mpiga vichwa
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 2,376
- 3,811
Miaka minne mfululizo ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom ulielekea katika viunga vya mitaa ya msimbazi.
Kwa kipindi chote hicho Tumekuwa tukisikia malalamiko ya kila aina kutoka upande wa pili kwa watani zao Yanga kuwa simba inapendelewa na tff na Marefa hali iliyopelekea mtifuano mkubwa Kati ya tff na Yanga hadi kufikia Mashabiki wa Yanga kuibatiza tff jina tifua tifua na wale wa simba kuwaita Yanga Malalamiko fc.
Msimu huu tangu uanze kwa udhamini wa NBC na baadae mdhamini mwenza GSM hayo malalamiko hayapo tena badala yake marefa na tff ni kusifiwa kila kona na Mashabiki wa timu iliyokuwa mstari wa mbele katika ukosowaji .
Maswali ya kujiuliza ;
1.Je, mwaka huu marefa walipata mafunzo ya kutosha namna ya uchezeshaji hivyo wanazingatia sheria zote 17 za mpira wa miguu na upande huo unaridhika Sana na uwezo wa marefa? Au
2.Yanga walikuwa wanafahamu ukweli wa kikosi chao kwamba ni kibovu ila tff na marefa walikuwa wanaangushiwa tu jumba bovu?Au
3.Kwakuwa GSM ni miongoni mwa wadhamini wa ligi hiyo na vilevile ndiye mdhamini wao, ndiyo Maana Yanga hawalalamiki Maana wanajua miongoni mwa wagawa mkate baba naye yumo?
Nawasilisha. Majibu tafadhari.
Povu rukhusa .