezekana nisiwe na ushahidi wa kutosha kukuridhisha lakini akili ya kawaida inaniambia nijiulize wale wote sita waliotuhumiwa walikuwa na manufaa gani na zile fujo za baada ya uchaguzi, kwa sababu miongoni mwao hakuna aliyekuwa mgombea urais, wengi wao waligombe ubunge na tayari walikuwa wameshatangazwa washindi, waliokuwa na manufaa na zile fujo za baada ya uchaguzi ni wagombea urais waliokuwa wanabishana yaani Raila na Kibaki na ndo maana walivyokubaliana kugawana madaraka zile fujo zilikoma.

Hebu nieleze zile fujo za Kenya zilikuwa na tofauti gani na zile za Ivory Coast baada ya Gbagbo kung'ang'ania ushindi lakini baadaye akajikuta yuko Hague.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…