March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

na safari hii hakuna serikali ya mseto...so uhuru aanze biashara ya kuuza mirungi tu...

Shenz type

Nina hakika una maana Raila, hata hivyo yeye pamoja na vingine alishafisadi kiwanda ha Mollases hivyo hawezi uza miraa
 
wATU WANAKATA TAMAA MAPEMA SANA..AISEE

kama Raila na Kalonzo wenyewe wameshakata tamaa wewe unategemea nini kwetu sisi tulioko huku kwenye mitandao??

Kama hatujafika hata nusu wameshakimbili kwenye media wanaonyesha jinsi walivyo na washauri wabaya na hawapaswi kukabidhiwa nchi maana wanakurupuka na kuanza kuwachanganya watu kwa kuwaaminisha jambo ambalo pengine halipo kwakuwa kama wangekuwa na ushahidi kuwa wanaibiwa wangeuto kuliko kusema tu unaibiwa na kwakuwa Katiba inaruhusu wangeenda mahakamani na huo ushahidi basi saa hii ungekuta tunaongea tofauti na sioni sababu ya kuanza kupiga kelele mapema maana hata baada ya matokeo rasmi kutoka kwa mujibu wa katiba bado wananafasi ya kupinga matokeo sio kama hapa bongo.

Raila na Kalonzo walipaswa kuwa na hekima na busara ya hali ya juu na kuwaacha watu wa mitaani waonge hayo wanayoyoyaongea wao
 
Bado mapema mkuu Crashwise.

Swali langu kama bado ni mapema kwanini Raila na Kalonzo wanalalamika wakati wao walikuwa na wawakili kwenye kituo na hao wawakilishi wanamatokeo ni vile tu hawna mamla ya kuwatangazia umma???
kama wanaushahidi wa kuibiwa kura si waende mahakamani??
 
Last edited by a moderator:
Bado mapema mkuu Crashwise.


wakuu Crashwise, Arushaone, Consigliere, ukwelikitugani, Kenyan
Na je ni kweli kuwa kwa usabuji wa manual kura zilizoharibika zimeenda zikipungua kutoka idadi iliyotaja wakati wa kuhesabu digital??

hii ni kwamuji wa citize wamesema tume imetoa sababu ya kwanini kura zilizoharibika imepungua nasikila kwenye neti na inakatikati hivyo sikupata kusikila vizuri je kuna mmoja wenu ameipata hiyo
 
Last edited by a moderator:
Vipi pressure imeanza kupanda, naona gap la 700000 linazidi kupungua..

umesahau kuwa ni Raila aliyeanza kwa kuongoza na kuishia kupigwa hilo gap?
Ambalo hata hivyo in time litaongezeka kiasi cha kupelekea FORA wengi kujitoa na kususia kuchangia uzi huu.
 
Updates

UHURU KENYATTA

3,152,486


RAILA ODINGA
2,580,302
 
kitalolo,
Fungua hapa ujisomee taarifa kamili kuhusu "Visingizio vya IEBC, Ati Database bug caused the multiplication of rejected votes by 8..yaani ilikuwa inazidisha mara nane...Huu ni uhuni.
IEBC blames database bug for rejected votes error - Politics - nation.co.ke
 
Last edited by a moderator:
Napata shida sana kuelewa definition ya rejected votes. Hapa namnukuu Isaack Hassan "For any rejected vote for any candidate, they were being multiplied by eight," said the IEBC chairman.

Rejected vote inaweza vipi kuwa for a certain candidate?
 
Napata shida sana kuelewa definition ya rejected votes. Hapa namnukuu Isaack Hassan "For any rejected vote for any candidate, they were being multiplied by eight," said the IEBC chairman.

Rejected vote inaweza vipi kuwa for a certain candidate?
Huu ndo uhuni wenyewe wa IEBC.!! That was a hacking, period!!
 
KAMA SI MTAJI WA 'KURA 600,000 ZA KI-MALAIKA' RAILA ODINGA NDIYE ATAKUA AKIONGOZA KWENYE MATOKEO YA HIVI PUNDE KWA
KUMZIDI KENYATTA KURA 28,632

Naona ile fomula ya tofauti ya kura 600,000 (katika hesabu za yule anayesadikiwa kuongoza) iliotumika kule kwenye MATOKE YA KUPITIA KULE SAFARICOM yaliokataliwa na tume tena inaendelea kutumika hata sasa.

Kimsingi mtu ukitaka kujua matokeo sahihi kati ya wagombea hawa wa Kenya, kwanza kaondoe jumla ya kura laki 6 ndipo uanze kupiga mahesabu ya ki-ukweli.

Kwa mantiki hiyo, pale ambapo tumeambiwa ya kwamba vinara wawili hawa katika kinyang'anyiro cha kugombea urais hawa kura zao hadi sasa eti nikama ifuatavyo:

Licha ya kuripotiwa na Tume kwamba Uhuru Kenyatta amezoa 3,134,654 na Raila Odinga 2,563,286; mtu yeyote akijaribu tu kuondoa kwanza zile kura 600,000 zilizoingizwa ki-fomula ndipo utakapogundua kwamba kura za kikweli za Mhe Uhuru Kenyatta ni 2,534,654 dhidi ya zile za mpinzani wake wa karibu Raila Odinga zikisimama pale kwenye 2,563,286.

Naam, hadi hapo hii itakua na maana kwamba ni Raila Odinga ndiye atakayekua akiongoza kwa kumuacha nyuma kwa kura 28,632 hadi hivi sasa.


Great Thinkers, kidogo mtu akifanya udadisi makini utagundua ya kwamba kinachofanyika pale Bomas hadi hivi sasa ni ka-mchezo to mdogo tu kwenye Excel.

Sasa mtu ukijiuliza lengo hasa hapa utagundua ya kwamba Ikulu ya Rais Kibaki KATU HAITAKI KITU Marudio ya kupigiwa kura kati ya Kenyatta na Raila kwa kuwa wanakumbuka utafiti wa Synovet ilivyoelekeza ukweli mtupu.

Naam, mara baada ya mtu kujisumbua japo kidogo akilini kwa kuondoa tu zile kura 600,000 zilizopenyezwa hata kule kwenye MATOKEO YA KWENYE MAKARATASI KULE BOMAS hivi sasa utagundua ukweli ule ule waliouona watu wa Synoveta na watafiti wengine kibao nchini humo.

Ndio, kwa hesabu haka kadogo tu ya kuondoa kale ka 600,00 ya uongo ki-fomula mtu yeyote atagundua kwamba hadi hivi sasa anayestahili kuwa mbele katika hayo matokeo ya Nairobi hadi dakika hii ni Raila Odinga akiwa na kura 2,563,286 akifuatwa na Uhuru kwa kura 2,534,654 kukiwa kuna tofauti ndogo sana ya 28,632 peke yake.

Kimsingi ukiangalia hoja yangu hapo juu utagundua ya kwamba kule kuondoa kwanza zile 'KURA ZA KI-MALAIKA MICROSOFT EXCEL 600,000', hii njia ninayozungumzia hapa inakubaliana moja kwa moja na ukweli kwamba si Raila Odinga wala Uhuru Kenyatta atakayeweza kufikia asilimia 51% ya kura zote zilizopigwa nchini humo ila tu wawili hao wataalazimika kwenda kwenye ngwe ya pili ili rais wa kweli nchini humo aweze kupatikana.

Tofauti sana na hii hoja yangu hapa juu, kuna hatari kubwa wapiga kura wa Kenya wakaishia kumuingiza 'RAIS WA MICROSOFT EXCEL' ikulu. Jambo hilo likiruhusiwa kutokea basi kimahesabu za haraka haraka 'SERIKALI YA MICROSOFT EXCEL' itakayozaliwa kwa mtaji wa kura za kipaumbele 600,000 italazimika KUTUMIA GHARAMA KUBWA MNO kutafuta kujihalalisha kwa wananchi ambapo utabiri wangu unaona dalili za akina Dr Ulimboka wetu huyu, Absalom Kibanda kuibuka kule Nairobi kwa kasi kubwa ajabu.

Kikubwa siku zote ni HAKI KWANZA kisha huu wimbo wa AMANI utafuaata tu mkondo wake bila hata ya mtu yeyote kulazimika kupanga polisi kibao barabarani kwenda kuwaua raia kama anavyofanya hivi sasa huyu 'RAIS WETU WA EXCEL' pale Magogoni.
 
Mzee Jaramongi huko aliko hali tete. Aliukosa urais japo wa siku moja, mwanae anamfuatia?
 
Ndio mambo yenyewe hayo nadhani kura zitajulikana tu mwisho ni nn maana ya kura kuharibika na zina uwiano na kura zilizopigwa
 
Huu ndo uhuni wenyewe wa IEBC.!! That was a hacking, period!!

Mkuu ukwelikituganiwe ni mpenzi wa raila??

Naomba kuulizwa we kwa fikra zako unafikiri kwanini tume wanakuwa wahuni kwa kina Raila na sio kwa ma suspects?

Na kama kweli tume wamekuwa wahuni na kama kuna ushahidi kwanini tusiwapeleke mahakamani haraka kuzuia machafuko au mpaka watu waingie mtaani kwamba hakutakuwa tena na muda wa kwenye mahakamani
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…