March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

Kweli kabisa na ukabila kenya haujaanza leo ma wenyewe wanaona ni kawaida!

Nyinyi mnaoshangaa ukabila kwa sababu ni wageni wa siasa za Kenya. Maeneo pekee ambako hamna ukabila ni Mombasa na huko nako kuna udini instead of ukabila.

Hakuna mtu anayeshinda uchaguzi Kenya bila ukabila kama jinsi Bongo ilivyokuwa haiwezekani kushinda uchaguzi bila rushwa.
 
Uhuru kenyatta lazima aibuke kidedea!
16:05 Mr Kenyatta 2,664,462 (53.71%) against Mr Odinga's 2,072,596 (41.78%)......MAY GOD BLESS KENYA, GOD BLESS EAST AFRICA
 
nimejaribu kutafuta wastani wa matokeo hayo kwa kujumlisha asilimia za kila jimbo kwa kila mgombea na kutafuta wastani. Nimepata kuwa kama yanaakisi matokeo ya mwisho basi uhuru anaweza akashinda kwa asilimia 50.6 na Odinga anaweza kupata asilimia 45.2. hata hivyo, kwa kuwa matokeo yaliyotolewa kwenye link hiyo kwa kila jimbo yametolewa kwa asilimia lolote laweza kutokea kwa sababu matokeo ya asilimia sio lazima yaakisi matokeo ya kura mojamoja zikijumlishwa kwaa nchi nzima na kutafutiwa asilimia kwa pamoja. kwa mfano fikiria mgombea wx katika jimbo A amepata kura 80 kati ya 100 zilizopigwa sawa na 8o% na katika jimbo B amepata kura 0 kati ya kura 10 zilizopigwa sawa na 0%. Mgombea yz amepata kura 20 kati ya 100 zilizopigwa katika jimbo A sawa na 20% na katika jimbo B akapata kura zote kumi kati ya kumi zilizopigwa sawa na asilimia 100%. ukitumia kutafuta wastani kwa kutumia asilimi yz ndo mshindi. lakini ukijumlisha kura moja moja na kuatafuta asilimia wx ndio mshindi. kwa hiyo mgawanyo wa kura kama unavoonekana kwenye link hiyo inawza kuakisi matokeo ya mwisho au isiakisi. tungoje na kusubiri tume itoe matokeo.
 
ningependa kuona Odinga anashinda coz namkubali sana huyu mzee,but natambua pia kuwa ni jukumu la wakenya wenyewe kuamua mustakabali wa nchi yao.so wish u jiranis all the best.always stay on the safe side/amani idumu.

Huyo Jamaa ni Mjaluo, halafu unampenda, wewe ni Mtanzania kweli?
 
Hivi mkuu Tiba,wewe si uko hapo ,hakuna watu wanaolinda kura hapo?

Mkuu,

Ulinzi upo wa kutosha. Mbali ya askari wenye silaha, kuna waangalizi wa kimataifa na pia wawakilishi wa vyama hivyo sioni uwezekano wa kuiba kura unless zinatumika mbinu nyingine chafu na za kificho zaidi.

Tiba
 
hadi sasa kura 300,000 laki tatu zimeharibika kutokana na wananchi kutokua na elimu jinsi ya kupiga kura. Hii inaweza ikatia doa matokeo!. mia

Hapa haswa ndipo ilipofanya Kenyata kuwa na tofauti na Odinga.
 
kwa hiyo ili urizike, ulitaka wapiga kura wa Kenya wawe wale tu wasio na makabila?

mkuu Consigliere ukabila pembeni kwanza tuangalie sera za candidate mhusika,most voters in East Africa ukiwauliza kwanini unampenda mgombea fulani? atakujibu
1.ni mkristo/muislamu mwezangu
2.ni kabila la kwetu
3.nimetokea tu kumpenda
tunapiga kura kwa mazoea tu,hakika hata mm ningesimama nafasi ya Uhuru Kenyatta ningekuwa rais wa kenya jpokuwa sina sifa yoyote zaidi ya kabila
 
Hapa haswa ndipo ilipofanya Kenyata kuwa na tofauti na Odinga.

Haiwezi kutia doa maana ni sehemu ya matokeo. Walichosema ni kuwa percentages zinazoonyeshwa sizo maana lazima wajumlishe na zilizoharibika ili watafute asilimia kwa upya. Utagundua kuwa hii inapunguza % za Kenyata which seems to shrink towards 50% by time, verly likely kukawa na run off, very likely with the trend we are seeing
 
mkuu Consigliere ukabila pembeni kwanza tuangalie sera za candidate mhusika,most voters in East Africa ukiwauliza kwanini unampenda mgombea fulani? atakujibu
1.ni mkristo/muislamu mwezangu
2.ni kabila la kwetu
3.nimetokea tu kumpenda
tunapiga kura kwa mazoea tu,hakika hata mm ningesimama nafasi ya Uhuru Kenyatta ningekuwa rais wa kenya jpokuwa sina sifa yoyote zaidi ya kabila

Usiwalaumu voters. Kilichopo katika nchi yetu ni kwamba wapiga kura wana uzoefu wa kuona viongozi hawatekelezi ahadi zao. Kwa hiyo zile sera wanazozihubiri huwa ni sound tu za kuingia madarakani. Hata ukichagua kwa sera haisaidii kitu kwa sababu in the end yatakayofanywa ni mengine.

Ili watu wachague kwa kupima sera ni LAZIMA waamini kuwa sera zinazohubiriwa kwenye majukwaa ndizo zitakazotekelezwa.

Ukitaka kuthibitisha hili anzisha thread ya kuuliza Mnyika ametekeleza vipi ahadi zake? Utashambuliwa na watakaokushambulia watakwambia yale aliyoahidi sio jukumu lake kutekeleza!!!

Ndio maana watu wanachagua kwa preferences za jinsi wanavyojisikia karibu na mgombea either kwa urafiki, ujirani au sababu nyingine.
 
...Haa ha ha, Kalonzo Musyoka akizungumza na Wanahabari, akisema mpaka sasa ni 30% tu ya kura zimehesabiwa na kuwalaumu Jubilee kwa kuanza kusherehekea ushindi wakati eti hakuna anayejua ni nani kashinda mpaka kura zitakapokamilika, ukiisoma body language yake na ya James Orengo aliyekuwepo nyuma yake hautahitaji ushahidi wa IEBC kuwa tayari CORD wameshachinjiwa baharini...
 
Usiwalaumu voters. Kilichopo katika nchi yetu ni kwamba wapiga kura wana uzoefu wa kuona viongozi hawatekelezi ahadi zao. Kwa hiyo zile sera wanazozihubiri huwa ni sound tu za kuingia madarakani. Hata ukichagua kwa sera haisaidii kitu kwa sababu in the end yatakayofanywa ni mengine.

Ili watu wachague kwa kupima sera ni LAZIMA waamini kuwa sera zinazohubiriwa kwenye majukwaa ndizo zitakazotekelezwa.

Ukitaka kuthibitisha hili anzisha thread ya kuuliza Mnyika ametekeleza vipi ahadi zake? Utashambuliwa na watakaokushambulia watakwambia yale aliyoahidi sio jukumu lake kutekeleza!!!

Ndio maana watu wanachagua kwa preferences za jinsi wanavyojisikia karibu na mgombea either kwa urafiki, ujirani au sababu nyingine.
Nitolee mfano wa mbunge wa Tanzania aliyetekeleza ahadi zake na akarudi bungeni kwa sababu hiyo, na uniambie ni nani na ni ahadi gani hizo.

Nitolee pia mifano ya wabunge ambao wamekataliwa kwa kutotimiza ahadi zao.

Hivi Juma Kapuya, John Komba, Anna Makinda na Abas Mtemvu, walitekeleza ahadi gani mpaka wakachaguliwa tena kama si ushabiki wa CCM? Hata jukumu la uwakilishi wa watu wao unaweza kujivunia nini.

ZeMarcopolo, ukipenda chongo utaita kengeza.
 
Kama waliopiga kura ni 70% kwa maana ya milioni 10.
Na ambazo zimeshahesabiwa ni milion karibu sita,ina maana bado kura million 4 hazijahesabiwa.
Inaonekana uhuru anapiga bao hapa.
 
Usiwalaumu voters. Kilichopo katika nchi yetu ni kwamba wapiga kura wana uzoefu wa kuona viongozi hawatekelezi ahadi zao. Kwa hiyo zile sera wanazozihubiri huwa ni sound tu za kuingia madarakani. Hata ukichagua kwa sera haisaidii kitu kwa sababu in the end yatakayofanywa ni mengine.

Ili watu wachague kwa kupima sera ni LAZIMA waamini kuwa sera zinazohubiriwa kwenye majukwaa ndizo zitakazotekelezwa.

Ukitaka kuthibitisha hili anzisha thread ya kuuliza Mnyika ametekeleza vipi ahadi zake? Utashambuliwa na watakaokushambulia watakwambia yale aliyoahidi sio jukumu lake kutekeleza!!!

Ndio maana watu wanachagua kwa preferences za jinsi wanavyojisikia karibu na mgombea either kwa urafiki, ujirani au sababu nyingine.

Mkuu umenena vyema kabisa manake hata mie naangalia na kufatilia kwa karibu ahadi za mbunge wangu David Mathayo sioni Kilichotekelezwa....
 
Hawa wakenya nao vipi inakuwaje hadi sasa matokeo ya Nairobi bado?
 
Back
Top Bottom