Mkuu
MALCOM LUMUMBA njoo utie Baraka zako hapa
MWANZO:
Mkuu Mseza,
Urusi alifanya makosa makubwa sana kuuza Alaska lakini tusema tu kwamba alikuwa hana jinsi yoyote zaidi ya kufanya vile. Ikumbukwe Urusi imemuuzia Marekani Alaska
1867 lakini miaka
11 nyuma yani mwaka
1856 Urusi alipigana
Vita ya Crimea (CRIMEAN WAR) dhidi ya falme za
Ufaransa,
Uingereza na
Uturuki. Hili lilipelekea Urusi kushindwa vita, kuzorota kiuchumi hasahasa baada ya kunyanganywa majimbo yake muhimu yaliyo karibu na bahari nyeusi. Shughuli nyingi za kiuchumi nchini Urusi zilkwama hasahasa baada ya kuzuiwa kutumia bahari nyeusi kama hapo mwanzo. Urusi kuona anazidiwa ikabidi mwaka
1856 kusaini mkataba wa amani wa Paris (
Pact of Paris 1856) na hayo mataifa matatu ambapo Uingereza na Ufransa walimlalia sana. Kabla ya hivi vita Urusi ndiyo lilikuwa taifa lenye nguvu nyingi barani Ulaya kiasi cha kuwapa changamoto kubwa
Waingereza,
Waturuki,
Waprashia,
Waaustria na
Wafaransa hivyo huu ukawa ndiyo muda muafaka wa kummaliza kabisa hasimu wao. Hivyo basi baada ya Ufalme wa Uingereza kuona kwamba Ufalme wa Urusi umezorota kijeshi wakapanga mkakati madhubuti wa kuvamia majimbo yake muhimu likiwemo jimbo lake la
ALASKA kupitia nchi ya
CANADA ambayo huko nyuma ilikuwa koloni la Uingereza.
Muingereza angefanikiwa kufanya hivi basi ni dhahiri kabisa Ufalme wa Urusi usingeweza kulinda hilo jimbo la mbali kama tu alishindwa kulinda majimbo yake ya karibu kama
Sevastopol kwenye
Vita ya Crimea ya mwaka
1853-1856. Hivyo wakiwa wamechanganyikiwa wakaamua tu kuuza ili wapate faida yoyote kuliko kukosa kabisa, maana kama falme ya Uingereza ingefanikiwa kuivamia ALASKA hata zile hela ambazo Marekani alilipa sijui kama angepata. Ikumbukwe kwamba kipindi hiki Uingereza alikuwa anachuana na Urusi kwasababu Urusi alikuwa na ndoto ya kuvamia dola la Uturuki ili kufika Mashariki ya kati. Lakini Muingereza alihisi kama akiuachia Ufalme wa Urusi kufika Mashariki ya kati basi hawataishia hapo ni lazima tu wangefika India na Mashariki ya mbali ambapo Muingereza alikuwa na maslahi makubwa kiuchumi; hivyo ili kuzuia Urusi isikue zaidi akaamua kufanya fitna za kijeshi hasa kwenye sehemu zenye umuhimu mkubwa kiuchumi kwa ufalme wa Urusi.
Warusi baada ya kung'amua kwamba Uingereza ina mpango huo dhidi yake wakaamua kuwawahi mapema angalau wapate hata kitu kidogo kuliko kukosa kabisa. Walipeleka mawazo kwenye serikali ya Marekani na yakapokelewa kwa mikono miwili, tena wakafanya hadi na sherehe ya makabidhiano. Hivyo sheria ilitumika na wala hakuna kosa lolote japo Warusi wengi hadi leo wanaulalamikia sana ule mkataba.
Lakini kwanini Ufalme wa Urusi Uliamua kuizia Marekani pekee?
Sababu muhimu kabisa ni hizi zifuatazo hasa pale unaposoma historia ya Ulaya.
1.
Sababu za kimkatati- Marekani kuanzia mwaka 1783 hadi kufika 1945 ilikuwa inaendeshwa na sera kuu mbili kubwa ambazo waasisi wake waliziweke. Sera ya kwanza Inaitwa
THE MONROE DOCTRINE na
ISOLATION POLICY: Ambapo Monroe Doctrine ilikataza kwa nchi yoyote ile duniani kuingilia maslahi ya taifa la Marekani iwe ni barani Amerika Kaskazini au Amerika Kusini. Isolation Policy ilisema kwamba Marekani haifungamani na taifa lolote lile duniani hasa yale ya Ulaya hivyo itafanya biashara na kila taifa. Hii ilisaidia kuepusha migogoro na kukua haraka kiuchumi. Sasa Ulaya kulikuwa na sera inayotwa "
ULINGANIFU WA NGUVU" au "
THE EUROPEAN BALANCE OF POWER" ambapo mataifa makubwa ya Ulaya yalikuwa yanazuiana yasikue kiuchumi wala kijeshi kwasababu taifa moja lilikua sana kiasi cha kumzidi mwenzie ni lazima italeta matatizo na vurugu hivyo kupelekea vita baina yao. Marekani alikuwa siyo mfuasi wa hii sera hivyo basi Urusi akaona kwamba Uingereza au taifa lolote la Ulaya likipata ALASKA ni lazima litakuwa na uchumi mkubwa kutokana na rasilimali zake hivyo kuharibu "
ULINGANIFU WA NGUVU" au "
THE BALANCE OF POWER" barani Ulaya hivyo kimkakati akaamua kuiuzia Marekani taifa ambalo lilikuwa halifungamani na upande wowote na lisingeleta madhara.
2.
Sababu za Kibiashara na kibinadamu- Kwasababu Marekani hafungamani na taifa lolote ingekuwa rahisi sana kwa Urusi kuendelea kufanya biashara kwenye eneo lile bila kupata bugudha yoyote ile. Lakini kubwa zaidi ni usalama wa raisi wa kirusi waliokuwa Waorthodoksi ambao walianzisha makazi yao humo Alaska. Lakini kwasababu alikuwa na ugomvi na mataifa ya Ulaya basi
ALAKSA ingeangukia mikononi kwa Ufaransa au Uingereza ingeharibu
BALANCE OF POWER.
3.
Historia nzuri ya mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili- Wakati Marekani anadai uhuru kutoka kwa Uingereza kuna kipindi ya miaka ya 1700's Uingereza aliomba msaada wa kijeshi kutoka Urusi ili wakawapige waasi lakini Malkia wa Urusi Catherine The Great alikataa na akawaambia Warusi kwamba itakuwa na faida sana kwa Urusi kama Marekani itakuwa taifa huru hivyo kuleta ushirikiano Imara wa kibiashara na taifa hilo. Upande wa pili wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani 1861-1864 Urusi ilikuwa inafanya biashara sana na Marekani na pia ilikuwa inaitambua serikali ya Abraham Lincoln kama ndiyo halali wakati mataifa ya Ulaya yalikuwa yanafanya sana biashara na majimbo yalioasi ya nchi za kusini mwa Marekani. Hivyo niseme tu uhusiano wao ulikuwa mzuri na Urusi aliona angekuwa salama sana kutokana na haya mambo ambayo imewahi kuwafanyia Wamarekani katika nyakati zao za shida. Hivyo biashara zao, watu, pamoja na maslahi yao yaliyokuwepo yamebakia
ALASKA hata baada ya Mauzo yalikuwa kwenye mikono ya taifa salama la watu wanaoaminika.
HITIMISHO:
Kwa mtazamo wangu Makosa ambayo yamemfanya Marekani kuwa Kiranja wa dunia hii siyo hili la ALASKA pekee. Mataifa ya Ulaya yamechangia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na tathmini hafifu juu za siku za mbeleni. Mfano mwaka 1783 Marekani, Uingereza na Ufaransa walisaini mkataba wa Paris (
Paris Treaty of 1783) ambao kwa mara ya kwanza Uingereza alikubali kuitambua Marekani kama taifa huru na kuamua kusitisha vita vya Uhuru. Ufaransa alipigia debe sana Marekani kuwa nchi huru akitegemea kwamba baada ya hapo Marekani haiwezi kujitawala yenyewe hivyo isingefika mbali na angeitawala yeye. Lakini kwa bahati mbaya Ufaransa ilikosea Mahesabu kwasababu miaka sita tu baada ya huu Mkataba Mapinduzi ya Ufaransa (
French Revolution) ya mwaka
1789 yakaanza na Ufalme wa
Lous XVI uliokuwa na ndoto ya kutawala Marekani ukaanguka.
Upande wa pili Uingereza aliiacha Marekani iwe huru kwasababu aliogopa kwamba Marekani inaweza kuungana na mataifa kama Ufaransa na Uhispania ambayo ni hasimu kwake hivyo kupelekea yeye kupoteza majimbo mengi zaidi ya yale ambayo Ufaransa aliyasaidia Makoloni ya Marekani kumnyang'anya muingereza. Hivyo akaamua kukubali na kutoa eneo kubwa sana kwa serikali ya Marekani kwasababu asingefanya hivyo Marekani walikuwa wanataka kufika hadi
CANADA na kulifanya jimbo lao. Mwaka 1812-1814 hili lilithibitika kwenye Vita Vikali baina ya Uingereza na Marekani (
Anglo-American War 1812) Marekani alitaka kuingia
CANADA lakini alishindwa na matokeo yake
THE WHITE HOUSE ilichomwa moto yote; mataifa yote mawili yakaishia kusaini mkataba wa amani.
Wanahistoria wengi wanasema mkataba huu wa
Paris wa Mwaka
1783 ni moja kati ya mikataba mitano mikubwa na muhimu sana kuwahi kutokea, ambayo imebadilisha historia ya dunia mbali kabisa na Ule wa
Westphalia (Peace of Westphalia) wa mwaka
1648 au
Versailles (
Versailles Peace Treaty) wa
1919. Kwasababu huu mkataba usingefikiwa na taifa la
Ufaransa na
Uingereza wangeamua kukubaliana tu kuhusu mgawanyo wa maslahi huenda taifa la Marekani lingesambaratika au lisingekuwa kubwa kama ilivyo leo. Mfano mzuri wa hili ni kipindi cha (
MOROCCAN CRISIS 1905-1906) ambapo
Uingereza na
Ufaransa japo ni maadaui waliamua kuungana ili kumzuia
Mjerumani asitawale
Morocco au kipindi cha (
FASHODA INCEDENT 1898) ambapo Ufaransa alikubali kumuacha Muingereza achukue sehemu kubwa ya eneo la
MTO NILE WA MISRI kwasababu walikuwa wanazuia nguvu ya
Ujerumani ambalo ndilo lilikuwa taifa kubwa linalokua kwa kasi kipindi hicho. Hivyo kama wangeendelea kupigana wenyewe ni dhahiri wangemtengeneza
Mmarekani wa pili; na kama huu mkakati ungetumika
1783 basi
Marekani ingekuwa bado ni mali ya
Uingereza au
Ufaransa.